Old/New Testament
Mafundisho Kuhusu Uzinzi
27 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usi zini’. 28 Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwa namke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kulia likikufanya utende dhambi, ling’oe ulitu pilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena. 30 Na kama mkono wako wa kuume ukiku fanya utende dhambi, ukate uutupilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena.
31 “Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’ 32 Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.”
Mafundisho Kuhusu Kuapa
33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”
Mafundisho Kuhusu Kulipiza Kisasi
38 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia; 40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. 42 Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa.”
Wapendeni Maadui Zenu
43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. 47 Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. 48 Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”
Copyright © 1989 by Biblica