Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Acheni Mabishano Miongoni Mwenu
10 Ndugu zangu, kwa mamlaka ya Bwana wetu Yesu Kristo, ninawasihi mpatane ninyi kwa ninyi. Msigawanyike katika makundi. Lakini iweni pamoja tena katika kuwaza kwenu na katika nia zenu.
11 Kaka na dada zangu, baadhi ya jamaa wa Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mabishano miongoni mwenu. 12 Baadhi yenu husema, “Mimi ninamfuata Paulo,”[a] na mwingine husema, “Mimi ninamfuata Apolo.” Mwingine husema, “Mimi ninamfuata Petro,”[b] na mwingine husema, “Mimi ninamfuata Kristo.” 13 Kristo hawezi kugawanywa katika makundi. Je, Paulo ndiye alikufa msalabani kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa katika jina la Paulo? 14 Ninashukuru kwa kuwa sikumbatiza mtu yeyote kwenu isipokuwa Krispo na Gayo. 15 Ninashukuru kwa sababu hakuna anayeweza kusema kuwa mlibatizwa katika jina langu. 16 (Niliwabatiza pia watu wote wa nyumbani mwa Stefana, lakini sikumbuki kuwa niliwabatiza watu wengine) 17 Kristo hakunipa kazi ya kubatiza watu. Alinipa kazi ya kuhubiri Habari Njema pasipo kutumia hekima ya maneno, inayoweza kubatilisha nguvu iliyo katika msalaba[c] wa Kristo.
Nguvu ya Mungu na Hekima Katika Kristo Yesu
18 Mafundisho kuhusu msalaba yanaonekana ni ya kipuuzi kwao wao wanaoelekea kwenye uharibifu. Lakini ni nguvu ya Mungu kwetu sisi tunaookolewa.
Yesu Aanza Kazi yake Galilaya
(Mk 1:14-15; Lk 4:14-15)
12 Yesu aliposikia kuwa Yohana alikuwa amefungwa gerezani, alirudi katika wilaya ya Galilaya. 13 Lakini aliondoka Nazareti. Alikwenda kuishi Kapernaumu, mji ulio kando kando ya Ziwa Galilaya katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14 Hili lilitokea ili kutimiza maneno aliyosema nabii Isaya:
15 “Sikilizeni, enyi nchi ya Zabuloni na Naftali,
nchi iliyo kando ya barabara iendayo baharini,
ng'ambo ya Mto Yordani!
Galilaya, wanapokaa Mataifa.
16 Watu wanaoishi katika giza ya kiroho,
nao wameiona nuru iliyo kuu.
Nuru hiyo imeangaza kwa ajili yao wale
wanaoishi katika nchi yenye giza kama kaburi.”(A)
17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”
Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi
(Mk 1:16-20; Lk 5:1-11)
18 Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao. 19 Yesu akawaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine. Nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 20 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata Yesu papo hapo.
21 Yesu akaendelea kutembea kutoka pale. Akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo. Walikuwa kwenye mashua pamoja na Zebedayo baba yao. Walikuwa wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. Yesu akawaita wamfuate. 22 Mara moja wakaiacha mashua pamoja na baba yao na wakamfuata Yesu.
Yesu Afundisha na Kuponya Watu
(Lk 6:17-19)
23 Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu.
© 2017 Bible League International