Book of Common Prayer
Paulo Atembelea Troa Mara ya Mwisho
7 Siku ya Jumapili[a] sote tulikusanyika pamoja kula Meza ya Bwana.[b] Paulo alizungumza na kundi. Kwa sababu alipanga kuondoka siku iliyofuata, aliendelea kuzungumza mpaka usiku wa manane. 8 Tulikuwa wote kwenye chumba ghorofani na kulikuwa taa nyingi chumbani. 9 Alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa amekaa dirishani aliyeitwa Eutiko. Paulo aliendelea kuzungumza, na Eutiko alianza kuchoka na kusikia ungungizi. Mwishowe alisinzia na kuanguka. Alianguka chini, nje kutoka ghorofa ya tatu. Watu walipokwenda kumnyenyua alikuwa amekwisha kufa.
10 Paulo alishuka, akaenda mahali alipokuwa Eutiko, akapiga magoti, na akamkumbatia. Akawaambia waamini wengine, “Msiwe na hofu. Ni mzima yuko hai sasa.” 11 Kisha Paulo akapanda ghorofani, akamega baadhi ya mikate na kula. Alizungumza nao kwa muda mrefu. Alimaliza kuzungumza mapema asubuhi na akaondoka. 12 Wafuasi wa Bwana walimpeleka Eutiko nyumbani akiwa hai, walifarijika sana wote.
Utangulizeni Kwanza Ufalme wa Mungu
(Mt 6:25-34,19-21)
22 Yesu akawaambia wafuasi wake, “Hivyo ninawaambia, msisumbuke juu ya vitu mnavyohitaji kwa ajili ya kuishi, mtakula nini au mtavaa nini. 23 Maisha ni muhimu zaidi ya chakula mnachokula na mwili ni zaidi ya mavazi mnayovaa. 24 Waangalieni kunguru, hawapandi, hawavuni au kuweka katika majumba au ghala, lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani sana kuliko ndege. 25 Hakuna mmoja wenu anayeweza kujiongezea muda katika maisha yake kwa kujihangaisha na maisha. 26 Na ikiwa hamwezi kufanya mambo madogo, kwa nini mnajihangaisha kwa mambo makubwa?
27 Yatafakarini maua yanavyoota. Hayafanyi kazi wala kujitengenezea mavazi. Lakini ninawaambia hata Sulemani, mfalme mkuu na tajiri, hakuvikwa vizuri kama maua haya. 28 Ikiwa Mungu huyavika vizuri namna hii majani ya porini, mnadhani atawafanyia nini ninyi? Hilo ni jani tu, siku moja li hai na siku inayofuata linachomwa moto. Lakini Mungu huyajali kiasi cha kuyapendezesha. Hakika atafanya zaidi kwa ajili yenu. Imani yenu ni ndogo!
29 Hivyo daima msijihangaishe na kile mtakachokula ama mtakachokunywa. Msisumbukie mambo haya. 30 Hayo ndiyo mambo ambayo watu wote wasiomjua Mungu huyafikiria daima. Lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnayahitaji mambo haya. 31 Mnapaswa kufikiri kuhusu ufalme wa Mungu. Naye Mungu atawapa mambo mengine yote mnayohitaji.
© 2017 Bible League International