Revised Common Lectionary (Complementary)
Huwezi Kuwatumikia Mabwana Wawili
(Lk 12:33-34; 11:34-36; 16:13)
19 Msijiwekee hazina hapa duniani, mahali nondo na kutu[a] huiharibu. Na wezi wanaweza kuvunja nyumba yako na kuziiba. 20 Badala yake jiwekeeni hazina mbinguni ambako haziwezi kuharibiwa na nondo wala kutu na ambako wezi hawawezi kuvunja na kuziiba. 21 Kwa kuwa roho yako itakuwa mahali ilipo hazina yako.
22 Jinsi unavyowaangalia watu wengine ndivyo inavyoonyesha jinsi wewe mwenyewe ulivyo ndani yako. Ukiwaangalia watu kwa nia njema utajawa na nuru ndani yako. 23 Lakini ukiwaangalia watu kwa nia mbaya, utajawa na giza ndani yako. Na ikiwa yote yanayoonekana ndani yako ni giza peke yake, basi unalo giza baya zaidi![b]
24 Hamwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Mtamchukia mmoja na kumpenda yule mwingine au mtakuwa waaminifu kwa mmoja na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na pesa.[c]
© 2017 Bible League International