Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Isa for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
1 Wakorintho 2:1-13

Ujumbe Wangu: Yesu Kristo Msalabani

Wapendwa kaka na dada zangu katika Kristo, nilipokuja kwenu, niliwaambia siri ya kweli iliyofunuliwa na Mungu. Lakini sikuja kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongea au mwenye hekima ya juu. Nilipokuwa pamoja nanyi, niliamua kusahau kila kitu isipokuwa Yesu Kristo na kifo chake msalabani. Nilipokuja kwenu nilikuwa mdhaifu na mwenye hofu. Mafundisho na kuzungumza kwangu hakukuwa kwa maneno yenye hila. Lakini uthibitisho wa mafundisho yangu ilikuwa nguvu inayotolewa na Roho. Nilifanya hivi ili imani yenu iwe katika nguvu ya Mungu siyo katika hekima ya kibinadamu.

Hekima ya Mungu

Tunafundisha hekima kwa watu ambao macho yao yamefunguliwa ili waione hekima ya siri ya Mungu. Si hekima ya watawala wa ulimwengu huu wanaobatilika. Tunaisema hekima ya Mungu katika namna ambayo baadhi wanaweza kuiona na wengine hawawezi. Ni hekima iliyofichwa mpaka wakati huu na Mungu aliipanga hekima hii kabla ya kuumba ulimwengu, kwa ajili ya utukufu wetu. Hakuna mtawala yeyote wa ulimwengu huu aliyeielewa hekima hii. Ikiwa wangeielewa, wasingemwua Bwana wetu mkuu na mwenye utukufu mwingi msalabani. Lakini kama Maandiko yanavyosema,

“Hakuna aliyewahi kuona,
    hakuna aliyewahi kusikia,
hakuna aliyewahi kufikiri
    kuhusu kile ambacho Mungu amewaandalia wanaompenda.”(A)

10 Lakini Mungu ametuonesha mambo haya kupitia Roho.

Roho anaweza kuchunguza mambo yote. Anajua hata siri za ndani kabisa za Mungu. 11 Hakuna mtu anayejua mawazo ya mtu mwingine. Ni roho inayoishi ndani ya mtu huyo ndiyo inajua mawazo ya mtu huyo. Ndivyo ilivyo hata kwa Mungu, ni Roho wa Mungu peke yake ndiye anayeyajua mawazo ya Mungu. 12 Tulipokea Roho wa Mungu, si roho wa ulimwengu. Tulimpokea Roho wa Mungu ili tuweze kujua yote aliyotupa Mungu.

13 Tunapozungumza, hatutumii hoja tulizofundishwa na wenye hekima. Bali hoja tulizofundishwa na Roho. Tunatumia hoja za Roho kuelezea kweli za Roho.

Yohana 14:21-29

21 Wale wanaonipenda kweli ni wale ambao si tu kwamba wanazijua amri zangu bali pia wanazitii. Baba yangu atawapenda watu wa jinsi hiyo, nami pia nitawapenda. Nami nitajitambulisha kwao.”

22 Kisha Yuda (siyo Yuda Iskariote) akasema, “Bwana, utawezaje kujitambulisha kwetu, lakini si kwa ulimwengu?”

23 Yesu akajibu, “Wale wote wanipendao watayafuata mafundisho yangu. Naye Baba yangu atawapenda. Kisha Baba yangu na mimi tutakuja kwao na kukaa pamoja nao. 24 Lakini yeyote asiyenipenda hafuati mafundisho yangu. Mafundisho haya mnayosikia kwa hakika siyo yangu. Ni kutoka kwa Baba yangu aliyenituma.

25 Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi. 26 Lakini yule Msaidizi atawafundisha kila kitu na kuwafanya mkumbuke kila nilichowaambia. Huyu Msaidizi ni Roho Mtakatifu[a] ambaye Baba atamtuma kwa jina langu.

27 Nawaachia amani. Ninawapa amani yangu mwenyewe. Ninawapa amani kwa namna tofauti kabisa na jinsi ulimwengu unavyofanya. Hivyo msihangaike. Msiogope. 28 Mlinisikia nikiwaambia, ‘Naondoka, lakini nitakuja tena kwenu.’ Mngenipenda, mngefurahi kuwa naenda kwa Baba, kwa sababu Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Nawaambia haya hivi sasa, kabla hayajatokea. Kisha yatakapotokea, mtaamini.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International