Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: 1Chr for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waebrania 13

Ibada Inayompendeza Mungu

13 Endeleeni kupendana ninyi kwa ninyi kama kaka na dada katika Kristo. Mkikumbuka kuwasaidia watu kwa kuwakaribisha majumbani mwenu. Watu wengine wamefanya hivyo na wakawa wamewasaidia malaika pasipo wao kujua. Msiwasahau wale walioko magerezani. Wakumbukeni kama vile mko magerezani pamoja nao. Na msiwasahau wale wanaoteseka. Wakumbukeni kama vile mnateseka pamoja nao.

Ndoa iheshimiwe na kila mmoja. Na kila ndoa itunzwe kwa usafi kati ya mume na mke. Mungu atawahukumu kuwa na hatia wale wanaofanya uzinzi na uasherati. Yatunzeni maisha yenu yawe huru kutokana na kupenda fedha. Na mridhike na kile mlichonacho. Mungu amesema: “Sitakuacha kamwe; Sitakukimbia kamwe.”(A) Hivyo tunaweza kuwa na uhakika na kusema:

“Bwana ndiye msaidizi wangu;
    Sitaogopa.
Watu hawawezi kunifanya chochote.”(B)

Wakumbukeni viongozi wenu. Waliwafundisha ujumbe wa Mungu. Kumbukeni jinsi walivyoishi na walivyokufa, na muiige imani yao. Yesu Kristo ni yule yule jana, leo na hata milele. Msiruhusu aina yoyote ya mafundisho mageni yawaongoze hadi katika njia isiyo sahihi. Itegemeeni neema ya Mungu pekee kwa ajili ya nguvu za kiroho, siyo katika sheria kuhusu vyakula. Kuzitii sheria hizi hakumsaidii yeyote.

10 Tunayo sadaka. Na wale makuhani waliotumika ndani ya Hema Takatifu hawawezi kula sadaka tuliyo nayo. 11 Kuhani mkuu hubeba damu za wanyama hadi Patakatifu pa Patakatifu na hutoa damu hiyo kwa ajili ya dhambi. Lakini miili ya wanyama hao huchomwa nje ya kambi. 12 Hivyo Yesu naye alitesekea nje ya mji. Alikufa ili awatakase watu wake kwa damu yake mwenyewe. 13 Hivyo tumwendee Yesu nje ya kambi na kuikubali aibu hiyo hiyo aliyoipata yeye. 14 Hatuna mji unaodumu milele hapa duniani. Lakini tunaungoja mji tutakaoupata hapo baadaye. 15 Hivyo kwa njia ya Yesu hatupaswi kuacha kumtolea Mungu sadaka zetu. Dhabihu hizo ni sifa zetu, zinazotoka katika vinywa vyetu vinavyolisema jina lake. 16 Na msisahau kutenda mema na kushirikishana na wengine mlivyo navyo, kwa sababu sadaka kama hizi zinamfurahisha sana Mungu.

17 Muwatii viongozi wenu. Muwe tayari kufanya yale wanayowaambia. Wanawajibika katika maisha yenu ya kiroho, hivyo nyakati zote wanaangalia jinsi ya kuwalinda ninyi. Muwatii ili kazi yao iwafurahishe wao, siyo kupata majonzi. Haitawasaidia ninyi mnapowasababishia matatizo.

18 Endeleeni kutuombea. Tunajisikia tuko sahihi katika tunayoyafanya, kwa sababu nyakati zote tunajitahidi kadri tuwezavyo. 19 Na nawasihi muombe ili Mungu anirudishe tena kwenu mapema. Nalitamani sana hili kuliko kitu chochote.

20-21 Ninawaombea Mungu wa amani awape ninyi mambo mazuri mnayohitaji ili muweze kufanya anayoyapenda. Mungu ndiye aliyemfufua Bwana Yesu kutoka katika kifo, Mchungaji Mkuu wa kondoo wake. Alimfufua kwa sababu Yesu aliitoa sadaka ya damu yake ili kulianza agano jipya lisilo na mwisho. Namwomba Mungu atuwezeshe kwa njia ya Yesu Kristo kufanya mambo yanayompendeza yeye. Utukufu ni wake milele. Amina.

22 Ndugu na dada zangu, nawasihi msikilize kwa uvumilivu katika yale niliyoyasema. Niliandika barua hii ili kuwatia moyo. Na siyo ndefu sana. 23 Nawataka mjue kwamba ndugu yetu Timotheo ametoka gerezani. Akija kwangu mapema, sote tutakuja kuwaona ninyi.

24 Fikisheni salama zangu kwa viongozi wote na kwa watu wote wa Mungu. Wote walioko Italia wanawasalimuni.

25 Naomba neema ya Mungu iwe nanyi nyote.

Error: Book name not found: Amos for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Luka 2

Kuzaliwa kwa Yesu

(Mt 1:18-25)

Ulikuwa wakati ambapo amri ilitolewa na Kaisari Augusto kwamba watu wote wanaoishi katika utawala wote wa Rumi[a] wahesabiwe na kuorodheshwa[b] katika kumbukumbu za serikali. Orodha hii ilikuwa ya kwanza tangu Kirenio alipokuwa gavana wa Shamu. Kila mtu alikwenda katika mji aliozaliwa ili akahesabiwe na kuingizwa katika orodha hiyo.

Hivyo Yusufu alitoka Nazareti, mji uliokuwa katika jimbo la Galilaya na kwenda katika mji wa Bethlehemu uliokuwa katika jimbo la Uyahudi. Pia, mji huu ulijulikana kama mji wa Daudi. Yusufu alikwenda Bethlehemu kwa sababu alikuwa mzaliwa wa ukoo wa Daudi. Yusufu alijiandikisha akiwa pamoja na Mariamu kwani alikuwa tayari amemchumbia ili amwoe. Na Mariamu alikuwa mjamzito. Yusufu na Mariamu walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua ulifika. Akamzaa mwanawe wa kwanza. Akamvingirishia nguo vizuri, kisha akamlaza katika hori la kulishia mifugo.[c] Walimweka humo kwa sababu chumba cha wageni kilikuwa kimejaa.

Wachungaji wa Mifugo Wajulishwa Kuhusu Yesu

Usiku ule, baadhi ya wachungaji walikuwa mashambani nje ya mji wa Bethlehemu wakilinda kondoo zao. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukaangaza kuwazunguka, wakaogopa sana. 10 Malaika akawaambia, “Msiogope, kwa kuwa nimewaletea habari njema zitakazowafurahisha watu wa Mungu wote. 11 Kwa sababu leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo,[d] Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: Mtamkuta mtoto mchanga amevingirishiwa nguo na amelala katika hori la kulishia mifugo.”

13 Kisha malaika pamoja na jeshi kubwa la mbinguni wakaanza kumsifu Mungu, wakisema:

14 “Atukuzwe Mungu juu mbinguni,
    na amani iwepo duniani
    kwa watu wote wanaompendeza.”

15 Malaika walipoondoka kurudi mbinguni, wale wachungaji wakaambiana wakisema, “Twendeni Bethlehemu, tukalione jambo hili lililotokea, ambalo Bwana ametujulisha.”

16 Wakaenda haraka, wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala katika hori la kulishia mifugo. 17 Wachungaji walipomwona huyo mtoto, walisimulia kile walichoambiwa na malaika kuhusu mtoto. 18 Kila aliyesikia maelezo ya wachungaji, alishangaa. 19 Mariamu aliendelea kuyatafakari mambo haya, na kuyaweka moyoni. 20 Wachungaji waliirudia mifugo yao, wakawa wanamsifu na kumshukuru Mungu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona. Ilikuwa kama walivyoambiwa na malaika.

21 Ilipofika siku ya nane mtoto alitahiriwa, akaitwa Yesu. Hili ndilo jina alilopewa na malaika kabla mama yake hajaibeba mimba yake.

Yesu Atambulishwa Hekaluni

22 Muda wa kutakaswa ulimalizika, kama ilivyotakiwa na Sheria ya Musa baada ya mtoto kuzaliwa.[e] Baada ya hapo walimpeleka Yesu Yerusalemu na kumweka mbele za Bwana. 23 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana: Mzaliwa wa kwanza akiwa mtoto wa kiume, atolewe wakfu kwa ajili ya Bwana.[f] 24 Pia Mariamu na Yusufu walikwenda Yerusalemu kutoa dhabihu kama Sheria ya Bwana inavyosema kuwa, “Ni lazima utoe dhabihu ya jozi moja ya hua[g] au makinda mawili wa njiwa.”

Simeoni Amwona Yesu

25 Alikuwepo mtu mmoja aliyeishi katika mji wa Yerusalemu, mtu huyu aliitwa Simeoni. Alikuwa mtu mwema na mcha Mungu na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. Alikuwa akiusubiri wakati ambao Mungu angeisaidia Israeli. 26 Roho Mtakatifu alimwambia kwamba asingekufa kabla ya kumwona Masihi kutoka kwa Bwana. 27 Roho Mtakatifu alimwongoza mpaka Hekaluni. Hivyo, alikuwemo Hekaluni wakati Mariamu na Yusufu walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Kiyahudi. 28 Simeoni alimbeba mtoto Yesu mikononi mwake, akamshukuru Mungu na kusema,

29 “Sasa, Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako nife kwa amani
    kwa kuwa umeitimiza ahadi yako kwangu.
30 Nimeona kwa macho yangu namna utakavyowaokoa watu wako.
31     Sasa watu wote wanaweza kuuona mpango wako.
32 Yeye ni mwanga wa kuionesha njia yako kwa mataifa mengine,
    na atawaletea heshima watu wako Israeli.”

33 Mariamu na Yusufu walishangazwa sana na maneno aliyosema Simeoni kuhusu Yesu. 34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu; “Wayahudi wengi wataanguka na wengi watainuka kwa sababu ya mtoto huyu. Atakuwa ishara kutoka kwa Mungu, lakini baadhi ya watu watamkataa. 35 Mawazo ya siri ya watu wengi yatajulikana. Na mambo yatakayotokea yatakuumiza, kama upanga unaokuchoma moyoni.”

Ana Amwona Yesu

36 Alikuwapo nabii aliyeitwa Ana binti Fanueli, kutoka katika kabila la Asheri. Alikuwa mwanamke mzee sana. Aliishi na mume wake kwa miaka saba, 37 kabla ya mume wake kufa na kumwacha peke yake. Na sasa alikuwa na umri wa miaka themanini na nne. Ana alikuwa Hekaluni daima, hakutoka. Alimwabudu Mungu kwa kufunga na kuomba usiku na mchana.

38 Simeoni alipokuwa anazungumza na Yusufu na Mariamu, Ana alikwenda walipokuwa na akaanza kumsifu Mungu na kuwaambia kuhusu Yesu watu wote waliokuwa wanasubiri Mungu kuikomboa Yerusalemu.

Yusufu, Mariamu na Yesu Warudi Nyumbani

39 Yusufu na Mariamu walipotimiza mambo yote yanayotakiwa katika sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, katika mji wao wa Nazareti. 40 Mtoto Yesu aliendelea kukua na kuwa kijana mwenye nguvu na aliyejaa hekima nyingi. Na Mungu alikuwa anambariki.

Yesu Akiwa Mvulana

41 Kila mwaka wazazi wa Yesu walikwenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. 42 Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda kwenye sikukuu kama ilivyokuwa desturi ya Kiyahudi. 43 Sikukuu ilipokwisha, walirudi nyumbani, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kutambua. 44 Walianza kumtafuta kwa jamaa na rafiki zao baada ya kusafiri kutwa nzima, wakidhani kuwa alikuwa pamoja nao katika msafara. 45 Walipomkosa, walirudi Yerusalemu kumtafuta.

46 Ikawa baada ya siku tatu wakamkuta Hekaluni, amekaa katikati ya walimu wa dini, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Na wote waliomsikiliza walishangazwa sana kwa ufahamu wake na majibu yake ya busara. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa pia, ndipo mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umefanya hivi? Mimi na baba yako tulikuwa na wasiwasi sana, na tumekuwa tukikutafuta.”

49 Yesu akawaambia, “Kwa nini mlikuwa mnanitafuta? Mnapaswa kujua kuwa inanilazimu kuwemo nyumbani mwa Baba yangu?” 50 Lakini wao hawakuelewa alichowaambia.

51 Yesu alirudi pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii. Mama yake aliendelea kuyaweka mambo haya yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International