Old/New Testament
Huduma Ya Paulo Kwa Mataifa
14 Mimi nimeridhika ndugu zangu kuwa ninyi mmejaa wema, mnao ufahamu wote, tena mnaweza kujengana. 15 Lakini kuhusu mambo fulani nimewaandikia kwa ujasiri nikiwa na shabaha ya kuwa kumbusha kwa sababu Mungu amenipa neema maalumu. 16 Amenichagua kuwa mtumishi wa Kristo Yesu kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu, nitoe huduma ya kikuhani kwa kuitangaza Injili ya Mungu, ili watu wa mataifa wawe sadaka inayokubaliwa na Mungu na iliy otakaswa na Roho Mtakatifu.
17 Kwa hiyo nina sababu ya kujisifu ndani ya Kristo kwa huduma yangu kwa Mungu. 18 Hata sitasema juu ya jambo lo lote isipokuwa katika yale tu ambayo Kristo mwenyewe ameyafanikisha kwa kunitumia, katika maneno na matendo yangu, akawavuta watu wa mataifa wamtii akitumia 19 nguvu za ishara na miujiza, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kuanzia Yerusalemu mpaka kando kando ya Iliriko nimekwisha kuhubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu. 20 Shabaha yangu imekuwa nisihubiri mahali ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwin gine. 21 Lakini kama ilivyoandikwa, “Wale ambao hawajaambiwa habari zake, wataona na wale ambao hawajasikia wataelewa.”
Paulo Apanga Kwenda Roma
22 Hii ndio sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.
23 Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimetamani sana kuja kwenu, 24 natu maini kuwaona nikiwa safarini kwenda Spania, nifurahi kwa muda pamoja nanyi, kisha mnipatie msaada kwa safari hiyo. 25 Ila sasa nakwenda kupeleka msaada kwa watu wa Mungu walioko Yerusalemu. 26 Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yameamua kutoa mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu wasiojiweza walioko huko Yerusalemu. 27 Wamependa kufanya hivyo lakini kwa kweli ni wajibu wao, maana kama watu wa mataifa mengine wameshiriki katika baraka za kiroho za Waisraeli, wanawajibika kuwahudumia Waisraeli katika mahitaji yao ya kimwili. 28 Kwa hiyo baada ya kukamilisha kazi hii na kuhakikisha kuwa wamepokea kila kitu kilichokusanywa, nitakwenda Spania kupitia kwenu. 29 Ninafahamu kwamba nitakapokuja kwenu, nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.
30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, muwe pamoja nami mkiniombea kwa Mungu. 31 Ombeni niepushwe na wale wasioamini walioko Uyahudi, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa na watu wa Mungu; 32 ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, niburudishwe pamoja nanyi. 33 Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.
Copyright © 1989 by Biblica