Revised Common Lectionary (Complementary)
Utu Wenu Mpya Mkiwa Nyumbani
18 Wake, muwe radhi kuwatumikia waume zetu. Ni jambo sahihi kufanya katika kumfuata Bwana.
19 Waume wapendeni wake zenu na msiwe na hasira nao.
20 Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote. Hili humfurahisha Bwana.
21 Wababa, msiwakorofishe watoto wenu, mkiwa wagumu kupendezwa nao; wanaweza kukata tamaa.
22 Enyi watumwa, watiini mabwana zenu katika mambo yote. Mwe watii kila wakati, hata kama wao hawawezi kuwaona. Msijifanye kazi kwa bidii ili wawatendee mema. Mnapaswa kuwatumikia mabwana[a] zenu kwa moyo kwa sababu mna hofu ya Bwana. 23 Kila kazi mnayoifanya, ifanyeni kwa bidii. Fanyeni kama mnamfanyia Bwana wenu wa mbinguni, na si kama mnamfanyia bwana wa dunia hii. 24 Mnajua kwamba mtapokea kutoka kwa Bwana ujira aliowaahidi watu wake. Ndiyo, mnamtumikia Kristo aliye Bwana[b] wenu halisi. 25 Kumbukeni kuwa Mungu hana upendeleo; kila afanyaye uovu ataadhibiwa kwa sababu ya uovu wake.
4 Enyi mabwana, wapeni kilicho chema na chenye haki watumwa wenu. Kumbukeni kuwa Mkuu wenu yuko mbinguni.
© 2017 Bible League International