Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Complementary)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with thematically matched Old and New Testament readings.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waebrania 11:1-3

Imani

11 Imani inaleta uthabiti wa mambo tunayoyatarajia. Ni uthibitisho wa yale tusiyoweza kuyaona. Mungu alifurahishwa na watu walioishi muda mrefu uliopita kwa sababu walikuwa na imani ya namna hii.

Imani hutusaidia sisi kufahamu kwamba Mungu aliumba ulimwengu wote kwa amri yake. Hii inamaanisha kwamba vitu tunavyoviona viliumbwa kwa kitu kisichoonekana.

Waebrania 11:8-16

Mungu alimwita Ibrahimu kusafiri kwenda sehemu ingine aliyoahidi kumpa. Ibrahimu hakujua hiyo sehemu ingine ilikuwa wapi. Lakini alimtii Mungu na akaanza kusafiri kwa sababu alikuwa na imani. Ibrahimu akaishi katika nchi ambayo Mungu aliahidi kumpa. Akaishi humo kama mgeni tu asiyekuwa mwenyeji. Alifanya hivi kwa sababu alikuwa na imani. Akaishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, ambao pia walipokea ahadi ile ile kutoka kwa Mungu. 10 Ibrahimu alikuwa anaungoja mji[a] ambao ulikuwa na misingi halisi. Alikuwa anaungoja mji ulibuniwa na kujengwa na Mungu.

11 Sara hakuwa na uwezo wa kupata watoto, na Ibrahimu alikuwa amezeeka sana. Lakini alikuwa anamwamini Mungu, akimwamini kuwa anaweza kutenda yale aliyoahidi. Hivyo Mungu akawawezesha kupata watoto. 12 Ibrahimu alikuwa amezeeka sana karibu ya kufa. Lakini kupitia kwa mtu huyo mmoja vikaja vizazi vingi kama zilivyo nyota za angani. Hivyo watu wengi wakaja kutoka kwake wakiwa kama punje za mchanga katika ufukwe wa bahari.

13 Watu hawa wote mashuhuri wakaendelea kuishi kwa imani hadi walipofariki. Hawakuwa wamepata mambo ambayo Mungu aliwaahidi watu wake. Lakini walikuwa na furaha kuona tu kwamba ahadi hizi zilikuwa zinakuja kwa mbali siku zijazo. Waliukubali ukweli kwamba wao walikuwa kama wageni na wasafiri hapa duniani. 14 Watu wanapolikubali jambo la namna hiyo, wanaonesha kuwa wanaingojea nchi itakayokuwa yao wenyewe. 15 Kama wangekuwa wanaifikiria nchi walikotoka, wangekuwa wamerejea. 16 Lakini walikuwa wanaingoja nchi iliyo bora zaidi, nchi ya mbinguni. Hivyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao. Naye amewaandalia mji.

Luka 12:32-40

Msitumainie Fedha

32 Msiogope, enyi kundi dogo. Kwa kuwa imempendeza Baba yenu kuwapa ninyi ufalme wake. 33 Uzeni vitu mlivyo navyo, wapeni fedha wale wanaohitaji. Hii ni njia pekee mnayoweza kufanya utajiri wenu usipotee. Mtakuwa mnaweka hazina isiyoisha mbinguni, mahali ambapo wezi hawawezi kuiba na hakuna wadudu wa kuharibu. 34 Kwa kuwa mahali ilipo hazina yako, ndipo roho yako itakapokuwa.

Iweni Tayari Daima

(Mt 24:42-44)

35 Iweni tayari! Vaeni kikamilifu na taa zenu zikiwaka. 36 Iweni tayari kama watumishi wanaomngojea bwana wao anayerudi kutoka kwenye sherehe ya harusi. Bwana wao anaporudi na kubisha mlangoni, watumishi huweza kumfungulia mlango haraka. 37 Bwana wao atakapoona kuwa wako tayari na wanamsubiri, itakuwa siku ya furaha kwa watumishi hao. Ninawaambia bila mashaka, bwana wao atavaa nguo, atawakaribisha kwenye chakula kisha atawahudumia. 38 Watumishi hao wanaweza kumsubiri bwana wao mpaka usiku wa manane. Lakini watafurahi sana kwa sababu aliporudi aliwakuta bado wanamsubiri.

39 Mwenye nyumba angefanya nini ikiwa angejua ni lini mwizi atakuja? Mnajua kuwa asingeruhusu mwizi akavunja na kuingia ndani. 40 Hivyo, iweni tayari ninyi nanyi, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja wakati msiotarajia!”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International