Revised Common Lectionary (Complementary)
Uhai Wenu Mpya
3 Mlifufuka pamoja na Kristo kutoka kwa wafu. Hivyo ishini maisha mapya, mkiyatazamia yaliyo mbinguni, ambako Kristo ameketi mkono wa kulia wa Mungu. 2 Msiyafikirie yaliyo hapa duniani bali yaliyo mbinguni. 3 Utu wenu wa kwanza umekufa, na utu wenu mpya umetunzwa na Kristo katika Mungu. 4 Kristo ndiye utu wenu mpya sasa, na atakaporudi mtashiriki katika utukufu wake.
5 Kwa hiyo kiueni chochote kilicho cha kidunia kilichomo ndani yenu: uasherati, matendo machafu, mawazo na tamaa mbaya. Msijitakie na kujikusanyia vitu vingi, kwani ni sawa na kuabudu mungu wa uongo. 6 Mungu ataionyesha hasira yake kwa wale wasiomtii,[a] kwa sababu ya maovu wanayotenda. 7 Ninyi pia mlifanya maovu haya huko nyuma, mlipoishi kama wao.
8 Lakini sasa, jitengeni mbali na mambo haya katika maisha yenu: hasira, ukorofi, chuki, na mazungumzo yenye matusi. 9 Msiambiane uongo ninyi kwa ninyi. Ninyi mmeyavua mavazi ya kale; utu wa kale mliokuwa nao na matendo mabaya mliyotenda hapo awali. 10 Na sasa mmevaa utu mpya unaofanywa upya kila siku hata kuufikia ufahamu kamili wa Kristo. Mfano wenu wa maisha mapya ni Kristo, aliye mfano na sura ya Mungu aliyewaumba ninyi. 11 Katika utu huu mpya haijalishi ikiwa wewe ni Myunani au Myahudi, umetahiriwa au hujatahiriwa. Haijalishi pia ikiwa unazungumza lugha tofauti au hata kama wewe ni mtu asiyestaarabika,[b] ikiwa ni mtumwa ama mtu huru. Kristo ndiye wa muhimu zaidi, naye yumo ndani yenu ninyi nyote.
Yesu Aaonya Kuhusu Ubinafsi
13 Mmoja wa watu katika kundi akamwambia Yesu, “Mwalimu, baba yetu amefariki hivi karibuni na ametuachia vitu, mwambie kaka yangu anigawie baadhi ya vitu hivyo!”
14 Lakini Yesu akamwambia, “Nani amesema mimi ni mwamuzi wa kuwaamulia namna ya ninyi wawili kugawana vitu vya baba yenu?” 15 Ndipo Yesu akawaambia, “Iweni waangalifu na jilindeni dhidi ya kila aina ya ulafi. Maana uhai wa watu hautokani na vitu vingi wanavyomiliki.”
16 Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Alikuwepo tajiri mmoja aliyekuwa na shamba. Shamba lake lilizaa mazao sana. 17 Akasema moyoni mwake, ‘Nitafanya nini? Sina mahali pa kuyaweka mazao yangu yote?’
18 Kisha akasema, ‘Ninajua nitakachofanya. Nitabomoa ghala zangu na kujenga ghala kubwa zaidi! Nitahifadhi nafaka zangu zote na vitu vingine vizuri katika ghala zangu mpya. 19 Kisha nitajisemea mwenyewe, nina vitu vingi vizuri nilivyotunza kwa ajili ya kutumia kwa miaka mingi ijayo. Pumzika, kula, kunywa na furahia maisha!’
20 Lakini Mungu akamwambia yule mtu, ‘Ewe mpumbavu! Leo usiku utakufa. Sasa vipi kuhusu vitu ulivyojiandalia? Nani atavichukua vitu hivyo?’
21 Hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mtu anayeweka vitu kwa ajili yake yeye peke yake. Mtu wa namna hiyo si tajiri kwa Mungu.”
© 2017 Bible League International