馬太福音 4
Chinese Standard Bible (Traditional)
耶穌受試探
4 隨後,耶穌被聖靈領到曠野去,受魔鬼的試探。 2 耶穌禁食了四十晝夜,後來就餓了。 3 那試探者前來對他說:「你如果是神的兒子,就吩咐這些石頭變成食物吧!」
4 耶穌回答說:「經上記著:
『人活著不是單靠食物,
而是靠神口裡所出的每一句話。』[a]」
5 接著,魔鬼帶他到聖城,讓他站在聖殿的頂端, 6 對他說:「你如果是神的兒子,就跳下去吧!因為經上記著:
『他會為你吩咐他的天使;
他們會用手托住你,
免得你的腳撞在石頭上。』[b]」
7 耶穌對他說:「經上又記著:『不可試探主——你的神。』[c]」
8 接著,魔鬼帶耶穌上了一座很高的山,給他看世界萬國和萬國的榮耀, 9 對他說:「你如果俯伏拜我,我就把這一切都給你。」
10 耶穌對他說:「撒旦,退去[d]!因為經上記著:
『要敬拜主——你的神,
唯獨事奉他。』[e]」
11 於是,魔鬼離開了耶穌。看哪,有天使們前來伺候他。
在加利利的服事
12 耶穌聽說約翰被逮捕了,就退到加利利地區。 13 後來,他離開拿撒勒,來到西布倫和拿弗他利境內,住在湖邊的迦百農。 14 這是為要應驗那藉著先知以賽亞所說的話:
17 從那時候起,耶穌開始傳道,說:「你們應當悔改,因為天國近了。」
第一批門徒
18 耶穌在加利利湖邊行走,看見兄弟兩個人,就是那叫彼得的西門和他弟弟[h]安得烈,正在湖裡撒網;他們本來是漁夫。 19 耶穌就對他們說:「來跟從我!我將要使你們成為得人的漁夫。」 20 他們立刻捨棄漁網,跟從了耶穌。
21 耶穌從那裡往前走,看見另外兩個兄弟,就是西庇太的兒子雅各和他弟弟約翰,正在船上與他們的父親西庇太一起修補漁網。耶穌就召喚他們, 22 他們立刻捨棄了船,告別他們的父親,跟從了耶穌。
教導、傳道、治病
23 耶穌走遍全加利利,在他們的會堂裡教導人,傳天國的福音,並且使民中各樣的疾病和各樣的症狀痊癒。 24 他的消息就在全敘利亞省傳開了。人們把所有的病人,就是患各種疾病的、受疼痛折磨的、有鬼魔附身的、癲癇的、癱瘓的,都帶到耶穌那裡。耶穌就使他們痊癒。 25 於是有一大群人從加利利、德卡波利斯、耶路撒冷、猶太和約旦河對岸來,跟隨耶穌。
Mathayo 4
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yesu Ajaribiwa na Shetani
(Mk 1:12-13; Lk 4:1-13)
4 Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza Yesu hadi nyikani ili akajaribiwe na Shetani. 2 Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana. 3 Mjaribu[a] akamwendea na akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, basi yaamuru mawe haya yawe mikate.”
4 Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”(A)
5 Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. 6 Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema,
‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea,
ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”(B)
7 Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”(C)
8 Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani. 9 Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.”
10 Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake!’”(D)
11 Baada ya hayo, Shetani akamwacha. Ndipo malaika wakaja kumhudumia.
Yesu Aanza Kazi yake Galilaya
(Mk 1:14-15; Lk 4:14-15)
12 Yesu aliposikia kuwa Yohana alikuwa amefungwa gerezani, alirudi katika wilaya ya Galilaya. 13 Lakini aliondoka Nazareti. Alikwenda kuishi Kapernaumu, mji ulio kando kando ya Ziwa Galilaya katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14 Hili lilitokea ili kutimiza maneno aliyosema nabii Isaya:
15 “Sikilizeni, enyi nchi ya Zabuloni na Naftali,
nchi iliyo kando ya barabara iendayo baharini,
ng'ambo ya Mto Yordani!
Galilaya, wanapokaa Mataifa.
16 Watu wanaoishi katika giza ya kiroho,
nao wameiona nuru iliyo kuu.
Nuru hiyo imeangaza kwa ajili yao wale
wanaoishi katika nchi yenye giza kama kaburi.”(E)
17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”
Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi
(Mk 1:16-20; Lk 5:1-11)
18 Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao. 19 Yesu akawaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine. Nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 20 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata Yesu papo hapo.
21 Yesu akaendelea kutembea kutoka pale. Akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo. Walikuwa kwenye mashua pamoja na Zebedayo baba yao. Walikuwa wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. Yesu akawaita wamfuate. 22 Mara moja wakaiacha mashua pamoja na baba yao na wakamfuata Yesu.
Yesu Afundisha na Kuponya Watu
(Lk 6:17-19)
23 Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu. 24 Habari kuhusu Yesu zilienea katika nchi yote ya Shamu, na watu waliwaleta wale wote wenye kuteswa na magonjwa na maumivu mbalimbali. Baadhi yao walikuwa na mashetani, wengine walikuwa na kifafa na wengine walikuwa wamepooza. Yesu akawaponya wote. 25 Makundi makubwa ya watu walimfuata; watu kutoka Galilaya, na jimbo lililoitwa Miji Kumi,[b] Yerusalemu, Yuda na maeneo ng'ambo ya Mto Yordani.
Copyright © 2011 by Global Bible Initiative
© 2017 Bible League International