Font Size
Marko 1:16-20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Marko 1:16-20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi
(Mt 4:18-22; Lk 5:1-11)
16 Alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa Galilaya, Yesu alimwona Simoni[a] na Andrea ndugu yake. Hao walikuwa wavuvi na walikuwa wakizitupa nyavu zao ziwani kukamata samaki. 17 Yesu akawaambia, “njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine, nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 18 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata.
19 Kisha Yesu akaendelea mbele kidogo na akawaona ndugu wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na kaka yake Yohana. Yesu aliwaona wakiwa kwenye mashua wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. 20 Naye akawaita mara moja. Hivyo wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua na watu waliowaajiri na kumfuata Yesu.
Read full chapterFootnotes
- 1:16 Simoni Jina lingine la Petro lilikuwa Simoni. Pia katika mistari wa 29,30,36.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International