Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Wakorintho 10:1-18

Mafundisho Kutoka Historia Ya Wayahudi

10 Nataka mkumbuke ndugu zangu, kwamba baba zetu wote wali kuwa wakiongozwa na wingu, na wote walipita katikati ya bahari ya Shamu. Wote walibatizwa kama wafuasi wa Musa katika lile wingu na ndani ya ile bahari. Wote walikula kile chakula cha kiroho, na wote walikunywa kile kinywaji cha kiroho. Kwa maana waliku nywa kutoka katika ule mwamba wa kiroho uliofuatana nao; na mwamba huo ulikuwa ni Kristo. Hata hivyo Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo maiti zao zilitapakaa jangwani.

Basi mambo haya ni onyo kwetu, tusitamani uovu kama wao walivyofanya. Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyofa nya. Kama Maandiko yasemavyo, “Watu walikaa chini wakala na kunywa, kisha wakainuka kucheza.” Wala tusifanye uasherati kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. Pia tusimjaribu Bwana, kama wengine walivyofa nya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msilalamike, kama wengine walivyofanya, wakaangamizwa na malaika wa kifo.

11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wen gine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.

12 Kwa hiyo mtu anayejidhania kwamba anasimama, awe na tahadhari asije akaanguka. 13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

14 Kwa hiyo rafiki zangu, msishiriki katika ibada za sanamu. 15 Nasema nanyi kama na watu wenye ufahamu. Amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16 Je? Kikombe cha baraka ambacho tuna kibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Na mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa kuna mkate mmoja, sisi tulio wengi, tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki mkate mmoja. 18 Fikirini kuhusu Waisraeli, je, Wanaokula kilichotolewa sadaka hawashiriki katika madhabahu?

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica