Print Page Options Listen to Luke 8-9
Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Luka 8-9

Baada ya haya Yesu alikwenda katika miji na vijiji akifu atana na wanafunzi wake. Kila alipokwenda alihubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu.

Baadhi ya wanawake aliokuwa amewatoa pepo wachafu na kuwa ponya walifuatana naye. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu ambaye aliitwa Magdalena, aliyetolewa pepo saba; Yohana mke wa Chuza -msimamizi wa ikulu ya Herode; Susana, na wengine wengi. Wana wake hawa walimhudumia Yesu na wanafunzi wake kutokana na mapato yao wenyewe.

Watu wengi walimiminika kutoka katika kila mji na umati mkubwa ulipokusanyika, Yesu akawaambia mfano huu: “Mkulima mmoja alikwenda shambani kwake kupanda mbegu. Alipokuwa akitawa nya mbegu, nyingine zilianguka njiani zikakanyagwa kanyagwa; na ndege wakazila. Na mbegu nyingine zilianguka penye miamba na zilipomea zikakauka kwa kukosa unyevu. Na mbegu nyingine zil ianguka kwenye miiba, ikazisonga zikafa. Mbegu nyingine zilian guka penye udongo mzuri, nazo zikamea na kutoa mazao mara mia zaidi ya mbegu alizopanda.” Baada ya kutoa mfano huu akasema: “Mwenye nia ya kusikia na asikie!”

Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano huu. 10 Naye akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waan galie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’ 11 Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. 12 Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa. 13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15 Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

Mfano Wa Taa

16 “Ni nani anayewasha taa kisha akaifunika, au akaiweka uvunguni, badala ya kuiweka mahali ambapo mwanga wake utaonekana? 17 Hakuna siri ambayo haitafichuliwa, wala hakuna jambo lililo fichika ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi. 18 Kwa hiyo muwe waangalifu mnaposikiliza, kwa sababu, yeye aliye na kitu ataonge zewa, naye ambaye hana, atanyang’anywa hata kile anachodhania anacho.”

Ndugu Wa Kweli

19 Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kum wona lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. 20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” 21 Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

Bwana Yesu Atuliza Dhoruba

22 Siku moja Yesu alipanda mashua na wanafunzi wake akawaam bia, “Twendeni ng’ambo ya pili ya ziwa.” Kwa hiyo wakaanza kuvuka. Walipokuwa wakivuka, akalala usingizi. Upepo mkali ukawa unavuma na mashua yao ikaanza kujaa maji; wakawa katika hatari ya kuzama.

24 Wale wanafunzi wakamkimbilia Yesu wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana, tunazama!” Ndipo akaamka akaukemea ule upepo na yale mawimbi vikakoma, pakawa shwari. 25 Kisha akawauliza, “Imani yenu iko wapi?” Wakashangaa na kuogopa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu ambaye anaamuru upepo na mawimbi navyo vikamtii?”

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo

26 Basi wakawasili ng’ambo ya pili katika jimbo la Wagerasi. 27 Na aliposhuka katika mashua alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyepagawa na pepo. Kwa muda mrefu mtu huyu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. 28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kuu, “Unataka nini kwangu, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu?

Nakuomba, tafadhali usinitese!”

29 Wakati huo Yesu alikuwa ameanza kumwamuru yule pepo mchafu amtoke. Mara nyingi pepo huyo alimwingia na hata alipo fungwa na minyororo na kuwekwa chini ya ulinzi aliivunjilia mbali minyororo hiyo na kukimbilia jangwani akiwa ametawaliwa kabisa na pepo huyo. 30 Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jeshi’ 31 Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda shimoni kwenye kifungo cha mashetani.

32 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo karibu wakilisha kando kando ya mlima. Wale pepo wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe. Akawaruhusu.

33 Kwa hiyo wakamtoka yule mtu wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe likatimka mbio katika ule mteremko mkali wakatumbukia ziwani na kuzama. 34 Watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe waliona yaliyotokea, wakakimbia wakaeneza habari hizi mjini na mashambani.

35 Watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotokea. Wali pofika hapo alipokuwa Yesu wakamwona yule mtu aliyetokwa na pepo amekaa karibu na Yesu, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa sana. 36 Wale walioona mambo yalivyotokea wakawasimu lia wenzao jinsi yule mtu alivyoponywa. 37 Watu wote wa jimbo hilo la Wagerasi wakamwomba Yesu aondoke kwao, kwa sababu wali kuwa wamejawa na woga. Basi akaingia katika mtumbwi akaondoka.

38 Yule mtu aliyetolewa pepo akamsihi Yesu afuatane naye. Lakini Yesu akakataa, akamwambia: 39 “Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu aliyokufanyia Mungu.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza mji mzima mambo makuu Yesu aliyomfanyia.

Yesu Amfufua Binti Wa Yairo

40 Yesu aliporudi ng’ambo ya pili umati mkubwa wa watu ukam pokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea.

41 Wakati huo akaja mtu mmoja jina lake Yairo, kiongozi wa sinagogi. Akapiga magoti mbele ya Yesu akamwomba afike nyumbani kwake, 42 kwa kuwa binti yake mwenye umri wa miaka kumi na mbili, aliyekuwa mtoto wake wa pekee, alikuwa mgonjwa mahututi, karibu ya kufa. Yesu alipokuwa akienda, umati ulimsonga sana.

43 Katika umati huo alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, wala hakuna mganga aliyeweza kumponya. 44 Akaja nyuma ya Yesu, akam gusa pindo la vazi lake. Mara damu iliyokuwa ikimtoka ikakauka, akapona. 45 Yesu akauliza: “Nani amenigusa?” Kila mtu alipo kana Petro akasema, “Bwana, watu ni wengi mno wanaokusonga kila upande.” 46 Yesu akasema: “Kuna mtu aliyenigusa maana naona ya kuwa nguvu za kuponya zimenitoka.” 47 Yule mama alipofahamu ya kuwa amegundulika akaja huku akitetemeka akapiga magoti mbele ya Yesu. Akamweleza Yesu mbele ya watu wote kilichomfanya amguse, na jinsi alivyoponywa mara. 48 Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” 49 Wakati Yesu alipo kuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo kum wambia, “Binti yako amefariki. Hakuna sababu ya kuendelea kum sumbua Mwalimu.” 50 Lakini Yesu aliposikia haya alimwambia Yairo, “Usiogope. Uwe na imani na binti yako atapona.” 51 Wal ipofika kwa Yairo akawazuia watu wote wasiingie ndani isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, na baba na mama wa yule binti. 52 Watu waliokuwepo walikuwa wakilia na kuomboleza lakini Yesu akawaam bia, “Acheni kulia! Huyu binti hajafa ila amelala!” 53 Wao wakamcheka kwa dharau maana walijua amekwisha kufa. 54 Yesu akamshika yule binti mkono akamwita: “Binti, amka!” 55 Uhai ukamrudia, naye akasimama mara moja. Yesu akaamuru apewe chakula. 56 Wazazi wake wakastaajabu sana lakini Yesu akawakataza wasim wambie mtu alivyomfufua binti yao.

Yesu Awatuma Wanafunzi Kumi Na wawili

Yesu akawaita pamoja wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka na uwezo wa kufukuza pepo wote na kuponya magonjwa yote. Kisha akawatuma waende wakautangaze Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha; na msichukue nguo za kubadili. Mkikaribishwa katika nyumba yo yote muwe wageni wa nyumba hiyo hadi mtakapoondoka katika kijiji hicho. Po pote ambapo hamtakaribishwa, mnapoondoka kung’uteni mavumbi miguuni mwenu kama ishara ya hukumu ya Mungu juu yao.”

Wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa. Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka!” Wengine wakasema, “Ni Eliya ametutokea” na wengine kwamba, “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?” Akajaribu sana amwone Yesu.

Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

10 Wanafunzi waliporudi walimweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua wakaenda peke yao mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. 11 Lakini watu wengi wakafahamu alipokwenda, wakamfuata. Akawa karibisha, akawafundisha tena kuhusu Ufalme wa mbinguni na akapo nya wangonjwa. 12 Ilipokaribia jioni, wale wanafunzi kumi na wawili wakamwambia Yesu, “Waruhusu watu hawa waondoke ili waweze kujitafutia chakula na mahali pa kulala katika vijiji na mashamba ya jirani kwa maana hapa tuko nyikani.” 13 Akawajibu, “Wapeni chakula.” Wakasema, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili. Unataka tukanunue chakula cha kuwatosha watu wote hawa?” 14 Kwa kuwa walikuwapo wanaume wapatao elfu tano! Lakini Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini-hamsini.” 15 Wakawaketisha wote. 16 Yesu akaichukua mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavi bariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. 17 Kila mtu akala na kutosheka na vilipokusanywa vipande vilivyobaki, vilijaa vikapu kumi na viwili.

Petro Amkiri Bwana Yesu Kuwa Ndiye Kristo

18 Siku moja Yesu alipokuwa akisali faraghani akiwa na wana funzi wake aliwauliza, “Watu husema mimi ni nani?” 19 Wakam wambia, “Watu husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni nabii wa kale aliyefufuka kutoka kwa wafu.”

20 Kisha akawauliza, “Ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiye Kristo wa Mungu.” 21 Yesu akawaka taza wasimwambie mtu jambo hilo 22 akisema, “Imenipasa mimi Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, maku hani wakuu na walimu wa sheria. Nitauawa na siku ya tatu nitafuf uliwa.” 23 Kisha akawaambia wote, “Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane nafsi yake, achukue msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa maana ye yote atakayeshughulikia zaidi usalama wa nafsi yake ataipoteza. Lakini ye yote atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataisalimisha. 25 Je, kuna faida gani kwa mtu kuupata ulimwengu mzima ambapo kwa kufanya hivyo ataipoteza nafsi yake? 26 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu, na mimi Mwana wa Adamu nitamwonea aibu mtu huyo nitakapo kuja katika utukufu wangu na wa Baba na wa malaika watakatifu. 27 Ninawaambia kweli, baadhi ya watu waliosimama hapa hawatakufa mpaka watakapouona Ufalme wa Mungu.”

Bwana Yesu Abadilika Sura

28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu alikwenda kusali mlimani pamoja na Petro, Yakobo na Yohana. 29 Alipokuwa akiomba, sura yake ili badilika, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta na kung’aa. 30 Ghafla wakawepo watu wawili wakaanza kuzungumza naye. Walikuwa ni Musa na Eliya! 31 Nao walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea Yerusalemu.

32 Petro na wenzake ambao walikuwa wamelala usingizi mzito waliamka wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Musa na Eliya walipoanza kuondoka, Petro akamwambia Yesu, “Bwana ni vizuri mno kwamba tuko hapa! Tutajenga vibanda vitatu - kimoja chako, kingine cha Musa na kin gine cha Eliya.” Lakini Petro hakujua anasema nini. 34 Petro alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu kubwa na kivuli chake kikawafunika, na wale wanafunzi wakashikwa na hofu lile wingu lilipowafikia. 35 Sauti ikatoka kwenye wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni yeye.” 36 Baada ya sauti hiyo kusema, alionekana Yesu peke yake. Wale wanafunzi wakakaa kimya na kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyoy aona.

37 Kesho yake aliposhuka kutoka mlimani alikutana na umati mkubwa wa watu. 38 Ghafla, mtu mmoja kati yao akapiga kelele akasema, “Mwalimu, tafadhali nakuomba umwangalie mtoto wangu, ni mwanangu wa pekee. 39 Mara kwa mara pepo humshika na kumfanya apige kelele kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu mdomoni. Anamtesa sana na hamwachii ila kwa shida. 40 Nimewaomba wanafunzi wako wamwondoe huyo pepo lakini wameshindwa.” 41 Yesu akajibu, “Enyi watu mliopotoka, msio na imani, nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”

42 Yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo akamwangusha, akam tia kifafa. Lakini Yesu akamwamuru yule pepo amtoke. Akamponya yule mtoto akamkabidhi kwa baba yake. 43 Watu wote walishangaa walipoona huo uweza mkuu wa Mungu. Wakati watu walipokuwa wanas taajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye aliwaambia wanafunzi wake: 44 “ Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa wanadamu.” 45 Lakini wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno hayo. Maana ya maneno hayo ilikuwa imefichwa ili wasiweze kuelewa, nao waliogopa kumwuliza.

Yesu Afundisha Kuhusu Ukubwa

46 Wanafunzi wakaanza kubishana wao kwa wao kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu zaidi. 47 Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao, akamsimamisha mtoto mdogo karibu naye 48 kisha akawaambia, “Ye yote atakayemkaribisha mtoto huyu mdogo kwa jina langu atakuwa amenikaribisha; na ye yote atakayenikaribisha mimi atakuwa amem karibisha yeye aliyenituma; kwa maana yeye aliye mdogo kati yenu, ndiye aliye mkubwa kuliko wote.” 49 Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako tukamzuia kwa maana yeye si mmoja wetu.” 50 Yesu akasema, “Msimzuie kwa sababu ye yote ambaye hapingani nanyi, yuko upande wenu.”

Yesu Akataliwa Samaria

51 Siku zake za kurudi mbinguni zilipokaribia, Yesu aliamua kwamba lazima aende Yerusalemu na akaanza safari kuelekea huko. 52 Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu. 53 Lakini watu wa kijiji hicho walikataa kumpokea kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba ali kuwa anakwenda Yerusalemu. 54 Basi wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuamuru moto kutoka mbinguni uwaangamize?” 55 Yesu akageuka, akawakemea. 56 Wakaenda kijiji kingine.

Gharama Ya Kumfuata Yesu

57 Walipokuwa wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufu ata po pote utakapokwenda.” 58 Yesu akamwambia, “Mbweha wanaishi kwenye mapango yao na ndege kwenye viota vyao lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulala na kupumzika.”

59 Yesu alimwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.” 60 Yesu akamwam bia, “Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautan gaze Ufalme wa Mungu.” 61 Mtu mwingine akamwambia, “Bwana nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.” 62 Yesu akamwambia, “Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.” Yesu Awatuma Wafuasi Sabini na Wawili

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica