Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Semicontinuous)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with sequential stories told across multiple weeks.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Exod for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Wafilipi 1:15-21

15 Baadhi ya watu wanahubiri ujumbe wa Kristo kwa sababu wananionea wivu na wanataka watu wawafuate wao badala yangu. Wengine wanahubiri kwa sababu wanataka kusaidia. 16 Wanahubiri kwa sababu ya upendo. Wanafahamu kuwa Mungu ameniweka humu gerezani ili kuitetea Habari Njema. 17 Lakini wengine wanahubiri kuhusu Kristo kwa sababu wanataka kujikweza wenyewe. Chachu yao si safi. Wanafanya hivi kwa kudhani kuwa itanisababishia uchungu mwingi niwapo gerezani. 18 Lakini hiyo haijalishi. Kitu cha muhimu ni kuwa wanawahubiri watu kuhusu Kristo, wakiwa na chachu safi au isiyo safi. Ninafurahi wanafanya hivyo.

Nitaendelea kufurahi, 19 kwa sababu ninajua kwamba kupitia maombi yenu na kipawa cha Roho wa Yesu Kristo mazingira haya magumu hatimaye yataniletea uhuru wangu. 20 Nimejaa tumaini na uhakika, sina sababu yeyote ya kuona haya. Nina uhakika nitaendelea kuwa na ujasiri wa kuhubiri kwa uhuru kama ambavyo nimekuwa. Na Kristo atatukuzwa kwa ninayoyafanya katika mwili wangu, ikiwa nitaishi au nitakufa. 21 Sababu yangu pekee ya kuishi ni kumtumikia Kristo. Kifo kingekuwa bora zaidi.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International