Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Matayo 20-21

Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu

20 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu mwenye shamba la mizabibu aliyeondoka alfajiri kwenda kutafuta vibarua wa kufanya kazi shambani kwake. Wakapatana kuwa atawalipa msha hara wa kutwa, yaani dinari moja, akawapeleka shambani.

“Mnamo saa tatu akaondoka tena akawakuta watu wengine wamesimama sokoni bila kazi. Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu na nitawalipa haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda. Mnamo saa sita na pia saa tisa alion doka tena akafanya hivyo hivyo. Mnamo saa kumi na moja akaon doka tena akawakuta watu wengine bado wanazurura. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ Wakamjibu, ‘Ni kwa kuwa hakuna aliyetuajiri.’ Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la miza bibu.’

“Ilipofika jioni, yule mwenye shamba akamwita msimamizi wa vibarua akamwambia, ‘Waite wafanyakazi uwalipe ujira wao, ukian zia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akalipwa dinari moja. 10 Basi wale wal ioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipewa dinari moja. 11 Walipoipokea, wakaanza kumlalamikia yule mwenye shamba wakisema, 12 ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu. Ime kuwaje wewe ukawalipa sawa na sisi ambao tumefanya kazi ngumu na kuchomwa na jua mchana kutwa?’

13 “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sija kudhulumu. Je, hatukupatana kwamba utafanya kazi kwa dinari moja? 14 Chukua haki yako uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu ali yeajiriwa mwisho sawa na wewe. 15 Je, siwezi kufanya nipendavyo na mali yangu? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’ 16 Hali kadhalika, wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Yesu Azungumza Tena Kuhusu Kifo Chake

17 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili akawaambia, 18 “Sasa tunakwenda Yerusalemu na mimi Mwana wa Adamu nitatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na walimu wa sheria nao watanihukumu adhabu ya kifo 19 na kunikabidhi kwa watu wa mataifa ambao watanizomea na kunipiga mijeledi na kunisulubisha; na siku ya tatu nitafufuliwa.”

Ombi La Mama Wa Wana Wa Zebedayo

20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akaja kwa Yesu akiwa na wanae, akapiga magoti akamwomba aseme neno.

21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, ruhusu wanangu hawa, waketi mmoja upande wako wa kulia na mwin gine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”

22 Yesu akawaambia, “Hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kuny wea kikombe nitakachonywea mimi?” Wakajibu, “Tunaweza.’ ’

23 Akawaambia, “Kikombe changu mtakinywea. Lakini kuhusu kuketi kulia au kushoto kwangu, sina mamlaka ya kuwaruhusu. Nafasi hizo ni za wale ambao Baba yangu amewaandalia.”

24 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya waliwakasi rikia hao ndugu wawili. 25 Lakini Yesu akawaita wote pamoja aka waambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa mataifa hupenda kuheshi miwa, na wenye vyeo hupenda kuonyesha mamlaka yao. 26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, anayetaka kuwa mkuu kati yenu hana budi kuwa mtumishi wenu. 27 Na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumishi wenu; 28 kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi.”

Yesu Awaponya Vipofu Wawili

29 Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu, walimfuata. 30 Vipofu wawili waliokuwa wameketi kando ya barabara waliposikia kwamba ni Yesu aliyekuwa akipita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 31 Watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao walizidi kupiga kelele wakisema, “ Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 32 Yesu akasimama na akawaita, akawau liza, “Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu, “Bwana tuna taka kuona.”

34 Yesu akawaonea huruma, akawagusa, na mara wakaweza kuona; wakamfuata.

Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

21 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, aka waagiza, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu na mkiingia mtamwona punda amefungwa na mwanapunda pamoja naye. Wafungueni mniletee. Kama mtu akiwauliza lo lote, mwambieni, ‘Bwana anawa hitaji Haya yalitokea ili kutimiza utabiri wa nabii aliposema, ‘Mwambieni binti Sayuni, tazama mfalme wako anakuja kwako ni mnyenyekevu, na amepanda punda, mwanapunda, mtoto wa punda.’

Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Wakamleta yule punda na mwanapunda. Wakatandika mavazi yao juu ya hao punda na Yesu akaketi juu yake. Umati mkubwa wa watu wakatandika nguo zao barabarani, wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani. Ule umati wa watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapiga kelele wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi . Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Hosana juu mbin guni.”

10 Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukajawa na hekaheka, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 11 Ule umati wa watu wakajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

Yesu Afukuza Wafanya Biashara Hekaluni

12 Yesu aliingia katika eneo la Hekalu akawafukuza wote wali okuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za watu waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”

14 Vipofu na vilema wakamwendea, naye akawaponya. 15 Lakini makuhani wakuu na walimu wa sheria waliudhika walipoona mambo ya ajabu aliyoyafanya na kuwasikia watoto wakishangilia Hekaluni wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi!” Wakamwuliza Yesu, 16 “Unasikia hawa wanavyosema?” Akawajibu, “Nasikia. Kwani hamjasoma maneno haya, ‘Kutoka katika vinywa vya watoto wadogo na wale wanaonyonya umeleta sifa kamili’? ” 17 Akawaacha akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

18 Asubuhi, Yesu alipokuwa akirudi mjini, aliona njaa. 19 Alipoona mtini kando ya bara bara aliusogelea akakuta hauna tunda lo lote ila majani tu. Akaulaani akisema, “Usizae matunda kamwe!” Wakati huo huo ule mtini ukanyauka. 20 Wanafunzi wake wakashangazwa na tukio hilo wakamwuliza, “Imekuwaje mtini huu ukanyauka ghafla?” 21 Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli, kama mna imani na msiwe na mashaka hata kidogo, mtaweza kufanya yaliy ofanyika kwa huu mtini; na hata mkiuambia mlima huu, ‘Ng’oka, nenda kajitupe baharini,’ itafanyika. 22 Na lo lote mtakaloomba katika sala, mtapewa, kama mna imani.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

23 Yesu alipoingia tena Hekaluni, makuhani wakuu na wazee walimjia alipokuwa akifundisha, wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani na ni nani amekupa mamlaka hayo?” 24 Yesu akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali na mkinijibu nami nita waambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Mbinguni au kwa watu?” Wakaanza kubishana kati yao wakisema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema ulitoka kwa wanadamu, tunaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.” 27 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatufahamu.” Naye aka waambia, “Nami sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wana Wawili

28 ‘Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili wa kiume. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ 29 Yule mwanae akasema, ‘Siendi,’ lakini baadaye akabadili mawazo akaenda. 30 Kisha yule baba akamwendea yule mwanae mwingine akamwambia vile vile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda baba,’ lakini asiende. 31 Ni yupi kati yao aliyetimiza alivyotaka baba yake?” Wakamjibu, “Yule wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu.

32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kum wamini.”

Mfano Wa Wapangaji Waovu

33 “Sikilizeni mfano mwingine: mtu mmoja mwenye shamba alilima shamba akapanda mizabibu. Akalizungushia ua, na ndani yake akachimba kisima cha kusindikia zabibu; na akajenga mnara. Kisha akalikodisha hilo shamba kwa wakulima fulani, akasafiri kwenda nchi nyingine.

34 “Wakati wa mavuno ulipokaribia aliwatuma watumishi wake kwa hao wakulima kupokea mavuno yake. 35 Wale wakulima wakawaka mata wale watumishi; wakampiga mmoja, wakamwua mwingine na kum piga mawe mwingine. 36 Akatuma watumishi wengine, wengi kuliko wale wa mwanzo. Wale wakulima wakawatendea vile vile. 37 Mwish owe akamtuma mwanae kwao akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwa nangu.’ 38 Lakini walipomwona mwanae, waliambiana, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumwue tuchukue urithi wake.’ 39 Basi wakamchu kua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. 40 Sasa, akija yule mwenye shamba, mnadhani atawafanya nini hao waku lima?” 41 Wakamjibu, “Atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake kwa wakulima wengine ambao watampatia matunda yake wakati wa mavuno.”

42 Yesu akawaambia, “Hamjapata kusoma katika Maandiko kwamba: ‘Lile jiwe walilokataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la pembeni; Bwana ndiye amefanya jambo hili nalo ni zuri ajabu machoni petu’?

43 Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na watapewa watu wawezao kutoa matunda yake.” [ 44 “Na ambaye ataanguka kwenye jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagika sagika.”]

45 Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia mifano yake, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 46 Wakatafuta njia ya kumkamata lakini waliogopa ule umati wa watu kwa kuwa wao walim tambua Yesu kuwa nabii.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica