Old/New Testament
Yesu Azungumza Tena Kuhusu Kifo Chake
17 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili akawaambia, 18 “Sasa tunakwenda Yerusalemu na mimi Mwana wa Adamu nitatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na walimu wa sheria nao watanihukumu adhabu ya kifo 19 na kunikabidhi kwa watu wa mataifa ambao watanizomea na kunipiga mijeledi na kunisulubisha; na siku ya tatu nitafufuliwa.”
Ombi La Mama Wa Wana Wa Zebedayo
20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akaja kwa Yesu akiwa na wanae, akapiga magoti akamwomba aseme neno.
21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, ruhusu wanangu hawa, waketi mmoja upande wako wa kulia na mwin gine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”
22 Yesu akawaambia, “Hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kuny wea kikombe nitakachonywea mimi?” Wakajibu, “Tunaweza.’ ’
23 Akawaambia, “Kikombe changu mtakinywea. Lakini kuhusu kuketi kulia au kushoto kwangu, sina mamlaka ya kuwaruhusu. Nafasi hizo ni za wale ambao Baba yangu amewaandalia.”
24 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya waliwakasi rikia hao ndugu wawili. 25 Lakini Yesu akawaita wote pamoja aka waambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa mataifa hupenda kuheshi miwa, na wenye vyeo hupenda kuonyesha mamlaka yao. 26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, anayetaka kuwa mkuu kati yenu hana budi kuwa mtumishi wenu. 27 Na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumishi wenu; 28 kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi.”
Yesu Awaponya Vipofu Wawili
29 Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu, walimfuata. 30 Vipofu wawili waliokuwa wameketi kando ya barabara waliposikia kwamba ni Yesu aliyekuwa akipita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 31 Watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao walizidi kupiga kelele wakisema, “ Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 32 Yesu akasimama na akawaita, akawau liza, “Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu, “Bwana tuna taka kuona.”
34 Yesu akawaonea huruma, akawagusa, na mara wakaweza kuona; wakamfuata.
Copyright © 1989 by Biblica