Book of Common Prayer
Maonyo ya Mwisho na Salamu
13 Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuwatembelea. Na mkumbuke, “Kila shitaka ni lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu wanaosema kuwa jambo hilo ni la kweli.”(A) 2 Nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili, nilitoa maonyo kwa wale waliotenda dhambi. Sipo hapo sasa, ila natoa onyo lingine kwao na kwa yeyote aliyetenda dhambi: Nitakapo kuja tena kwenu, nitawaadhibu walio miongoni mwenu ambao bado wanatenda dhambi. 3 Mnatafuta uthibitisho kuwa Kristo anasema kupitia mimi. Uthibitisho wangu ni kuwa yeye si dhaifu kuwashughulikia bali yeye anaonesha uweza wake miongoni mwenu. 4 Ni kweli kuwa Kristo alikuwa dhaifu alipouawa msalabani, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Ni kweli pia kwamba twashiriki unyonge wake, lakini kwa kushughulika nanyi, tutakuwa hai pamoja nae katika uweza wa Mungu.
5 Jiangalieni ninyi wenyewe. Mjipime ninyi wenyewe mkaone kama mngali mnaishi katika imani. Hamtambui kuwa Kristo Yesu yu ndani yenu? La mkishindwa jaribio hilo; ikiwa hamtakuwa mkiishi katika imani; basi Kristo hayumo ndani yenu. 6 Lakini ni matumaini yangu kuwa mtagundua ya kwamba hatujashindwa jaribio hilo. 7 Tunawaombea kwa Mungu msifanye lolote lililo baya. Tunachojali hapa si kwamba watu waone kuwa tumeshinda jaribio katika ile kazi tuliyofanya pamoja nanyi. Tunachokitaka zaidi ni ninyi kufanya lililo jema, hata ikiwa itaonekana kuwa tumeshindwa jaribio. 8 Hatuwezi kufanya lolote lililo kinyume na kweli bali lile linalodumisha kweli. 9 Tunafuraha kuonekana tu wadhaifu ikiwa ninyi mko imara. Na hili ndilo tunaloomba, kwamba maisha yenu yatakamilishwa katika haki tena. 10 Ninaandika haya kabla sijaja kwa kuwa niko mbali nanyi ili nijapo nisilazimike kutumia mamlaka kuwaadhibu. Bwana alinipa mamlaka hayo kuwaimarisha, na sio kuwaharibu.
11 Sasa, wapendwa dada zangu na kaka zangu mjazwe furaha. Jitahidini kutengeneza njia zenu, fanyeni nilichowaomba kufanya. Mpatane kila mmoja na mwenziwe, na ishini katika amani. Ndipo Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
25 Alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa akitoka damu (kama ilivyo desturi ya wanawake kila mwezi) kila siku kwa miaka kumi na miwili. 26 Huyu alikuwa ameteseka sana akiwa chini ya uangalizi wa madaktari wengi. Yeye alikuwa ametumia vyote alivyokuwa navyo. Hata hivyo hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi.
27 Wakati aliposikia juu ya Yesu, alimwendea kwa nyuma akiwa katika kundi lile na kuligusa joho lake. 28 Kwani alikuwa akijisemea mwenyewe, “Ikiwa nitagusa tu vazi lake, nitapona.” 29 Mara moja chanzo cha kutoka kwake damu kikakauka, na akajisikia mwilini mwake kwamba amepona matatizo yake. 30 Naye Yesu akatambua mara moja kwamba nguvu zilimtoka. Aligeuka nyuma na kuuliza “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
31 Wanafunzi wake wakamwambia, “Uliliona kundi likisukumana kukuzunguka, nawe unauliza, Nani aliyenigusa?”
32 Lakini Yesu aliendelea kuangalia kumzunguka kuona ni nani aliyeyafanya haya. 33 Yule Mwanamke akiwa anatetemeka kwa hofu akijua nini kilichotokea kwake, alikuja na kuanguka mbele yake, akamweleza ukweli wote. 34 Kisha Yesu akamwambia, “Binti yangu imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, na uendelee kupona matatizo yako.”
© 2017 Bible League International