Old/New Testament
Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji
57 Ikawa siku za kujifungua kwake Elizabeti zilipotimia, alizaa mtoto wa kiume . 58 Habari zikawafikia majirani na jamaa jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu. Nao wakafurahi pamoja naye. 59 Mtoto alipokuwa na umri wa siku nane, watu wakaja kuhudhuria tohara yake. Wote wakataka wampe yule mtoto jina la Zakaria, yaani jina la baba yake. 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “La si hilo. Jina lake litakuwa Yohana.” 61 Wakamjibu, “Mbona hakuna mtu katika jamaa yako mwenye jina kama hilo?” 62 Basi wakaamua kumwuliza Zakaria kwa ishara kwamba yeye angependa mtoto aitwe nani. 63 Akaomba mahali pa kuandikia, naye akaandika: “Jina lake ni Yohana.” Watu wote wakastaajabu. 64 Papo hapo uwezo wa kusema ukamrudia Zakaria naye akaanza kumsifu Mungu. 65 Watu wote walioshuhudia jambo hili wakastaajabu mno, na habari hii ikaenea sehemu zote za wilaya ile ya Yudea. 66 Na kila aliyezisikia habari hizi aliwaza moyoni: “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Utabiri Wa Zakaria
67 Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akata biri akisema: 68 “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake ili awakomboe. 69 Naye ametusimamishia nguvu ya wokovu katika ukoo wa Daudi mtumishi wake; 70 kama alivy oahidi kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani: 71 kwamba atatuokoa na maadui zetu na kututoa kutoka katika mikono ya wote watuchukiao. 72 Aliahidi ataonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu 73 aliloagana na baba yetu Ibrahimu: 74 kutuokoa kutoka katika mikono ya adui zetu na kutuwezesha kumtumikia pasipo woga, 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. 76 Na wewe mwanangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia Bwana na kumwandalia njia; 77 na kuwafahamisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na 79 kuwaangazia wote waishio katika giza na katika uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” 80 Yule mtoto akakua na kuko maa kiroho; akaishi nyikani hadi alipoanza kuwahubiria Waisraeli hadharani.
Copyright © 1989 by Biblica