Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Isa for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Wathesalonike 3:6-18

Wajibu wa Kufanya kazi

Kwa mamlaka ya Bwana wetu Yesu Kristo tunawaambia kukaa mbali na mwamini yeyote anayekataa kufanya kazi. Watu kama hao wanaokataa kufanya kazi hawafuati mafundisho tuliyowapa. Ninyi wenyewe mnafahamu kwamba mnatakiwa kuishi kwa kuiga mfano wetu. Hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi wala hatukuishi pasipo utaratibu unaofaa. Hatukupokea chakula kutoka kwa yeyote bila ya kukilipia. Tulifanya kazi ili tusiwe mzigo kwa yeyote. Tulifanya kazi usiku na mchana. Tulikuwa na haki ya kuomba mtusaidie. Lakini tulifanya kazi ili tuwe mfano wa kuigwa nanyi. 10 Tulipokuwa nanyi, tuliwapa kanuni hii: “Yeyote asiyefanya kazi asile.”

11 Tunasikia kwamba watu wengine katika kundi lenu wanakataa kufanya kazi. Hawashughuliki kufanya kazi badala yake wanashughulika kwa kuyafuatilia maisha ya wengine. 12 Maagizo yetu kwao ni kuwakataza kuwasumbua wengine, waanze kufanya kazi na kupata chakula chao wenyewe. Ni kwa mamlaka ya Bwana Yesu Kristo tuwaagize kufanya hivi. 13 Msichoke kabisa kutenda wema.

14 Wakiwapo wengine huko wanaokataa kufanya tunayowaambia katika barua hii, basi mkumbuke wao ni kina nani. Msichangamane nao. Ndipo pengine wanaweza kujisikia aibu. 15 Lakini msiwafanye kama adui. Washaurini waachane na tabia hiyo kama watu wa nyumbani mwake Mungu.

Maneno ya Mwisho

16 Tunaomba kwamba Bwana wa amani awape amani wakati wote na kwa njia yo yote. Bwana atakuwa pamoja nanyi nyote.

17 Hizi ni salamu zangu kwa mwandiko wangu: Paulo. Ninafanya hivi katika barua zangu zote kuonesha zinatoka kwangu. Hivi ndivyo ninavyoandika.

18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.

Luka 22:31-38

Petro Atajaribiwa na Kushindwa

(Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Yh 13:36-38)

31 Shetani ameomba ili awapepete kwa nguvu kama mkulima anavyopepeta ngano kwenye ungo ili mwanguke. Simoni, Simoni,[a] 32 nimekuombea ili usipoteze imani yako! Wasaidie ndugu zako kuwa imara utakaponirudia.”

33 Lakini Petro akamwambia Yesu, “Bwana, niko tayari kufungwa gerezani pamoja nawe. Hata kufa pamoja nawe!”

34 Lakini Yesu akasema, “Petro, asubuhi kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.”

Iweni Tayari kwa Matatizo

35 Kisha Yesu akawaambia mitume, “Kumbukeni nilipowatuma bila pesa, mkoba, wala viatu. Je, mlipungukiwa chochote?”

Mitume wakajibu, “Hapana.”

36 Yesu akawaambia, “Lakini sasa kama una pesa au mkoba, uchukue pamoja nawe. Kama huna upanga, uza koti lako ukanunue. 37 Maandiko yanasema, ‘Alidhaniwa kuwa mhalifu.’(A) Maandiko haya lazima yatimizwe. Yaliyoandikwa kuhusu mimi yanatimilika sasa.”

38 Wafuasi wakasema, “Tazama Bwana, hapa kuna panga mbili.”

Yesu akawaambia, “Nyamazeni, acheni mazungumzo ya namna hiyo!”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International