Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

New Testament in a Year

Read the New Testament from start to finish, from Matthew to Revelation.
Duration: 365 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Warumi 8:22-39

22 Tunajua kuwa kila kitu alichoumba Mungu kimekuwa kikingoja hadi sasa katika kuugua na uchungu kama wa mwanamke aliye tayari kuzaa mtoto. 23 Siyo uumbaji tu, bali sisi pia tumekuwa tukingoja kwa kuugua na uchungu ndani yetu. Tunaye Roho kama sehemu ya kwanza ya ahadi ya Mungu. Kwa hiyo tunamngoja Mungu amalize kutufanya sisi watoto wake yeye mwenyewe. Nina maana kuwa tunasubiri kuwekwa huru kwa miili yetu. 24 Tuliokolewa ili tuwe na tumaini hili. Ikiwa tunaweza kuona kile tunachokisubiri, basi hilo siyo tumaini la kweli. Watu hawatumaini kitu ambacho tayari wanacho. 25 Lakini tunatumaini kitu tusichokuwa nacho, na hivyo tunakisubiri kwa uvumilivu.

26 Roho hutusaidia pia. Sisi ni dhaifu sana, lakini Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Hatujui jinsi ya kuomba kama Mungu anavyotaka, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa Mungu kwa kuungua kusikotamkika. 27 Tayari Mungu anayajua mawazo yetu ya ndani sana. Na anaelewa Roho anataka kusema nini, kwa sababu Roho huomba kwa ajili ya watu wa Mungu katika namna inayokubaliana na mapenzi ya Mungu.

28 Tunajua kwamba katika kila kitu Mungu[a] hufanya kazi ili kuwapa mema wale wanaompenda. Hawa ni watu aliowachagua Mungu, kwa sababu huo ndiyo ulikuwa mpango wake. 29 Mungu aliwajua kabla hajauumba ulimwengu. Na aliamua hao wangekuwa kama Mwanaye. Na Yesu angekuwa mzaliwa wa kwanza wa watoto wake wengi. 30 Mungu aliwakusudia wao wawe kama Mwanaye. Aliwachagua na kuwahesabia haki pamoja na Mungu. Na alipowahesabia haki, akawapa utukufu wake.

Mungu Huonesha Pendo lake Kupitia Yesu

31 Hivyo tuseme nini juu ya hili? Ikiwa Mungu yuko kwa ajili yetu, hakuna anayeweza kuwa kinyume nasi. 32 Naye alimwacha mwanae ateswe kwa ajili yetu. Mungu alimtoa Mwanaye kwa ajili yetu sisi sote. Sasa kwa kuwa tu wa Kristo, hakika Mungu atatupa mambo mengine yote. 33 Nani atakayewashitaki watu waliochaguliwa na Mungu? Hayupo! Mungu ndiye hutuhesabia haki. 34 Ni nani anaweza kuwahukumu watu wa Mungu kuwa wana hatia? Hayupo! Kristo Yesu alikufa kwa ajili yetu na alifufuliwa kutoka kwa wafu. Na sasa ameketi upande wa kulia wa Mungu na anazungumza na Mungu kwa ajili yetu. 35 Je, kuna kitu chochote kinachoweza kututenga na upendo wa Kristo? Je, ni matatizo au shida au mateso? Ikiwa hatuna chakula au mavazi au tunakabiliwa na hatari au kifo, je mambo hayo yatatutenga sisi kutoka katika upendo wake? 36 Kama Maandiko yanavyosema,

“Kwa ajili yako, tunakabiliana na kifo wakati wote.
    Watu wanadhani hatuna thamani kama kondoo wanaowachinja.”(A)

37 Lakini katika shida zote hizo tuna ushindi kamili kupitia Mungu, aliyetuonyesha upendo wake. 38-39 Ndiyo, nina uhakika kuwa hakuna kitu kinachoweza kututenganisha sisi na upendo wa Mungu, si kifo, maisha, malaika, wala roho zinazotawala. Nina uhakika kuwa hakuna wakati huu, hakuna wakati ujao; hakuna mamlaka, hakuna kilicho juu yetu au chini yetu, hakuna katika ulimwengu wote ulioumbwa, kitakachoweza kututenganisha sisi na upendo wa Mungu ulioonyeshwa kwetu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International