Read the Gospels in 40 Days
Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo
23 Kisha Yesu akawaambia ule umati wa watu pamoja na wana funzi wake: 2 “Walimu wa sheria na Mafarisayo wamechukua nafasi ya Musa, 3 kwa hiyo watiini na kufanya yote wanayowaambia mfa nye. Lakini msifuate matendo yao; kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuwabebesha watu, lakini wao wenyewe hawajaribu hata kunyoosha kidole kuisogeza!
5 “Wao hufanya mambo yao yote ili waonekane na watu. Wanavaa vipande vipana vya ngozi vilivyoandikwa sheria na kurefusha zaidi pindo za mavazi yao ya sala. 6 Wanapenda kukaa viti vya wageni wa heshima karamuni na viti vya mbele katika masinagogi. 7 Hupenda kuamkiwa masokoni na kuitwa ‘Rabi.’
8 “Lakini ninyi msipende kuitwa ‘Rabi’ kwa sababu mnaye rabi mmoja, na ninyi nyote ni ndugu. 9 Na msimwite mtu ye yote hapa duniani ‘baba’ kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni. 10 Hali kadhalika msipende kuitwa ‘mabwana’ kwa maana mnaye Bwana mmoja tu, yaani Kristo. 11 Aliye mkuu kuliko ninyi nyote atakuwa mtumishi wenu. 12 Ye yote anayejikuza atashushwa; na ye yote anayejinyenyekeza atainuliwa.
13 “Lakini ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnafungia watu milango ya Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, wala hamruhusu wale ambao wange penda kuingia waingie. [
14 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnadhulumu nyumba za wajane, na kwa kujionyesha kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.”]
15 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja awe mfuasi wa dini yenu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya astahili kwenda Jehena mara mbili zaidi yenu!
16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mnasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu iliyoko Hekaluni, itambidi atimize kiapo hicho.’ 17 Ninyi vipofu wajinga! Ni kipi kilicho bora zaidi, ni ile dhahabu au ni Hekalu ambalo ndilo linafanya dhahabu hiyo kuwa takatifu? 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyoko madhabahuni itambidi atimize kiapo hicho.’ 19 Ninyi vipofu! Ni kipi bora zaidi, sadaka, au madhabahu ambayo ndio inafanya sadaka hiyo kuwa takatifu? 20 Kwa hiyo mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hiyo madhabahu na vitu vyote vilivyoko juu yake. 21 Na mtu anapoapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na huyo aishie ndani yake. 22 Naye anayeapa kwa mbingu anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.
23 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnatoa fungu la kumi la mnanaa, na bizari na jira; lakini mmepuuza mambo makuu zaidi ya sheria: haki, huruma na imani. Haya mlipaswa kuyafanya bila kusahau yale mengine. 24 Ninyi viongozi vipofu, mnachuja nzi lakini mnameza ngamia!
25 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa ulafi na unyang’anyi. 26 Ninyi Mafarisayo vipofu! Kwanza safisheni kikombe na sahani kwa ndani, ndipo nje patakuwa safi.
27 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28 Hali kadhalika, nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
29 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kupamba makaburi ya wenye haki 30 mkisema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu tusingel ishiriki katika kuwaua manabii !’ 31 Kwa kusema hivyo mnakiri kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32 Haya basi, kamilisheni hiyo kazi waliyoianza baba zenu! 33 Ninyi nyoka, ninyi kundi la nyoka! Mtaepukaje hukumu ya Jehena? 34 Kwa sababu hiyo nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwatundika msalabani, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawatesa toka mji mmoja hadi mji mwingine. 35 Na kwa hiyo damu ya wote wenye haki ambayo imemwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia ambaye mlimwua kati kati ya Patakatifu na madhabahu, itakuwa juu yenu. 36 Nawaambia kweli haya yote yatatokea wakati wa kizazi hiki.”
Yesu Awaonya Watu Wa Yerusalemu
37 “Ninyi watu wa Yerusalemu; mnawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Nilitamani sana kuwakusanya wana wenu kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! 38 Tazama nyumba yenu imeachwa tupu na ukiwa. 39 Kwa maana nawahakikishia kuwa, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema: ‘Amebarikiwa yeye anayekuja kwa jina la Bwana.
Dalili Za Siku Za Mwisho
24 Yesu aliondoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wana funzi wakamwendea ili wakamwonyeshe majengo ya Hekalu. 2 Lakini yeye akawaambia, “Mnayaona haya yote? Nawaambieni kweli, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, yote yatatupwa chini.”
3 Yesu alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni wanafunzi wake walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tueleze, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kuja kwako na mwisho wa dunia?”
4 Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu asije akawadanganya. 5 Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema, ‘Mimi ndiye Kristo’ nao watawapotosha wengi. 6 Mtasikia habari za vita na tetesi za vita, msitishike; kwa maana haya hayana budi kutokea; lakini mwisho utakuwa bado. 7 Taifa kwa taifa na nchi kwa nchi zitapigana. Kutakuwa na njaa na tetemeko la ardhi sehemu mbalim bali. 8 Haya yote yatakuwa kama mwanzo wa uchungu wa uzazi.
9 “Kisha mtasalitiwa, mtateswa na kuuawa na mtachukiwa na watu wa mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Wakati huo, wengi wataacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana, 11 na watatokea manabii wengi wa uongo ambao watawapotosha watu. 12 Kwa sababu uovu utakuwa umeenea sana, upendo wa watu wengi utapoa. 13 Lakini mtu atakayesimama imara mpaka mwisho, ataoko lewa. 14 Na hii Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kama ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utafika.
15 “Mtakapoona lile ‘Chukizo la Uharibifu’ linalozungumzwa na nabii Danieli limesimama mahali Patakatifu - msomaji na aelewe - 16 basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 17 Aliyeko juu ya nyumba asishuke kuchukua vitu vyake ndani. 18 Aliyeko sham bani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 19 Ole wao wanawake watakaokuwa na mimba na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ili mtakapokuwa mnakimbia, isiwe ni kipindi cha baridi au siku ya sabato. 21 Kwa maana kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa na ambayo haitatokea tena. 22 Kama siku hizo zisingepunguzwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angesalimika, lakini kwa ajili ya wale walioteu liwa na Mungu, siku hizo zitapunguzwa. 23 Wakati huo mtu aki waambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa!’ au ‘Kristo yule pale!’ msi sadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu. 25 Angalieni, nawatahadharisha mapema.
26 “Kwa hiyo wakiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msitoke. Au wakisema, ‘Yuko chumbani 27 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea mashariki na kuangaza mpaka magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwangu mimi Mwana wa Adamu. 28 Kwa maana po pote ulipo mzoga, ndipo wakusanyikapo tai.
29 “Mara baada ya dhiki ya wakati huo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake tena, na nyota zitaanguka kutoka mbin guni; nguvu za anga zitatikisika. 30 Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu angani na watu wote ulimwenguni wataomboleza. Nao wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 31 Na nitawatuma malaika zangu kwa sauti kuu ya tarumbeta na watawakusanya wateule wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
32 “Jifunzeni kutoka kwa mti wa mtini. Matawi yake yana poanza kuwa laini na majani kuchipua, mnafahamu kwamba kiangazi kimekaribia. 33 Basi, pia mkiona dalili hizi, fahamuni kwamba amekaribia kurudi, na yu karibu na mlango. 34 Nawaambieni kweli, hakika kizazi hiki hakitapita kabla mambo haya hayajatokea. 35 Mbingu na dunia zitatoweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa
36 “Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni wala Mwana, isipokuwa Baba peke yake. 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.
40 “Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 41 Wanawake wawili watakuwa wanatwanga; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa.
42 “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani ataka pokuja Bwana wenu.
43 “Lakini fahamuni kwamba, kama mwenye nyumba angalifahamu ni saa ngapi za usiku ambapo mwizi atakuja, angalikaa macho asiache nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo ninyi pia lazima muwe tayari kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja saa ambayo hamnita zamii.”
Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu
45 “Basi, ni nani mtumishi mwaminifu ambaye bwana wake amemweka awe msimamizi wa watumishi wengine nyumbani kwake, awape posho yao kwa wakati wake? 46 Heri mtumishi ambaye atakapokuja bwana wake atamkuta anafanya hivyo. 47 Nawaambieni kweli, atam fanya mtumishi huyo asimamie mali yake yote.
48 “Lakini kama mtumishi huyo ni mwovu atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu hatarudi kwa muda mrefu,’ 49 na ataanza kuwapiga watumishi wenzake na kula na kunywa na walevi. 50 Bwana wake atakuja wakati ambapo mtumishi huyo hamtazamii na saa ambayo haijui. 51 Ndipo atamwadhibu huyo mtumishi na kumweka katika kundi la wanafiki; huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.”
Copyright © 1989 by Biblica