Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
10 Hivyo tunaweza kuwatambua walio watoto wa Mungu na walio watoto wa Mwovu. Hawa ndiyo wasio watoto wa Mungu: Wale wanaotenda mambo yasiyo haki na wale wasiowapenda ndugu zao wa kike na wa kiume katika familia ya Mungu.
Ni lazima Tupendane Sisi kwa Sisi
11 Haya ni mafundisho mliyoyasikia toka mwanzo: Ni lazima tupendane sisi kwa sisi. 12 Msiwe kama Kaini. Aliyekuwa upande wa Mwovu. Kaini alimwua ndugu yake. Lakini kwa nini alimwua? Ni kwa sababu alichokifanya Kaini kilikuwa cha kiovu, na alichokifanya nduguye kilikuwa cha haki.
13 Kaka zangu na dada zangu, msishangae watu wa dunia hii wakiwachukia. 14 Tunafahamu ya kuwa tumevuka kutoka mautini na kuingia uzimani. Tunafahamu hili kwa sababu tunapendana sisi kwa sisi kama ndugu wa kike na wa kiume. Yeyote asiyewapenda kaka zake na dada zake angali amekufa. 15 Kila anayemchukia nduguye anayeamini ni muuaji. Nanyi mnajua kuwa hakuna muuaji aliye na uzima wa milele.
16 Hivi ndivyo tunavyojua jinsi upendo wa kweli ulivyo: Yesu aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Hivyo nasi tunapaswa kuyatoa maisha yetu, kwa ajili ya ndugu wa kike na wa kiume katika familia ya Kristo.
© 2017 Bible League International