Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Yesu Aingia Yerusalemu Kama Mfalme
(Mk 11:1-11; Lk 19:28-38; Yh 12:12-19)
21 Yesu na wafuasi wake walipokaribia Yerusalemu, walisimama Bethfage kwenye kilima kinachoitwa Mlima wa Mizeituni. Wakiwa hapo Yesu aliwatuma wafuasi wake wawili mjini. 2 Aliwaambia, “Nendeni kwenye mji mtakaoweza kuuona huko. Mtakapoingia katika mji huo, mtamwona punda na mwanapunda wake.[a] Wafungueni wote wawili, kisha waleteni kwangu. 3 Mtu yeyote akiwauliza kwa nini mnawachukua punda, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji. Atawarudisha mapema.’”
4 Hili lilitimiza maneno yaliyosemwa na nabii:
5 “Waambie watu wa Sayuni,[b]
‘Mfalme wako anakuja sasa.
Ni mnyenyekevu na amempanda punda.
Na amempanda mwana punda dume tena safi.’”(A)
6 Wafuasi walikwenda na kufanya yale walioambiwa na Yesu. 7 Waliwaleta kwake punda jike na mwanapunda. Waliwafunika punda kwa nguo zao na Yesu akaketi juu yao. 8 Akiwa njiani kuelekea Yerusalemu, watu wengi walitandaza mavazi yao barabarani kwa ajili Yake. Wengine walikata matawi ya miti na kuyatandaza barabarani ili kumkaribisha. 9 Wengine walimtangulia Yesu, na wengine walikuwa nyuma yake. Wote walipaza sauti wakisema:
“Msifuni[c] Mwana wa Daudi!
‘Karibu! Mungu ambariki yeye
ajaye katika jina la Bwana!’(B)
Msifuni Mungu wa mbinguni!”
10 Kisha Yesu aliingia Yerusalemu. Watu wote mjini wakataharuki. Wakauliza, “Mtu huyu ni nani?”
11 Kundi la watu waliomfuata Yesu wakajibu, “Huyu ni Yesu. Ni nabii kutoka katika mji wa Nazareti ulio Galilaya.”
5 Hivi ndivyo mnapaswa kufikiri, kuhisi na kutenda katika maisha yenu kwa pamoja, kama vile Kristo Yesu alivyofikiri:
6 Alikuwa sawa na Mungu katika namna zote,
lakini hakufikiri kwamba kuwa sawa na Mungu
kilikuwa kitu cha manufaa kwake.
7 Badala yake, aliacha kila kitu,
hata sehemu yake pamoja na Mungu.
Akakubali kuwa kama mtumwa,
akiwa katika umbo la binadamu.
Wakati wa maisha yake kama mtu,
8 Alijinyenyekeza na akawa mtiifu kabisa kwa Mungu,
hata jambo hilo liliposababisha kifo chake msalabani.
9 Hivyo ndiyo sababu Mungu alimpa mahali pa heshima sana,
na akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.
10 Hivyo kila mtu atasujudu kumheshimu Yesu.
Kila mmoja aliye mbinguni, duniani na wale walio chini ya dunia.
11 Wote watakiri kwamba, “Yesu Kristo ni Bwana,”
na hili litamtukuza Mungu Baba.
Yuda Akubali Kuwasaidia Adui wa Yesu
(Mk 14:10-11; Lk 22:3-6)
14 Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu alikwenda kuzungumza na wakuu wa makuhani. 15 Akasema, “Nikimkabidhi Yesu kwenu, mtanilipa nini?” Makuhani walimpa sarafu thelathini za fedha. 16 Kuanzia siku hiyo, Yuda alianza kutafuta muda mzuri wa kumsaliti Yesu.
Karamu ya Pasaka
(Mk 14:12-21; Lk 22:7-14,21-23; Yh 13:21-30)
17 Ilipofika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wafuasi wake walimjia Yesu na kumwambia, “Tutaandaa kila kitu kwa ajili yako ili ule mlo wa Pasaka. Unataka tuandae wapi mlo wa Pasaka?”
18 Yesu akajibu, “Nendeni mjini kwa mtu ninayemfahamu. Mwambieni kuwa Mwalimu anasema, ‘Muda uliowekwa kwa ajili yangu umekaribia sana. Mimi na wafuasi wangu tutakula mlo wa Pasaka katika nyumba yako.’” 19 Walitii na kufanya kama Yesu alivyowaambia. Waliandaa mlo wa Pasaka.
20 Jioni ilipowadia, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 21 Walipokuwa wakila Yesu akasema, “Niaminini, ninapowaambia kuwa mmoja wenu ninyi kumi na wawili atanikabidhi kwa maadui zangu.”
22 Wanafunzi walisikitika sana waliposikia hili. Kila mmoja akasema, “Bwana, hakika si mimi!”
23 Yesu akajibu, “Yeye aliyechovya mkate wake katika kikombe kile kile nilichochovya mimi ndiye atakayenisaliti. 24 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama Maandiko yanavyosema. Lakini ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe. Ni bora mtu huyo asingezaliwa.”
25 Ndipo Yuda, ambaye ndiye angemsaliti, akamwambia Yesu, “Mwalimu, hakika si mimi unayemzungumzia, ama ndiye?”
Yesu akamjibu, “hicho ndicho unachosema.”
Chakula cha Bwana
(Mk 14:22-26; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)
26 Walipokuwa wakila, Yesu alichukua baadhi ya mikate na akamshukuru Mungu. Alimega baadhi ya vipande, akawapa wafuasi wake na akasema, “Chukueni mkate huu na mle. Ni mwili wangu.”
27 Kisha akachukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu na akawapa. Akasema, “Kila mmoja wenu anywe divai iliyo katika kikombe hiki. 28 Divai hii ni damu yangu, itakayomwagika ili kusamehe dhambi za watu wengi na kuanza Agano Jipya ambalo Mungu analifanya na watu wake. 29 Ninataka mjue kuwa, hii ni mara ya mwisho nitakunywa divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”
30 Waliimba wimbo kwa pamoja kisha wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni.
Yesu Asema Wafuasi Wake Watamwacha
(Mk 14:27-31; Lk 22:31-34; Yh 13:36-38)
31 Yesu akawaambia wafuasi wake, “Usiku wa leo ninyi nyote mtapoteza imani yangu kwangu. Maandiko yanasema,
‘Nitamwua mchungaji,
na kondoo watatawanyika.’(A)
32 Lakini baada ya kuuawa, nitafufuka Kisha nitakwenda Galilaya. Nitakuwa huko kabla ninyi hamjaenda huko.”
33 Petro akajibu, “Wafuasi wengine wote wanaweza kupoteza imani juu yako. Lakini imani yangu haitatetereka.”
34 Yesu akajibu, “Ukweli ni huu, usiku wa leo utasema haunifahamu. Utanikana mara tatu kabla jogoo hajawika.”
35 Lakini Petro akajibu, “Sitasema kwamba sikufahamu! Mimi hata nitakufa pamoja nawe!” Na wafuasi wengine wote wakasema kitu hicho hicho.
Yesu Aomba Akiwa Peke Yake
(Mk 14:32-42; Lk 22:39-46)
36 Kisha Yesu akaondoka pamoja na wafuasi wake na kwenda mahali panapoitwa Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa wakati ninakwenda mahali pale kuomba.” 37 Alimwambia Petro na wana wawili wa Zebedayo waende pamoja naye. Kisha akaanza kuhuzunika na kuhangaika. 38 Yesu akamwambia Petro na wana wa Zebedayo, “Moyo wangu ni mzito na wenye huzuni hata kujisikia kana kwamba huzuni hiyo itaniua. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
39 Kisha Yesu akaenda mbele kidogo. Akainama hadi chini uso wake ukiigusa nchi akiomba na akasema, “Baba yangu, ikiwezekana, usifanye nikinywee kikombe hiki cha mateso.[a] Lakini fanya lile ulitakalo na si lile ninalolitaka mimi.” 40 Kisha akarudi walipokuwa wafuasi wake na akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Je hamkuwa na uwezo wa kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? 41 Amkeni kesheni na kuomba ili muyashinde majaribu. Roho zenu zinataka kufanya mambo sahihi, lakini miili yenu ni dhaifu.”
42 Kisha Yesu akaenda mara ya pili na akaomba akisema, “Baba yangu, ikiwa ni lazima nikinywee kikombe hiki na haiwezekani nikakwepa, basi mapenzi yako na yatimizwe.”
43 Kisha akarudi na kwenda walipokuwa wafuasi wake, akawakuta wamelala tena. Hawakuweza kukesha. 44 Hivyo akawaacha akaenda tena kuomba. Mara hii ya tatu alipokuwa anaomba akasema kama alivyosema hapo mwanzo.
45 Kisha Yesu akawarudia wafuasi wake na akasema, “Bado mnalala na kupumzika? Wakati wa Mwana wa Adamu kukabidhiwa kwa wenye dhambi umewadia. 46 Simameni! Tuondoke. Tazama yeye atakayenikabidhi anakuja.”
Yesu Akamatwa
(Mk 14:43-50; Lk 22:47-53; Yh 18:3-12)
47 Yesu alipokuwa anazungumza, Yuda mmoja wa wanafunzi wake kumi na mbili alifika akiwa na kundi kubwa la watu, waliokuwa wamebeba majambia na marungu. Walikuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 48 Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” 49 Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.
50 Yesu akajibu, “Rafiki yangu, fanya ulilokuja kufanya.”
Kisha wale watu wakaja na kumkamata Yesu. 51 Jambo hili lilipotokea, mmoja wa wafuasi wa Yesu alichukua jambia lake na kumkata sikio mtumishi wa kuhani mkuu.
52 Yesu akamwambia, “Rudisha jambia lako mahali pake. Atumiaye jambia atauawa kwa jambia. 53 Hakika unajua kuwa ningemwomba Baba yangu yeye angenipa zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika. 54 Lakini hilo lisingekubaliana na yale Maandiko, yanayosema hivi ndivyo ilivyopasa itokee.”
55 Kisha Yesu akaliambia kundi, “Kwa nini mnakuja kunikamata mkiwa na mikuki na marungu kama vile mimi ni mhalifu? Nimekuwa nakaa eneo la Hekalu nikifundisha kila siku. Kwa nini hamkunikamata kule? 56 Lakini mambo haya yote yametokea ili kutimiza Maandiko yaliyoandikwa na manabii.” Ndipo wafuasi wake wote wakamwacha na kukimbia.
Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini
(Mk 14:53-65; Lk 22:54-55,63-71; Yh 18:13-14,19-24)
57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu. Walimu wa Sheria na viongozi wazee wa Kiyahudi walikuwa wamekusanyika huko. 58 Petro alimfuata Yesu lakini alikuwa mbali kidogo. Alimfuata mpaka katika ua wa nyumba ya kuhani mkuu. Petro alienda uani na akakaa pamoja na walinzi. Alitaka kuona nini kingetokea.
59 Viongozi wa makuhani na baraza kuu walijaribu kutafuta kosa ili waweze kumwua Yesu. Walijaribu kutafuta watu ili wadanganye kuwa Yesu alifanya kosa. 60 Watu wengi walikuja na akasema uongo kuhusu Yesu. Lakini baraza lilishindwa kupata ushahidi wa kuutumia ili kumwua. Ndipo watu wawili walikuja 61 na akasema, “Mtu huyu[b] alisema, ‘Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’”
62 Kisha kuhani mkuu alisimama na kumwambia Yesu, “Huna neno lolote la kujitetea dhidi ya mashtaka haya juu yako? Wanasema kweli?” 63 Lakini Yesu hakusema neno lolote.
Kisha kuhani mkuu akamwambia Yesu, “Apa mbele za Mungu aliye hai kwamba utatuambia kweli. Je, wewe ni Masihi, Mwana wa Mungu?”
64 Yesu akajibu, “Unaweza akasema hivyo, Mimi ndiye. Lakini ninawaambia, kitambo kidogo mtamwona Mwana wa Adamu akiwa amekaa upande wa kuume wa Mungu, mwenye Nguvu. Na mtamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
65 Kuhani mkuu aliposikia hili, alilarua vazi lake kwa hasira. Akasema, “Mtu huyu amemtukana Mungu! Hatuhitaji mashahidi zaidi. Ninyi nyote mmesikia matusi yake. 66 Mnasemaje?”
Viongozi wa Kiyahudi wakajibu, “Ana hatia, na ni lazima afe.”
67 Na baadhi ya waliokuwa pale wakamtemea mate Yesu usoni na kumpiga makonde na wengine walimpiga makofi. 68 Wakasema, “Tuonyeshe kuwa wewe ni nabii, Masihi! Nani amekupiga!”
Petro Amkana Yesu
(Mk 14:66-72; Lk 22:56-62; Yh 18:15-18,25-27)
69 Petro alipokuwa amekaa nje uani, msichana mtumishi akamwendea. Akasema, “Ulikuwa pamoja na Yesu, yule mtu kutoka Galilaya.”
70 Lakini Petro akamwambia kila mtu aliyekuwa pale kuwa si kweli. Akasema “Sijui unachosema.”
71 Kisha akaondoka uani. Akiwa kwenye lango msichana mtumishi akamwona na akawaambia watu waliokuwa pale, “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.”
72 Kwa mara nyingine tena Petro akasema hakuwa pamoja na Yesu. Akasema, “Ninaapa kwa Mungu, simfahamu mtu huyu!”
73 Baada ya muda mfupi baadaye, watu waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro na kumwambia, “Tunajua wewe ni mmoja wao. Hata namna unavyoongea inaonesha wazi kuwa ndivyo hivyo.”
74 Kisha Petro akaanza kujiapiza mwenyewe ikiwa anaongopa. Akasema, “Ninaapa kwa Mungu, simfahamu mtu huyu!” Mara alipomaliza akasema hili, jogoo akawika. 75 Kisha akakumbuka maneno alivyoambiwa na Yesu kuwa: “Kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.” Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu sana.
Yesu Apelekwa kwa Gavana Pilato
(Mk 15:1; Lk 23:1-2; Yh 18:28-32)
27 Mapema asubuhi, viongozi wote wa makuhani na viongozi wazee walikutana na kuamua kumwua Yesu. 2 Wakamfunga kamba, wakamwondoa na kwenda kumkabidhi kwa Pilato, gavana wa Kirumi.
Yuda Ajiua
(Mdo 1:18-19)
3 Baada ya kumkabidhi Yesu, Yuda aliona kila kitu kilichotokea na kujua kuwa wameamua kumwua Yesu. Naye alihuzunika sana kutokana na kile alichokifanya. Hivyo alirudisha vile vipande thelathini vya sarafu vya fedha kwa wakuu wa makuhani na viongozi wazee. 4 Yuda aliwaambia, “Nimetenda dhambi. Nimemsaliti kwenu mtu asiye na hatia ili auawe.”
Viongozi wa Kiyahudi wakajibu, “Hilo halituhusu. Ni tatizo lako, siyo letu sisi.”
5 Hivyo Yuda akavitupa vipande thelathini vya fedha Hekaluni, kisha akatoka akaenda kujinyonga.
6 Viongozi wa makuhani wakaviokota vile vipande vya fedha Hekaluni. Wakasema, “Sheria yetu haituruhusu kuweka fedha hii katika hazina ya Hekalu, kwa sababu fedha hii imelipwa kwa ajili ya kifo, ni fedha yenye damu.” 7 Hivyo wakaamua kutumia fedha hiyo kwa kununulia shamba linaloitwa Shamba la Mfinyanzi kwa ajili ya kuwazikia wageni wanapokufa wakiwa ziarani katika mji wa Yerusalemu. 8 Ndiyo sababu eneo hilo bado linaitwa Shamba la Damu. 9 Hili lilitimiza maneno ya nabii Yeremia aliposema:
“Walichukua sarafu thelathini za fedha. Hicho ni kiasi ambacho Waisraeli waliamua kulipa kwa ajili ya uhai wake. 10 Walizitumia sarafu hizo thelathini za fedha kununulia shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniamuru.”[c]
Gavana Pilato Amhoji Yesu
(Mk 15:2-5; Lk 23:3-5; Yh 18:33-38)
11 Yesu alisimama mbele ya Gavana, Pilato, ambaye alimwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Waweza kusema hivyo.”
12 Lakini viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi walipomshutumu, hakusema kitu.
13 Hivyo Pilato akamwambia, “Husikii mashtaka haya yote wanayokushtaki wewe? Kwa nini hujibu?”
14 Lakini Yesu hakujibu kitu, gavana alishangaa sana.
Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu
(Mk 15:6-15; Lk 23:13-25; Yh 18:39-19:16)
15 Kila mwaka wakati wa Pasaka, gavana angemwachia huru mfungwa mmoja yeyote ambaye watu wangetaka aachiwe huru. 16 Wakati huo alikuwepo mtu gerezani aliyejulikana kuwa ni mtu mbaya. Mtu huyu aliitwa Baraba.
17 Kundi la watu lilipokusanyika, Pilato aliwaambia, “Nitamwacha huru mtu mmoja. Mnataka nani nimwache huru: Baraba au Yesu aitwaye Masihi?” 18 Pilato alijua kuwa viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu walikuwa wanamwonea wivu.
19 Pilato alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akamtumia ujumbe uliosema, “Usifanye jambo lolote juu ya huyo mtu. Hana hatia. Nimeota ndoto juu yake usiku, na ndoto hiyo imenihangaisha sana.”
20 Lakini viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi waliwaambia watu waombe Baraba aachiwe huru na Yesu auawe.
21 Pilato akasema, “Nina Baraba na Yesu. Je, mnataka nimwache huru yupi?”
Watu wakajibu, “Baraba!”
22 Pilato akauliza, “Sasa nimfanye nini Yesu, aitwaye Masihi?”
Watu wote wakasema, “Mwue msalabani!”
23 Pilato akauliza, “Kwa nini mnataka nimwue Yesu? Amefanya kosa gani?”
Lakini walipaza sauti wakisema, “Mwue msalabani!”
24 Pilato akaona hakuna jambo ambalo angefanya ili kubadili nia yao. Kiukweli ilionekana wazi kuwa kungetokea fujo. Hivyo alichukua maji na kunawa mikono yake[d] mbele yao wote. Akasema, “Sina hatia na kifo cha mtu huyu. Ninyi ndio mnaofanya hili!”
25 Watu wakajibu, “Tutawajibika kwa kifo chake sisi wenyewe na hata watoto wetu!”
26 Kisha Pilato akamwachia huru Baraba. Na akawaambia baadhi ya askari wamchape Yesu viboko. Kisha akamkabidhi Yesu kwa askari ili akauawe msalabani.
Askari wa Pilato Wamdhihaki Yesu
(Mk 15:16-20; Yh 19:2-3)
27 Kisha askari wa Pilato wakamchukua Yesu mpaka kwenye nyumba ya gavana, kikosi kizima cha wale askari kikakusanyika pamoja kumzunguka Yesu. 28 Wakamvua nguo zake na kumvalisha kivazi chekundu.[e] 29 Kisha wakatengeneza taji kutokana na matawi ya miiba na kuiweka kwenye kichwa chake na wakaweka fimbo kwenye mkono wake wa kulia. Kisha kwa kumdhihaki, wakainama mbele zake. Wakasema, “Tunakusalimu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Walimtemea mate. Kisha wakachukua fimbo yake na kuanza kumpiga nayo kichwani. 31 Baada ya kumaliza kumdhihaki, askari walimvua kivazi chekundu na kumvalisha nguo zake. Kisha wakamwongoza kwenda kuuawa msalabani.
Yesu Awambwa Msalabani
(Mk 15:21-32; Lk 23:26-43; Yh 19:17-19)
32 Askari walipokuwa wanatoka mjini wakiwa na Yesu, walimwona mtu mmoja kutoka Kirene aliyeitwa Simoni, na wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu. 33 Walifika mahali palipoitwa Golgotha. (Yaani “Eneo la Fuvu la Kichwa”.) 34 Askari walimpa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo.[f] Lakini alipoionja, alikataa kuinywa.
35 Askari walimgongomea Yesu msalabani, kisha wakacheza kamari ili wagawane nguo za Yesu. 36 Askari walikaa pale ili kumlinda. 37 Wakaweka alama juu ya kichwa chake kuonesha mashtaka dhidi yake yaliyosema: Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.
38 Wahalifu wawili waligongomewa kwenye misalaba pamoja na Yesu, mmoja aliwekwa upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto wa Yesu. 39 Watu waliokuwa wakipita pale walitikisa vichwa vyao na kumtukana Yesu matusi 40 kwa kusema, “Ulisema ungeweza kubomoa Hekalu na kulijenga tena katika siku tatu. Jiokoe mwenyewe! Teremka chini kutoka kwenye huo msalaba ikiwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu!”
41 Viongozi wa Makuhani, walimu wa sheria, na viongozi wazee wa Kiyahudi walikuwepo pale pia. Nao pia walimdhihaki Yesu kama watu wengine walivyofanya. 42 Walisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa yeye mwenyewe! Watu husema kuwa yeye ni mfalme wa Israeli. Ikiwa yeye ni mfalme, ashuke kutoka msalabani. Ndipo tutamwamini. 43 Alimtumaini Mungu. Hivyo Mungu amwokoe sasa, ikiwa hakika Mungu anamtaka. Yeye mwenyewe alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’” 44 Hata wale wahalifu wawili waliokuwa misalabani upande wa kulia na wa kushoto wa Yesu walimtukana.
Yesu Afariki
(Mk 15:33-41; Lk 23:44-49; Yh 19:28-30)
45 Ilipofika adhuhuri, giza liliifunika Israeli yote kwa muda wa masaa matatu. 46 Yapata saa tisa alasiri Yesu alilia kwa sauti kuu akisema, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha peke yangu?”(B)
47 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hili wakasema, “Anamwita Eliya.”[g]
48 Mtu mmoja alikimbia haraka akaenda kuchukua sponji, akaijaza siki, akaifunga kwenye fimbo na akanyoosha fimbo ili kumpa Yesu sponji ili anywe siki. 49 Lakini wengine walisema, “Usimjali. Tunataka tuone ikiwa Eliya atakuja kumsaidia.”
50 Yesu akalia kwa sauti kuu tena, kisha akafa.[h]
51 Yesu alipokufa, pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili. Mpasuko wake ulianzia juu mpaka chini. Kulitokea pia tetemeko la ardhi na miamba ilipasuka. 52 Makaburi yalifunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa walifufuka kutoka kwa wafu. 53 Walitoka makaburini. Na baada ya Yesu kufufuliwa kutoka kwa wafu, walikwenda kwenye mji mtakatifu wa Yerusalemu, na watu wengi waliwaona.
54 Afisa wa jeshi na askari waliokuwa wanamlinda Yesu walitetemeka sana kwa kuogopa tetemeko la ardhi na kila walichokiona kikitokea. Wakasema, “Hakika alikuwa Mwana wa Mungu!”
55 Wanawake wengi waliomfuata Yesu kutoka Galilaya kumhudumia walikuwepo pale wakiangalia wakiwa wamesimama mbali na msalaba. 56 Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu na pia mama yao Yakobo na Yohana[i] alikuwepo pale.
Yesu Azikwa
(Mk 15:42-47; Lk 23:50-56; Yh 19:38-42)
57 Jioni ile, mtu mmoja tajiri aliyeitwa Yusufu alikuja Yerusalemu. Alikuwa mfuasi wa Yesu kutoka katika mji wa Arimathaya. 58 Alikwenda kwa Pilato na akamwomba mwili wa Yesu. Pilato akawaamuru askari wampe Yusufu wa Arimathaya mwili wa Yesu. 59 Aliuchukua mwili na kuuvingirisha katika kitambaa mororo cha kitani safi. 60 Yusufu akauzika mwili wa Yesu katika kaburi mpya alilokuwa amelichonga kwenye mwamba mlimani. Kisha akalifunga kaburi kwa kuvingirisha jiwe kubwa kuziba mlango wa kaburi. Baada ya kufanya hivi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na mwanamke mwingine aliyeitwa Mariamu walikuwa wamekaa karibu na kaburi.
Kaburi la Yesu Lalindwa
62 Siku ile ilikuwa Siku ya Maandalizi. Siku iliyofuata, viongozi wa makuhani na Mafarisayo walimwendea Pilato. 63 Wakamwambia, “Mkuu, tunakumbuka kuwa yule mwongo alipokuwa hai alisema, ‘Nitafufuka kutoka kwa watu katika siku tatu.’ 64 Hivyo amuru ili kaburi lilindwe kwa siku tatu. Wafuasi wake wanaweza kuja na kujaribu kuiba mwili. Kisha wataweza kumwambia kila mtu kuwa alifufuka kutoka kwa wafu. Uongo huo utakuwa hatari zaidi ya hata waliyosema juu yake alipokuwa hai.”
65 Pilato akasema, “Chukueni baadhi ya askari, na mwende mkalinde kaburi kwa namna mnavyojua.” 66 Kisha walikwenda kaburini na kuliweka salama dhidi ya wezi. Walifanya hivi kwa kuliziba kwa jiwe langoni na kuwaweka askari wa kulinda kaburi.
Gavana Pilato Amhoji Yesu
(Mk 15:2-5; Lk 23:3-5; Yh 18:33-38)
11 Yesu alisimama mbele ya Gavana, Pilato, ambaye alimwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Waweza kusema hivyo.”
12 Lakini viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi walipomshutumu, hakusema kitu.
13 Hivyo Pilato akamwambia, “Husikii mashtaka haya yote wanayokushtaki wewe? Kwa nini hujibu?”
14 Lakini Yesu hakujibu kitu, gavana alishangaa sana.
Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu
(Mk 15:6-15; Lk 23:13-25; Yh 18:39-19:16)
15 Kila mwaka wakati wa Pasaka, gavana angemwachia huru mfungwa mmoja yeyote ambaye watu wangetaka aachiwe huru. 16 Wakati huo alikuwepo mtu gerezani aliyejulikana kuwa ni mtu mbaya. Mtu huyu aliitwa Baraba.
17 Kundi la watu lilipokusanyika, Pilato aliwaambia, “Nitamwacha huru mtu mmoja. Mnataka nani nimwache huru: Baraba au Yesu aitwaye Masihi?” 18 Pilato alijua kuwa viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu walikuwa wanamwonea wivu.
19 Pilato alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akamtumia ujumbe uliosema, “Usifanye jambo lolote juu ya huyo mtu. Hana hatia. Nimeota ndoto juu yake usiku, na ndoto hiyo imenihangaisha sana.”
20 Lakini viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi waliwaambia watu waombe Baraba aachiwe huru na Yesu auawe.
21 Pilato akasema, “Nina Baraba na Yesu. Je, mnataka nimwache huru yupi?”
Watu wakajibu, “Baraba!”
22 Pilato akauliza, “Sasa nimfanye nini Yesu, aitwaye Masihi?”
Watu wote wakasema, “Mwue msalabani!”
23 Pilato akauliza, “Kwa nini mnataka nimwue Yesu? Amefanya kosa gani?”
Lakini walipaza sauti wakisema, “Mwue msalabani!”
24 Pilato akaona hakuna jambo ambalo angefanya ili kubadili nia yao. Kiukweli ilionekana wazi kuwa kungetokea fujo. Hivyo alichukua maji na kunawa mikono yake[a] mbele yao wote. Akasema, “Sina hatia na kifo cha mtu huyu. Ninyi ndio mnaofanya hili!”
25 Watu wakajibu, “Tutawajibika kwa kifo chake sisi wenyewe na hata watoto wetu!”
26 Kisha Pilato akamwachia huru Baraba. Na akawaambia baadhi ya askari wamchape Yesu viboko. Kisha akamkabidhi Yesu kwa askari ili akauawe msalabani.
Askari wa Pilato Wamdhihaki Yesu
(Mk 15:16-20; Yh 19:2-3)
27 Kisha askari wa Pilato wakamchukua Yesu mpaka kwenye nyumba ya gavana, kikosi kizima cha wale askari kikakusanyika pamoja kumzunguka Yesu. 28 Wakamvua nguo zake na kumvalisha kivazi chekundu.[b] 29 Kisha wakatengeneza taji kutokana na matawi ya miiba na kuiweka kwenye kichwa chake na wakaweka fimbo kwenye mkono wake wa kulia. Kisha kwa kumdhihaki, wakainama mbele zake. Wakasema, “Tunakusalimu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Walimtemea mate. Kisha wakachukua fimbo yake na kuanza kumpiga nayo kichwani. 31 Baada ya kumaliza kumdhihaki, askari walimvua kivazi chekundu na kumvalisha nguo zake. Kisha wakamwongoza kwenda kuuawa msalabani.
Yesu Awambwa Msalabani
(Mk 15:21-32; Lk 23:26-43; Yh 19:17-19)
32 Askari walipokuwa wanatoka mjini wakiwa na Yesu, walimwona mtu mmoja kutoka Kirene aliyeitwa Simoni, na wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu. 33 Walifika mahali palipoitwa Golgotha. (Yaani “Eneo la Fuvu la Kichwa”.) 34 Askari walimpa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo.[c] Lakini alipoionja, alikataa kuinywa.
35 Askari walimgongomea Yesu msalabani, kisha wakacheza kamari ili wagawane nguo za Yesu. 36 Askari walikaa pale ili kumlinda. 37 Wakaweka alama juu ya kichwa chake kuonesha mashtaka dhidi yake yaliyosema: Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.
38 Wahalifu wawili waligongomewa kwenye misalaba pamoja na Yesu, mmoja aliwekwa upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto wa Yesu. 39 Watu waliokuwa wakipita pale walitikisa vichwa vyao na kumtukana Yesu matusi 40 kwa kusema, “Ulisema ungeweza kubomoa Hekalu na kulijenga tena katika siku tatu. Jiokoe mwenyewe! Teremka chini kutoka kwenye huo msalaba ikiwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu!”
41 Viongozi wa Makuhani, walimu wa sheria, na viongozi wazee wa Kiyahudi walikuwepo pale pia. Nao pia walimdhihaki Yesu kama watu wengine walivyofanya. 42 Walisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa yeye mwenyewe! Watu husema kuwa yeye ni mfalme wa Israeli. Ikiwa yeye ni mfalme, ashuke kutoka msalabani. Ndipo tutamwamini. 43 Alimtumaini Mungu. Hivyo Mungu amwokoe sasa, ikiwa hakika Mungu anamtaka. Yeye mwenyewe alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’” 44 Hata wale wahalifu wawili waliokuwa misalabani upande wa kulia na wa kushoto wa Yesu walimtukana.
Yesu Afariki
(Mk 15:33-41; Lk 23:44-49; Yh 19:28-30)
45 Ilipofika adhuhuri, giza liliifunika Israeli yote kwa muda wa masaa matatu. 46 Yapata saa tisa alasiri Yesu alilia kwa sauti kuu akisema, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha peke yangu?”(A)
47 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hili wakasema, “Anamwita Eliya.”[d]
48 Mtu mmoja alikimbia haraka akaenda kuchukua sponji, akaijaza siki, akaifunga kwenye fimbo na akanyoosha fimbo ili kumpa Yesu sponji ili anywe siki. 49 Lakini wengine walisema, “Usimjali. Tunataka tuone ikiwa Eliya atakuja kumsaidia.”
50 Yesu akalia kwa sauti kuu tena, kisha akafa.[e]
51 Yesu alipokufa, pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili. Mpasuko wake ulianzia juu mpaka chini. Kulitokea pia tetemeko la ardhi na miamba ilipasuka. 52 Makaburi yalifunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa walifufuka kutoka kwa wafu. 53 Walitoka makaburini. Na baada ya Yesu kufufuliwa kutoka kwa wafu, walikwenda kwenye mji mtakatifu wa Yerusalemu, na watu wengi waliwaona.
54 Afisa wa jeshi na askari waliokuwa wanamlinda Yesu walitetemeka sana kwa kuogopa tetemeko la ardhi na kila walichokiona kikitokea. Wakasema, “Hakika alikuwa Mwana wa Mungu!”
© 2017 Bible League International