Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Maagizo ya Mwisho na Salamu
12 Tunawaomba mwatambue wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao, kama wafuasi wa Bwana, wanatumika kama viongozi wenu na kuwafundisha namna ya kuishi. 13 Wapeni heshima ya hali ya juu na upendo kwa sababu ya kazi wanayofanya.
Ishini kwa amani kila mmoja na mwenzake. 14 Tunawasihi, kuwaonya wale wanaokataa kuishi kwa kuwajibika.[a] Watieni moyo wanaoogopa. Wasaidieni walio dhaifu. Mvumilieni kila mmoja. 15 Asiwepo anae jaribu kulipiza baya kwa baya. Lakini kila mara mfanye lililo jema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
16 Mwe na furaha daima. 17 Msiache kuomba. 18 Shukuruni kwa kila jambo. Hivi ndivyo Mungu anavyotutaka tuishi katika Kristo Yesu.
19 Msiizimishe kazi ya Roho Mtakatifu. 20 Msiuchukulie unabii kama kitu kisicho cha muhimu. 21 Lakini pimeni kila kitu. Lishikeni lililo jema, 22 na mkae mbali na kila aina ya ovu.
© 2017 Bible League International