Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Deut for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Marko 14:1-26

Mpango Wa Kumwua Yesu

14 Siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na sherehe ya mikate isiyotiwa chachu, makuhani wakuu na walimu wa sheria wali kuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa siri na kumwua. Wakaambiana, “Jambo hili tusilifanye wakati wa sikukuu maana watu wanaweza kufanya ghasia.”

Yesu Apakwa Manukato

Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni ambaye aliwahi kuwa na ukoma. Alipokuwa mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia ndani akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu manukato hayo kichwani. Baadhi ya watu waliokuwapo wali chukia wakasema, “Kwa nini anapoteza bure manukato hayo? Si afadhali yangeliuzwa kwa dinari zaidi ya mia tatu na fedha hizo wakapewa maskini?” Wakamkemea huyo mama kwa hasira. Lakini Yesu akawaambia, “Kwa nini mnamnyanyasa? Mwacheni! Amenitendea jambo zuri na jema. Maskini mnao wakati wote na mnaweza kuwapa tia msaada wakati wo wote mtakapo. Lakini hamtakuwa nami wakati wote. Huyu mama amenitendea lile aliloweza. Amenipaka manukato kuniandaa kwa mazishi yangu. Nawaambieni hakika, mahali po pote duniani ambapo Habari Njema itahubiriwa, jambo hili alilo nitendea huyu mama, litatajwa kwa ukumbusho wake.”

Yuda Anapanga Kumsaliti Yesu

10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu kuwaambia kuwa yuko tayari kuwasaidia wamkamate Yesu. 11 Walifurahishwa sana na habari hizi, wakaahidi kumlipa fedha. Kwa hiyo yeye akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti.

Yesu Anakula Pasaka Na Wanafunzi Wake

12 Siku ya kwanza ya sherehe ya Mikate isiyotiwa chachu siku ambayo kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza Yesu, “Unapenda tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?” 13 Aka watuma wanafunzi wawili akawaagiza, “Nendeni mjini. Huko mtaku tana na mwanamume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni, 14 na pale atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anasema hivi, kiko wapi chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’ 15 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichopangwa tayari. Tuandalieni humo.” 16 Wale wanafunzi walikwenda mjini wakakuta kila kitu kama alivyowaambia; wakaandaa chakula cha Pasaka. 17 Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 18 Walipokuwa mezani wakila, akawaambia, “Ninawaam bia hakika, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.” 19 Wote wakasikitika. Wakamwuliza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 20 Akawajibu, “Ni mmoja wenu kumi na wawili, yule anayechovya kipande chake cha mkate kwenye bakuli pamoja nami. 21 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama maandiko yasemavyo. Lakini ole wake yeye atakayenisaliti. Ingelikuwa heri kama hakuz aliwa!”

Chakula Cha Bwana

22 Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru , akaumega akawapa wanafunzi wake akisema, “Pokeeni, huu ni mwili wangu.” 23 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa, wote wakanywa humo. 24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu ya agano, inayomwagwa kwa faida ya wengi. 25 Nawaambieni hakika, sita kunywa tena divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya katika Ufalme wa Mungu.”

26 Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica