Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Judg for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 5:12-26

Uthibitisho kutoka kwa Mungu

12 Mitume walipewa nguvu ya kufanya ishara nyingi za miujiza na maajabu katikati ya watu. Walikuwa wanakutanika pamoja mara kwa mara katika eneo la Hekalu lililoitwa Ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu yeyote ambaye hakuwa mwamini alikaa na kushirikiana nao, lakini kila mtu alisema mambo mazuri juu yao. 14 Watu wengi zaidi na zaidi walimwamini Bwana; na watu wengi, wanaume kwa wanawake waliongezwa katika kundi la waamini. 15 Hivyo watu waliwatoa wagonjwa majumbani na kuwaweka mitaani katika vitanda vidogo na mikeka. Walitumaini kuwa ikiwa Petro atapita karibu yao na kivuli chake kikawaangukia watapona. 16 Watu walikuja kutoka katika miji kuzunguka Yerusalemu. Waliwaleta wagonjwa au waliosumbuliwa na pepo wachafu. Wote waliponywa.

Mitume Wakamatwa

17 Kuhani mkuu na wafuasi wake wote wa karibu, kundi liitwalo Masadukayo wakaingiwa wivu sana. 18 Waliwakamata mitume na kuwafunga katika gereza la mji. 19 Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana alifungua milango ya gereza. Malaika akawaongoza mitume nje ya gereza na kusema, 20 “Nendeni mkasimame katika eneo la Hekalu. Waelezeni watu kila kitu kuhusu maisha haya mapya.” 21 Mitume waliposikia hili, walifanya kama walivyoambiwa. Walikwenda katika eneo la Hekalu asubuhi na mapema jua lilipokuwa linachomoza na kuanza kuwafundisha watu.

Kuhani mkuu na wafuasi wake wakakusanyika na kuitisha mkutano wa Baraza kuu na wazee wa Kiyahudi. Wakawatuma baadhi ya watu gerezani ili wawalete mitume kwao. 22 Watu wale walipokwenda gerezani, hawakuwaona mitume. Hivyo walirudi na kuwaambia viongozi wa Kiyahudi kuhusu hili. 23 Walisema, “Gereza lilikuwa limefungwa na milango ilikuwa imefungwa. Walinzi walikuwa wamesimama milangoni. Lakini tulipofungua milango, gereza lilikuwa tupu!” 24 Mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani walipolisikia hili, walichanganyikiwa na kujiuliza maana yake ni nini.

25 Ndipo mtu mwingine akaja na kuwaambia, “Sikilizeni! Watu mliowafunga gerezani wamesimama katika eneo la Hekalu wanawafundisha watu!” 26 Mkuu wa walinzi na askari walinzi wa Hekalu walikwenda na kuwarudisha mitume. Lakini askari hawakutumia nguvu, kwa sababu waliwaogopa watu. Waliogopa watu wangewapiga kwa mawe mpaka wafe.

Yohana 3:1-21

Yesu na Nikodemu

Alikuwepo mtu aliyeitwa Nikodemu, mmoja wa Mafarisayo. Yeye alikuwa kiongozi muhimu sana wa Kiyahudi. Usiku mmoja alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa kutoka kwa Mungu. Hayupo mtu yeyote anayeweza kutenda ishara na miujiza unayotenda bila msaada wa Mungu.”

Yesu akajibu, “Hakika nakuambia, ni lazima kila mtu azaliwe upya.[a] Yeyote ambaye hajazaliwa mara ya pili hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.”

Nikodemu akasema, “Yawezekanaje mtu ambaye tayari ni mzee akazaliwa tena? Je, anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa kwa mara ya pili?”

Yesu akamjibu, “Uniamini ninapokwambia kuwa kila mtu anapaswa kuzaliwa tena kwa maji na kwa Roho. Yeyote ambaye hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Maisha pekee ambayo watu huyapata kutoka kwa wazazi wao ni ya kimwili. Lakini maisha mapya anayopewa mtu na Roho ni ya kiroho. Usishangae kwa kuwa nilikuambia, ‘Ni lazima mzaliwe upya.’ Upepo huvuma kuelekea popote unakopenda. Unausikia, lakini huwezi kujua unakotoka na unakoelekea. Hivyo ndivyo ilivyo kwa kila aliyezaliwa kwa Roho.”

Nikodemu akauliza, “Je, haya yote yanawezekana namna gani?”

10 Yesu akasema, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Israeli, inakuwaje huelewi mambo haya? 11 Ukweli ni kwamba, tunaongea yale tunayoyafahamu. Tunayasema yale tuliyoyaona. Hata hivyo ninyi hamyakubali yale tunayowaambia. 12 Nimewaeleza juu ya mambo ya hapa duniani, lakini hamniamini. Vivyo hivyo nina uhakika hamtaniamini hata nikiwaeleza mambo ya mbinguni! 13 Sikiliza, hakuna mtu aliyewahi kwenda kwa Mungu mbinguni isipokuwa Mwana wa Adamu. Yeye pekee ndiye aliyekuja duniani kutoka mbinguni.”

14 Unakumbuka yule nyoka wa shaba ambaye Musa alimwinua kule jangwani?[b] Vivyo hivyo Mwana wa Adamu anapaswa kuinuliwa juu. 15 Kisha kila anayemwamini aweze kuupata uzima wa milele.[c]

16 Kweli, hivi ndivyo Mungu alivyouonyesha upendo wake mkuu kwa ulimwengu: akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu anayemwamini asiharibiwe na mauti bali aupate uzima wa milele. 17 Mungu alimtuma Mwanawe ili kuuokoa ulimwengu. Hakumtuma kuja kuuhukumu na kuuweka hatiani, bali kuuokoa kwa njia ya mwanawe. 18 Wote wanaomwamini Mwana wa Mungu hawahukumiwi hatia yoyote. Lakini wale wasiomwamini wamekwisha kuhukumiwa tayari, kwa sababu hawakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19 Wamehukumiwa kutokana na ukweli huu: Kwamba nuru[d] imekuja ulimwenguni, lakini watu hawakuitaka nuru. Bali walilitaka giza, kwa sababu walikuwa wanatenda mambo maovu. 20 Kila anayetenda maovu huichukia nuru. Hawezi kuja kwenye nuru, kwa sababu nuru itayaweka wazi matendo maovu yote aliyotenda.

21 Lakini yeyote anayeifuata njia ya kweli huja kwenye nuru. Nayo nuru itaonesha kuwa Mungu amekuwepo katika matendo yake yote.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International