Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Gen for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waefeso 1:3-14

Baraka za Rohoni katika Kristo

Sifa kwake Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Katika Kristo, Mungu ametupa baraka zote za rohoni zilizoko mbinguni. Kwa kuwa anatupenda alituchagua katika Kristo kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu ili tuwe watakatifu wake, tusio na hatia tunaoweza kusimama mbele zake. Aliamua tangu mwanzo kutufanya kuwa watoto wake kupitia Yesu Kristo. Hivi ndivyo Mungu alivyotaka na ilimpendeza yeye kufanya hivyo. Sifa kwake Mungu kwa sababu ya neema yake ya ajabu aliyotupa bure kupitia Kristo anayempenda.

Tumewekwa huru katika Kristo kupitia sadaka ya damu yake. Tumesamehewa dhambi kwa sababu ya wingi na ukuu wa neema ya Mungu. Mungu alitupa bure neema hiyo yote, pamoja na hekima na uelewa wote, na ametuwezesha kuujua mpango wake wa siri. Hivi ndivyo Mungu alitaka, na alipanga kuutekeleza kupitia Kristo. 10 Lengo la Mungu lilikuwa kuukamilisha mpango wake muda sahihi utakapofika. Alipanga kuwa vitu vyote vilivyoko mbinguni na duniani viunganishwe pamoja na Kristo kama kichwa.

11 Tulichaguliwa katika Kristo ili tuwe milki ya Mungu. Mungu alikwisha panga ili tuwe watu wake, kwa sababu ndivyo alivyotaka. Na ndiye ambaye hufanya kila kitu kifanyike kulingana na utashi na maamuzi yake. 12 Sisi Wayahudi ndiyo tuliokuwa wa kwanza kutumaini katika Kristo. Na tulichaguliwa ili tuweze kumletea sifa Mungu katika utukufu wake wote. 13 Ndivyo ilivyo hata kwenu ninyi. Mliusikia ujumbe wa kweli, yaani Habari Njema kuhusu namna ambavyo Mungu anavyowaokoa. Mlipoisikia Habari Njema hiyo, mkamwamini Kristo. Na katika Kristo, Mungu aliwatia alama maalum kwa kuwapa Roho Mtakatifu aliyeahidi. 14 Roho ni malipo ya kwanza yanayothibitisha kuwa Mungu atawapa watu wake kila kitu alichonacho kwa ajili yao. Sisi sote tutaufurahia uhuru kamili uliowekwa tayari kwa ajili ya walio wake. Na hili litamletea Mungu sifa katika utukufu wake wote.

Yohana 1:29-34

Yesu, Mwanakondoo wa Mungu

29 Siku iliyofuata Yohana akamwona Yesu akija kwake na kusema, “Tazama, Mwanakondoo wa Mungu mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu.” 30 Huyu ndiye niliyezungumza habari zake niliposema, “Kuna mtu anayekuja baada yangu aliye mkuu zaidi yangu, kwa sababu yeye aliishi muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwangu.” 31 Nami sikumjua yeye ni nani. Lakini nilikuja kuwabatiza watu kwa maji ili watu wa Israeli waelewe kuwa huyo ndiye Masihi.

32-34 Kisha Yohana akasema maneno yafuatayo ili kila mtu asikie, “Mimi pia sikujua nani hasa alikuwa Masihi. Lakini yule aliyenituma kubatiza aliniambia, ‘Utamwona Roho akishuka na kutua kwa mtu. Huyo ndiye atakayewabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.’ Nami nimeyaona haya yakitokea. Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama njiwa na kutulia juu ya mtu huyu. Hivyo haya ndiyo ninayowaambia watu: ‘Yeye huyo ndiye Mwana wa Mungu.’”[a]

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International