Book of Common Prayer
Msiwaruhusu Watu Wenu Waishi Katika Dhambi
5 Sitaki kuyaamini yale ninayosikia, ya kwamba kuna uzinzi katikati yenu. Na ni aina mbaya ya uzinzi ambayo hata wasiomwamini Mungu wetu hawauruhusu. Watu wanasema kuwa huko kwenu kuna mtu anayetenda dhambi ya zinaa na mke wa baba yake. 2 Na mna kiburi! Mngepaswa kuwa na huzuni badala yake. Na mtu aliyetenda dhambi hiyo ilipaswa kuwa amefukuzwa kutoka katika kundi lenu. 3 Siwezi kuwa hapo pamoja nanyi ana kwa ana, lakini niko pamoja nanyi katika roho. Na nimekwisha mhukumu mtu aliyetenda hii kama ambavyo ningemhukumu ikiwa ningekuwa hapo. 4 Nanyi pia mnapaswa kufanya vivyo hivyo. Kusanyikeni pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu. Nitakuwa pamoja nanyi katika roho, na nguvu ya Bwana Yesu itakuwa pamoja nanyi. 5 Mtoeni mtu huyu kwa Shetani ili tabia yake ya kujisifu[a] iangamizwe lakini mtu mwenyewe na kanisa, lilojazwa Roho, liweze kuokolewa siku Bwana atakaporudi.
6 Kujisifu kwenu si kuzuri. Mnajua msemo unaosema, “Chachu kidogo huchahua donge zima.” 7 Ondoeni chachu ya zamani ili muwe donge jipya. Ninyi kwa hakika ni mkate usio na chachu, mkate wa Pasaka,[b] Ndiyo, Kristo aliye Mwanakondoo wetu wa Pasaka[c] amekwisha usawa. 8 Hivyo na tuule mlo wetu wa Pasaka, lakini si pamoja na mkate wenye chachu ya zamani, yaani dhambi na matendo mabaya. Lakini tule mkate usio na chachu. Huu ni mkate wenye ukweli na chachu njema.
19 na Yuda Iskariote,[a] ambaye ndiye aliyemsaliti Yesu.
Nguvu ya Yesu Inatoka kwa Mungu
(Mt 12:22-32; Lk 11:14-23; 12:10)
20 Kisha Yesu akaenda nyumbani. Kwa mara nyingine tena umati wa watu ukakusanyika, kiasi kwamba Yesu na wanafunzi wake hawakupata nafasi ya kula. 21 Familia ya Yesu ilipoyasikia haya, walikwenda kumchukua kwa sababu watu walisema amerukwa na akili.
22 Walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikuwa wanasema, “Yeye ana Beelzebuli[b] ndani yake! Kwani anafukuza mashetani kwa nguvu ya mkuu wa mashetani!”
23 Yesu akawaita na kuanza kuzungumza nao kwa kulinganisha: “Inawezekanaje Shetani ambaye ni roho mchafu kufukuza mashetani? 24 Ikiwa basi ufalme utagawanyika katika sehemu mbili zinazopingana zenyewe kwa zenyewe, ufalme huo hautaendelea. 25 Vivyo hivyo ufalme wa Shetani ukigawanyika naye akapigana dhidi ya pepo wake wabaya, basi huo utakuwa ndio mwisho wa ufalme wake. Pia ikiwa nyumba itapingana yenyewe kwa yenyewe, nyumba hiyo haitaweza kusalimika. 26 Kwa hiyo ikiwa Shetani atajipinga mwenyewe na kugawanyika basi hataweza kuendelea na huo utakuwa mwisho wake.
27 Hakika, hakuna anayeweza kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuzichukua mali zake bila kwanza kumfunga mtu huyo mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kuiba katika nyumba hiyo.
28 Ninawaambia ukweli: Watu wanaweza kusamehewa dhambi zao zote na maneno yao yenye matusi kwa Mungu. 29 Lakini yeyote atakayemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa kabisa. Kwa sababu mtu anayefanya hivyo atakuwa na hatia ya dhambi isiyosamehewa milele.”
30 Yesu alisema haya kwa sababu walimu wa sheria walikuwa wanasema, “Yeye ana pepo mchafu ndani yake.”
Wafuasi wa Yesu ni Familia Yake Halisi
(Mt 12:46-50; Lk 8:19-21)
31 Kisha mama yake Yesu na nduguze wakaja. Wao walisimama nje na wakamtuma mtu aende kumwita ndani. 32 Humo lilikuwepo kundi lililoketi kumzunguka, lakini wao wakamwambia, “Tazama! Mama yako, kaka zako na dada zako wako[c] nje wanakusubiri.”
33 Yesu akauliza, “Mama yangu ni nani na kaka zangu ni akina nani?” 34 Yesu akawatazama wale walioketi kumzunguka na akasema “Hapa yupo mama yangu na wapo kaka zangu na dada zangu! 35 Yeyote anayeyafanya mapenzi ya Mungu ndiye kaka yangu, dada yangu, na mama yangu.”
© 2017 Bible League International