Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Complementary)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with thematically matched Old and New Testament readings.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Zech for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Petro 2:4-21

Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwaacha bila kuwaadhibu. Aliwatupia kuzimu. Aliwaweka malaika wale katika mapango yenye giza, wanakofungiwa mpaka wakati watakapohukumiwa na Mungu.

Na Mungu aliwaadhibu watu waovu walioishi zamani. Alileta gharika katika ulimwengu uliojaa watu waliokuwa kinyume na Mungu. Lakini alimwokoa Nuhu na watu wengine saba waliokuwa pamoja naye. Nuhu ndiye aliyewaambia watu kuhusu kuishi kwa haki.

Pia, Mungu aliiadhibu miji miovu ya Sodoma na Gomora. Aliichoma kwa moto mpaka kila kitu kikawa majivu. Alitumia miji hiyo kama mfano wa kile kitakachowapata watu walio kinyume na Mungu. Lakini alimwokoa Lutu, mtu mwema aliyeishi huko. Lutu aliugua sana moyoni kutokana na mwenendo wa kimaisha usiofaa na matendo ya uasi ya wale watu. Kila siku mtu huyu mwema aliishi miongoni mwa watu walioharibika, na moyo wake mwema uliumia kutokana na uhalifu na uvunjaji wa sheria aliyouona na kusikia.

Unaona namna ambavyo Mungu anajua kuwaokoa wale wanaomheshimu kutokana na matatizo yao. Na Bwana anajua jinsi ya kuwaweka watu waovu kifungoni hadi atakapowaadhibu siku ya hukumu. 10 Hukumu hiyo ni kwa wale ambao daima wanaofuata tamaa za udhaifu wao wa kibinadamu. Hiyo ni kwa ajili ya wale ambao wanadharau mamlaka ya Bwana.

Walimu hawa wa uongo hufanya chochote wanachotaka, na hujivuna sana. Wala hawaogopi kuwanenea mabaya viumbe wenye nguvu walioko angani. 11 Malaika wa Mungu ni hodari zaidi na wana nguvu kuliko viumbe hawa. Lakini hata hivyo malaika hao wa Mungu hawawatukani na kuwanenea mabaya viumbe hawa mbele za Bwana.

12 Lakini walimu hawa wa uongo wanasema uovu dhidi ya mambo wasiyoyaelewa. Wako kama wanyama ambao hufanya mambo bila ya kufikiri, ni kama wanyama wa porini waliozaliwa ili wakamatwe na kuuawa. Nao kama wanyama wataangamizwa. 13 Wamesababisha watu wengi kuteseka. Hivyo hata wao watateseka. Hayo ndiyo malipo yao kwa yale waliyofanya.

Wanadhani ni jambo la kufurahisha kutenda dhambi ambapo kila mtu anaweza kuwaona. Wanazifikiria sherehe zenye matendo yasiyofaa hata wakati wa mchana kweupe. Hivyo wao ni kama madoa ya uchafu na ni fedheha mnapokula pamoja nao. 14 Kila wakati wanapomwona mwanamke, wanamtamani na kumtaka. Wanatenda dhambi kwa njia hii daima. Na wanawasababisha wanyonge kutenda dhambi. Wamejifunza vyema wao wenyewe kuwa walafi. Wako chini ya laana.[a]

15 Walimu hawa wa uongo waliiacha njia sahihi na wakaiendea njia mbaya. Waliifuata njia ile ile aliyoifuata Balaamu. Alikuwa mwana wa Beori, aliyependa kulipwa kwa kufanya mabaya. 16 Alikemewa na punda kwa sababu alikuwa anatenda jamba baya. Punda alizungumza kwa sauti ya kibinadamu na akamzuia nabii yule kutenda kwa wazimu.

17 Walimu hawa wa uongo ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayosukumwa na dhoruba. Mahali penye giza nene pameandaliwa kwa ajili yao. 18 Wanajisifu kwa maneno yasiyo na maana. Wanawaongoza watu katika mitego ya dhambi. Wanawatafuta watu ambao wamechana na maisha ya kutenda dhambi na wanawarudisha tena katika kutenda dhambi. Wanafanya hivi kwa kutumia mambo ya aibu ambayo watu wanataka kuyatenda katika mapungufu yao ya kibinadamu. 19 Walimu hawa wa uongo wanawaahidi watu hao uhuru, lakini wao wenyewe hawako huru. Ni watumwa wa akili iliyoharibiwa na dhambi. Ndiyo, watu ni watumwa wa kitu chochote kinachowashinda.

20 Watu wanaweza kuwekwa huru ulimwenguni kutoka katika matendo ya aibu. Wanaweza kuyakwenda haya kwa kumwamini Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Lakini wakiyarudia maovu hayo na yakawatawala, hali yao inakuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni. 21 Ndiyo, ingekuwa bora kwao kutoijua kamwe njia sahihi. Ingekuwa bora kuliko kuijua njia sahihi kisha kugeuka kutoka katika mafundisho matakatifu waliyopewa.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International