Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Read the New Testament in 24 Weeks

A reading plan that walks through the entire New Testament in 24 weeks of daily readings.
Duration: 168 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
2 Wakorintho 3-4

Watumishi wa Agano Jipya la Mungu

Je, mnadhani tunaanza kujitafutia sifa? Je, tunahitaji barua za utambulisho kuja kwenu au kutoka kwenu kama wengine? Hapana, ninyi wenyewe ni barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu. Inafahamika na kusomwa na watu wote. Mnaonyesha kuwa ninyi ni barua toka kwa Kristo aliyoituma kupitia sisi. Barua ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa katika mbao za mawe[a] lakini katika mioyo ya wanadamu.

Tunaweza kusema hili, kwa sababu Kristo ndiye anayetupa uhakika huu mbele za Mungu. Simaanishi kuwa tuna uwezo wa kufanya jambo lolote jema kwa uwezo wetu wenyewe. Mungu ndiye anatuwezesha kufanya yote tunayoyafanya. Ametuwezesha pia kuwa watumishi wa agano jipya lililotoka kwake kwenda kwa watu wake. Si agano la sheria zilizoandikwa, ni la Roho. Sheria zilizoandikwa huleta mauti, bali Roho huleta uzima.

Namna Nzuri ya Kumtumikia Mungu

Agano la kale lililoleta mauti, lililoandikwa kwenye mawe, lilikuja na utukufu wa Mungu. Kwa kweli, uso wa Musa ulikuwa unang'aa utukufu (Utukufu uliokuwa na ukomo) hata watu wa Israel hawakuweza kuendelea kumtazama usoni. Hivyo kwa hakika zaidi huduma ya agano jipya linalokuja kutoka kwa Roho anayeleta uzima lina utukufu zaidi. Maana yangu ni kuwa: utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu uliwaweka watu katika hatia ya dhambi na kuwapa hukumu, lakini lilikuwa na utukufu. Hivyo kwa hakika utaratibu mpya wa kumtumikia Mungu unaowaweka huru watu kutoka hukumu una utukufu mkubwa zaidi. 10 Utaratibu wa zamani wa utumishi kwa Mungu ulikuwa na utukufu. Lakini kwa hakika unapoteza utukufu wake unapolinganishwa na utukufu mkubwa zaidi wa utaratibu mpya wa utumishi kwa Mungu. 11 Ikiwa utumishi ule wa muda ulikuja na utukufu, basi utumishi wa kudumu umekuja na utukufu mkubwa zaidi.

12 Kwa sababu tuna tumaini hili tunatenda kwa ujasiri mkubwa. 13 Hatuko kama Musa, ambaye alifunika uso wake ili watu wa Israel wasiendelee kuona kuwa utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu ulikuwa unaelekea mwisho. 14 Lakini mioyo yao ilikuwa imefungwa. Na hata leo, watu wale wanapolisoma agano la kale, fahamu zao zinakuwa zimefunikwa. Ni kwa kupitia Yesu Kristo tu agano la kale linaondolewa. 15 Ndiyo, hata leo, wanaposoma sheria ya Musa, fahamu zao zimefunikwa. 16 Lakini, kama maandiko yanavyosema juu ya Musa, “Kila anapomgeukia Bwana, ufahamu wake unafunuliwa.” 17 Katika maandiko hayo Bwana ni Roho, na palipo na Roho wa Bwana, pana uhuru. 18 Na sura zetu hazikufunikwa. Sote tunaendelea kuutazama utukufu wa Bwana, na tunabadilishwa na kufanana na mfano huo huo tunaouona. Badiliko hili linatuletea utukufu zaidi na zaidi, na linatoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.

Hazina ya kiroho katika Vyungu vya Udongo

Mungu, kwa rehema zake, alitupa sisi huduma hii ili tuifanye, hivyo hatukati tamaa. Lakini tumekataa mambo ya aibu ya siri. Hatumdanganyi mtu yeyote, na hatuyabadilii mafundisho ya Mungu. Tunaifundisha kweli wazi wazi. Na hivi ndivyo watu wanaweza kutambua mioyoni mwao sisi ni watu wa namna gani mbele za Mungu. Habari Njema tunazowahubiri watu hazijafichika kwa yeyote isipokuwa kwa waliopotea. Mtawala[b] wa dunia hii amezitia giza akili za wasioamini. Hawawezi kuona nuru ya Habari Njema; ujumbe juu ya uungu wa Kristo, taswira halisi ya Mungu. Hatuwaambii watu habari zetu wenyewe. Lakini tunawaambia habari za Kristo Yesu kuwa ni Bwana, na tunawaambia kuwa sisi ni watumwa wenu kwa ajili ya Yesu. Kuna wakati Mungu alisema, “Na nuru ing'ae gizani”[c] na huyu ni Mungu yule yule anayesababisha nuru ing'ae katika mioyo yetu ili tutambue utukufu wa uungu wake mkuu unaongaa katika sura ya Kristo.

Tuna hazina hii kutoka kwa Mungu, lakini sisi ni kama vyombo vya udongo tu vinavyobeba hazina. Hii ni kuonesha kuwa nguvu ya kustaajabisha tuliyo nayo inatoka kwa Mungu, si kwetu. Tunasumbuliwa kila upande, lakini hatushindwi. Mara kwa mara hatujui tufanye nini, lakini hatukati tamaa. Tunateswa, lakini Mungu hatuachi. Tunaangushwa chini wa nyakati zingine, laki hatuangamizwi. 10 Hivyo tunashiriki kifo cha Yesu katika miili yetu kila wakati, lakini haya yanatokea ili uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu. 11 Tuko hai, lakini kwa ajili ya Yesu tupo katika hatari ya kifo kila wakati, ili kwamba uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ya kufa. 12 Kwa hiyo kifo kinafanya kazi ndani yetu, lakini matokeo yake ni kwamba uzima unafanya kazi ndani yenu.

13 Maandiko yanasema, “Niliamini, hivyo nikasema.”(A) Tuna Roho huyo huyo anayetupa imani kama hiyo. Tunaamini, na hivyo tunasema pia. 14 Mungu alimfufua Bwana Yesu kutoka kwa wafu, nasi tunajua kuwa atatufufua pamoja na Yesu. Mungu atatukusanya pamoja nanyi, na tutasimama mbele zake. 15 Mambo yote haya ni kwa ajili yenu. Na hivyo neema ya Mungu inatolewa kwa watu wengi zaidi na zaidi. Hili litaleta shukrani nyingi zaidi na utukufu kwa Mungu.

Kuishi kwa Imani

16 Hii ndiyo sababu hatukati tamaa. Miili yetu inazidi kuzeeka na kuchoka, lakini roho zetu ndani zinafanywa upya kila siku. 17 Tuna masumbufu, lakini ni madogo na ni ya muda mfupi. Na masumbufu haya yanatusaidia kuupata utukufu wa milele ulio mkuu kuliko masumbufu yetu. 18 Hivyo twafikiri juu ya mambo tusiyoweza kuyaona, si tunayoona. Tunayoyaona ni ya kitambo tu, na yale tusiyoyaona yanadumu milele.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International