Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Esth for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 5:1-6

Anania na Safira

Alikuwepo mtu aliyeitwa Anania na mke wake aliyeitwa Safira. Anania aliuza shamba lake, lakini aliwapa mitume sehemu tu ya pesa alizopata baada ya kuuza shamba lake. Kwa siri alibakiza kiasi cha pesa kwa ajili yake mwenyewe. Mke wake alilijua hili na akalikubali.

Petro akasema, “Anania, kwa nini umemruhusu Shetani aitawale akili yako kwa wazo la namna hii? Umebakiza sehemu ya pesa kwa ajili yako mwenyewe na kumdanganya Roho Mtakatifu! Je, kabla ya kuuza shamba, halikuwa lako? Na hata baada ya kuliuza, ungeweza kutumia pesa kwa namna yoyote unayotaka. Imekuwaje hata ufikirie kufanya jambo hili? Hukutudanganya sisi bali Mungu!”

5-6 Anania aliposikia hili, alianguka chini na kufa. Baadhi ya vijana wakaja na kuufunga mwili wake. Wakautoa nje na kuuzika. Kila mtu aliyelisikia hili aliingiwa hofu.

Baada ya kama saa tatu baadaye, mkewe naye alifika. Safira hakujua kilichompata mumewe. Petro akamwambia, “Niambie mlipata pesa kiasi gani baada ya kuuza shamba lenu. Kilikuwa kiasi hiki?”

Safira akajibu, “Ndiyo, hicho ndicho tulichopata baada ya kuuza shamba.”

Petro akamwambia, “Kwa nini wewe na mume wako mlikubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Sikiliza! Unasikia vishindo hivyo vya miguu? Watu waliomzika mume wako, wako mlangoni. Watakuchukua nje kwa njia hiyo hiyo.” 10 Safira akaanguka miguuni kwa Petro na kufa papo hapo. Vijana wakaingia, walipomwona amekwisha kufa, walimchukua na kumzika kando ya mume wake. 11 Kanisa lote na watu wote waliosikia kuhusu hili waliingiwa hofu.

Uthibitisho kutoka kwa Mungu

12 Mitume walipewa nguvu ya kufanya ishara nyingi za miujiza na maajabu katikati ya watu. Walikuwa wanakutanika pamoja mara kwa mara katika eneo la Hekalu lililoitwa Ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu yeyote ambaye hakuwa mwamini alikaa na kushirikiana nao, lakini kila mtu alisema mambo mazuri juu yao. 14 Watu wengi zaidi na zaidi walimwamini Bwana; na watu wengi, wanaume kwa wanawake waliongezwa katika kundi la waamini. 15 Hivyo watu waliwatoa wagonjwa majumbani na kuwaweka mitaani katika vitanda vidogo na mikeka. Walitumaini kuwa ikiwa Petro atapita karibu yao na kivuli chake kikawaangukia watapona. 16 Watu walikuja kutoka katika miji kuzunguka Yerusalemu. Waliwaleta wagonjwa au waliosumbuliwa na pepo wachafu. Wote waliponywa.

Mitume Wakamatwa

17 Kuhani mkuu na wafuasi wake wote wa karibu, kundi liitwalo Masadukayo wakaingiwa wivu sana. 18 Waliwakamata mitume na kuwafunga katika gereza la mji. 19 Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana alifungua milango ya gereza. Malaika akawaongoza mitume nje ya gereza na kusema, 20 “Nendeni mkasimame katika eneo la Hekalu. Waelezeni watu kila kitu kuhusu maisha haya mapya.” 21 Mitume waliposikia hili, walifanya kama walivyoambiwa. Walikwenda katika eneo la Hekalu asubuhi na mapema jua lilipokuwa linachomoza na kuanza kuwafundisha watu.

Kuhani mkuu na wafuasi wake wakakusanyika na kuitisha mkutano wa Baraza kuu na wazee wa Kiyahudi. Wakawatuma baadhi ya watu gerezani ili wawalete mitume kwao.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International