Add parallel Print Page Options

Yesu Atembea Juu ya Maji

(Mt 14:22-33; Yh 6:16-21)

45 Mara Yesu akawafanya wafuasi wake wapande kwenye mashua na wamtangulie kwenda Bethsaida upande wa pili wa ziwa, wakati yeye akiliacha lile kundi liondoke. 46 Baada ya Yesu kuwaaga wale watu, alienda kwenye vilima kuomba.

47 Ilipotimia jioni, mashua ilikuwa katikati ya ziwa, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 48 Naye akawaona wanafunzi wake wakihangaika kupiga makasia, kwani upepo uliwapinga. Kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi Yesu aliwaendea akitembea juu ya ziwa. Yeye akiwa karibu kuwapita, 49 wanafunzi wake wakamwona akitembea juu ya ziwa,[a] na wakafikiri kuwa alikuwa ni mzimu, ndipo walipopiga kelele. 50 Kwa kuwa wote walimwona, na wakaogopa. Mara tu alizungumza nao na kuwaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Usiogope.” 51 Kisha alipanda kwenye mtumbwi pamoja nao, na upepo ukatulia. Wakashangaa kabisa, 52 kwa kuwa walikuwa bado hawajauelewa ule muujiza wa mikate. Kwani fahamu zao zilikuwa zimezibwa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 6:49 akitembea juu ya ziwa Watu zama za Marko waliamini kwamba mizimu isingeweza kutembea juu ya maji, lakini waliamini miungu wangeweza kutembea juu ya maji. Watu hao wangeshangaa kuona mitume wa Yesu wakiwa tayari kuamini kitu potovu kabla ya kuamini kuwa Yesu alisimama mbele yao ni Mungu kwani ametembea majini.