Old/New Testament
Kuhusu Ndoa
7 Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. 2 Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
3 Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhal ika mke kwa mumewe. 4 Kwa maana mke hatawali mwili wake mwe nyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume hata wali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala. 5 Msiny imane, isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia. 6 Nasema haya kama ushauri, na si sheria. 7 Ningalipenda wote wawe kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa karama yake kutoka kwa Mungu, mmoja ana karama hii na mwingine ana karama ile.
8 Na sasa nasema kwa wale wasioolewa na kwa wajane. Ingekuwa vizuri kama wangeendelea kuishi bila kuoa au kuolewa kama mimi. 9 Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe. Ni afadhali kuoa kuliko kuwaka kwa tamaa.
10 Kwa wale waliooana ninayo amri, si amri yangu ila ni ya Bwana. Mke asimwache mumewe. 11 Lakini kama akimwacha, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Na mume asimpe mkewe talaka.
12 Lakini kwa wengine nasema, si Bwana ila ni mimi: kama ndugu ana mke asiyeamini, na huyo mke amekubali kuishi pamoja naye, basi asimpe talaka. 13 Na kama mwanamke mwamini ameolewa na mwanaume asiyeamini, na huyo mwanaume amekubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimpe talaka. 14 Kwa maana huyo mwanaume asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mkewe naye mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wao wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 15 Lakini kama yule asiyeamini akitaka kuachana na mwenzake anayeamini, basi na iwe hivyo. Katika hali hiyo mke au mume ambaye ni mwamini hafungwi. Kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16 Wewe mke, unajuaje kama hutamwokoa mumeo? Wewe mume unajuaje kama hutamwokoa mkeo?
Kuishi Kama Mlivyoitwa
17 Kila mtu aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, na ambayo ameitiwa na Mungu. Hii ndio amri ninayotoa kwa makanisa yote.
18 Kama mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa, basi asijaribu kuondoa alama za kutahiriwa kwake. Na kama mtu alikuwa hajatahi riwa alipoitwa, basi, asitafute kutahiriwa. 19 Kwa kuwa kutahi riwa au kutotahiriwa si kitu. Jambo lililo muhimu ni kutii amri za Mungu .
Copyright © 1989 by Biblica