Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Warumi 11:19-36

19 Pengine mtasema, “Matawi yalikatwa ili nipate nafasi ya kupandikizwa katika shina.” 20 Hii ni kweli. Lakini kumbuka kuwa matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini; na wewe umesimama imara kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijisifu, bali ujinyenyekeze na kuogopa. 21 Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, hatakuacha wewe, atakuondoa. 22 Tafakari basi kuhusu wema na ukali wa Mungu. Yeye ni mkali kwa wale walio anguka, bali amekuonyesha wewe wema wake, kama utadumu katika wema wake. Vinginevyo, na wewe utakatiliwa mbali. 23 Na hata hao Waisraeli, kama wakiacha kudumu katika kutokuamini kwao, atawar udisha kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwarejesha. 24 Ikiwa ninyi mmekatwa kutoka katika mizeituni mwitu, na ki nyume cha asilia mkapandikizwa kwenye mzeituni uliopandwa, ita kuwa ni rahisi kiasi gani matawi haya ya asili kurejeshwa kwenye shina lake?

Huruma Ya Mungu Ni Kwa Wote

25 Ndugu zangu, napenda mfahamu siri hii, msije mkaanza kujiona. Waisraeli wamekuwa na mioyo migumu kwa kiasi fulani mpaka idadi kamili ya watu wa mataifa mengine watakapoamini. 26 Na ndipo Waisrael wote wataokoka kama ilivyoandikwa, “Mko mbozi atakuja kutoka Sayuni, na kuuondoa uasi wote kutoka katika uzao wa Yakobo. 27 Na hii itakuwa ni agano langu nao, nitakapoondoa dhambi zao.”

28 Basi Waisraeli ni maadui wa Mungu kwa sababu ya Injili. Hii ni kwa faida yenu. Lakini kuhusu uchaguzi, Waisraeli bado ni wapendwa wa Mungu kwa sababu ya ahadi yake kwa Abrahmu, Isaki na Yakobo. 29 Kwa maana karama za Mungu na wito wake hazifutiki. 30 Kama ninyi zamani mlivyokuwa mmemwasi Mungu na sasa mmepokea rehema kwa sababu ya kutokutii kwao, 31 hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi kwa ajili ya rehema mliyopata kutoka kwa Mungu, ili wao pia wapate rehema. 32 Kwa maana Mungu amewaachia wana damu wote wawe katika uasi, ili aweze kuwahurumia wote.

Wimbo Wa Shukrani

33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachu nguziki! 34 Kwa maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake? 35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe? 36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu kwake. Utukufu ni wake milele. Amina.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica