Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Sir for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 12:25-13:3

25 Baada ya Barnaba na Sauli kumaliza kazi yao Yerusalemu, walirudi Antiokia, walimchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.

Barnaba na Sauli Wapewa Kazi Maalum

13 Walikuwepo baadhi ya manabii na walimu katika kanisa la Antiokia. Walikuwa Barnaba, Simeoni (ambaye pia aliitwa Nigeri[a]), Lukio (kutoka mji wa Kirene), Manaeni (aliyekua pamoja na Mfalme Herode[b]), na Sauli. Watu hawa wote kwa pamoja walikuwa wanamwabudu Bwana na wamefunga Roho Mtakatifu alipowaambia, “Nitengeeni Barnaba na Sauli ili wanifanyie kazi maalumu. Wao ndio niliowachagua kuifanya kazi hiyo.”

Hivyo kanisa lilifunga na kuomba. Wakaweka mikono yao juu ya Barnaba na Sauli, wakaagana nao na kuwaacha waende.

Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Timotheo 4:1-11

Nakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, ambaye punde atawahukumu wale walio hai na wale waliokwisha kufa na juu ya kuja kwa mara ya pili kwa Kristo kwa sababu kwa hakika atatokea kuja kutawala kama Mfalme: Hubiri Ujumbe, uwe tayari kutimiza wajibu wako wakati ulio sahihi hata ule usio sahihi. Wathibitishie watu kwa wanafanya makosa na uwaonye juu ya yale yatakayowatokea. Ufanye hivi kwa subira kubwa na tahadhari katika yale unayofundisha.

Nasema hivi kwa sababu utakuja wakati ambapo watu hawatakuwa tayari kuyasikiliza mafundisho yenye uzima. Badala yake watawatafuta walimu wanaowapendeza. Watawatafuta walimu wanaosema yale wanayotaka kusikia. Na watayageuzia mbali masikio yao kutoka kwenye kweli na kugeukia simulizi za uongo. Lakini wewe ujizuie mwenyewe katika mambo yote; vumilia mateso; fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema; ifanye huduma uliyopewa na Mungu.

Kwangu mimi, nimemiminwa kama kinywaji cha sadaka, na wakati wa kuondoka kwangu kutoka katika maisha haya umekwisha kufika. Nimejihusisha katika mashindano ya thamani; nimemaliza mbio; nimeilinda imani. Sasa tuzo ya mshindi inaningoja, hii ni taji inatolewa kwa wenye haki. Bwana, aliye hakimu wa haki atanipa taji hiyo katika Siku ile. Ndio atanipa mimi na yeyote mwingine anayengojea kwa dhati kuja kwake.

Maelezo Binafsi

Jitahidi kuja kuniona mapema uwezavyo, 10 kwani Dema aliniacha kwa sababu aliupenda ulimwengu wa sasa na ameenda Thesalonike. Kreske ameenda Galatia, na Tito ameenda Dalmatia. 11 Luka ni peke yake aliyebaki nami. Mchukue Marko na uje naye utakapokuja, kwa sababu anaweza kunisaidia katika kazi yangu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International