Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Eccl for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Wagalatia 3:15-22

Sheria na Ahadi

15 Ndugu zangu, hebu niwape mfano kutoka maisha ya kila siku: Fikiri kuhusu makubaliano ambayo mtu hukubaliana na mwingine. Baada ya makubaliano hayo kufanywa rasmi, hakuna anayeweza kuongeza chochote kwenye makubaliano hayo na hakuna anayeweza kulipuuza. 16 Mungu aliweka agano kwa Ibrahimu na uzao wake. Maandiko hayasemi, “na kwa ajili ya uzao wenu”. Hilo lingekuwa na maana ya watu wengi. Lakini linasema, “na kwa uzao wako”. Hiyo ina maana ya uzao mmoja tu, na uzao huo ni Kristo. 17 Hii ndiyo maana yangu: Agano ambalo Mungu aliliweka na Ibrahimu lilifanywa rasmi na Mungu muda mrefu kabla ya kuja kwa sheria. Sheria ilikuja miaka 430 baadaye. Hivyo sheria haingeweza kulifuta agano hilo na kuibadili ahadi ya Mungu.

18 Baraka alizonazo Mungu kwa ajili ya watu wake hazipatikani kwa njia ya sheria. Ikiwa ingekuwa hivyo, basi isingekuwa ahadi ya Mungu inayotuletea sisi baraka hiyo. Lakini Mungu aliitoa bure baraka yake kwa Ibrahamu kama agano.

19 Hivyo kwa nini sheria ilitolewa? Sheria ililetwa baadaye kwa sababu ya makosa wanayotenda[a] watu. Lakini sheria ingeendelea kutumika hadi kuja kwa Uzao wa Ibrahimu. Huyu ni Uzao unaotajwa katika agano lililotolewa na Mungu. Lakini sheria ilitolewa kupitia malaika na malaika walimtumia Musa kama mpatanishi wa kuwapa watu sheria. 20 Hivyo mpatanishi anahitajika pale ambapo upande mmoja unapaswa kufikia mapatano. Lakini Mungu ambaye ni mmoja, hakumtumia mpatanishi alipompa ahadi Ibrahimu.[b]

Lengo la Sheria ya Musa

21 Je, hili lamaanisha kwamba sheria hutenda kazi kinyume na ahadi za Mungu? La hasha. Sheria iliyotolewa kamwe haikuwa na uwezo wa kuwaletea watu maisha mapya. Ingekuwa hivyo, basi tungehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kuifuata sheria. 22 Lakini hilo halikuwa kusudi la sheria. Maandiko yanauweka ulimwengu wote chini ya udhibiti wa dhambi kama aina ya kifungo gerezani. Ili kile ambacho Mungu aliahidi kipokelewe kwa njia ya imani katika[c] Yesu Kristo. Hii hutolewa kwa wale wanaomwamini.

Mathayo 14:22-36

Yesu Atembea Juu ya Maji

(Mk 6:45-52; Yh 6:16-21)

22 Mara baada ya hili Yesu akawaambia wafuasi wake wapande kwenye mtumbwi. Akawaambia waende upande mwingine wa ziwa. Aliwaambia angekuja baadaye, alikaa pale ili kuwaaga watu. 23 Baada ya Yesu kuwaaga watu, alikwenda kwenye vilima peke yake kuomba. Ikawa jioni na alikuwa pale peke yake. 24 Wakati huu mtumbwi ilikuwa mbali kutoka pwani. Kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kinyume na mtumbwi, mtumbwi ulikuwa unapata msukosuko kwa sababu ya mawimbi.

25 Kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi, wafuasi wa Yesu walikuwa bado ndani ya mtumbwi. Yesu akaenda kwao akitembea juu ya maji. 26 Iliwatisha walipomwona anatembea juu ya maji. Wakapiga kelele kwa woga “Ni mzuka!”

27 Lakini haraka Yesu akawaambia, “Msihofu! Ni mimi! Msiogope.”

28 Petro akasema, “Bwana, ikiwa hakika ni wewe, niambie nije kwako juu ya maji.”

29 Yesu akasema, “Njoo, Petro.”

Kisha Petro akauacha mtumbwi na kutembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini Petro alipokuwa anatembea juu ya maji, aliyaona mawimbi na upepo. Aliogopa na kuanza kuzama katika maji. Akapiga kelele, “Bwana, niokoe!”

31 Haraka Yesu akamshika Petro kwa mkono wake. Akasema, “Imani yako ni ndogo. Kwa nini ulisita?”

32 Baada ya Petro na Yesu kuingia kwenye mtumbwi, upepo ukakoma. 33 Kisha wafuasi wakamwabudu Yesu na kusema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

Yesu Awaponya Watu Wengi Wagonjwa

(Mk 6:53-56)

34 Baada ya kuvuka ziwa, wakafika pwani katika eneo la Genesareti. 35 Baadhi ya watu pale wakamwona Yesu na wakamtambua kuwa ni nani. Hivyo wakatuma ujumbe kwa watu wengine katika eneo lote kuwa Yesu amekuja. Watu wakawaleta wagonjwa wao wote kwake. 36 Walimsihi Yesu awaruhusu waguse tu upindo wa vazi lake ili waponywe. Na wagonjwa wote waliogusa vazi lake waliponywa.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International