Book of Common Prayer
6 Kuishi kwa kumheshimu Mungu, hakika, ni njia ambayo watu hutajirika sana, kwa sababu inamaanisha wanaridhika na walivyo navyo. 7 Tulipokuja ulimwenguni, tulikuja bila kitu, na tutakapokufa hatutachukua chochote. 8 Hivyo, kama tukiwa na chakula na nguo, tutaridhika navyo. 9 Watu ambao wanatamani kuwa matajiri wanajiletea majaribu wenyewe. Wananasa katika mtego. Wanaanza kutaka vitu vingi vya kijinga ambavyo vitawaumiza na kuwaharibu. 10 Kupenda fedha kunasababisha aina zote za uovu. Watu wengine wamegeuka kutoka kwenye imani yetu kwa sababu wanataka kupata fedha nyingi zaidi. Lakini wamejisababishia wenyewe maumivu mengi na huzuni.
Baadhi ya mambo ya Kukumbuka
11 Lakini wewe ni mali ya Mungu. Hivyo kaa mbali na mambo hayo yote, daima jaribu kutenda mema ili umheshimu Mungu na uwe na imani, upendo, uvumilivu, na upole. 12 Tunatakiwa tupigane kutunza imani yetu. Jaribu kwa bidii kadri unavyoweza kushinda vita vya thawabu. Tunza uzima wa milele. Ni uzima mliyouchagua kuupata mlipoikiri imani yenu katika Yesu; huo ukweli wa ajabu mliousema waziwazi kwa wote kuusikia. 13 Mbele ya Mungu na Kristo Yesu nakupa amri. Yesu ni yule aliyeshuhudia ukweli aliposimama mbele ya Pontio Pilato. Mungu ndiye anayetoa uhai kwa kila kitu. Nakuambia haya sasa: 14 Tenda niliyokuamuru kufanya bila dosari au kulaumu mpaka muda atakapo rudi. 15 Mungu atafanya hayo yatokee wakati utakapotimia. Yeye ni mwenye utukufu zaidi na mtawala pekee, mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. 16 Mungu pekee hafi, anaishi katika nuru angavu sana ambayo watu hawawezi kusogea karibu. Hakuna mtu aliyemwona Mungu; wala anayeweza kumuona. Heshima na nguvu ni zake milele. Amina.
17 Wape amri hii wale ambao ni matajiri wa vitu vya ulimwengu huu. Waambie wasiwe na majivuno, bali wamtumaini Mungu wala si katika fedha zao. Fedha haziwezi kuaminiwa, lakini Mungu anatuhudumia kwa ukarimu mkubwa na anatupa vitu vyote ili tufurahi. 18 Waambie wale ambao ni matajiri watende mema. Wawe matajiri katika kuzifanya kazi njema. Na uwambie wawe tayari kutoa na kuwapa wengine vitu. 19 Kwa kufanya hivi, watajiwekea hazina kwa ajili yao wenyewe. Na hazina hiyo itakuwa ni msingi imara huo utakuwa msingi imara ambao maisha yao ya siku zijazo yatajengwa. Wataweza kuwa na maisha yaliyo ya kweli kabisa.
20 Timotheo, Mungu ameweka vitu vingi kwako uvitunze. Uvitunze vyema. Jitenge na watu wanaosema mambo yasiyofaa ambayo hayatoki kwa Mungu na wale wanaokupinga na “elimu” ambayo siyo “elimu” kabisa. 21 Watu wengine wanaodai kuwa na “elimu” wamepotea mbali kabisa kutokana na wanachoamini.
Ninaomba neema ya Mungu iwe kwenu nyote.
Je, Masihi ni Mwana wa Daudi?
(Mt 22:41-46; Lk 20:41-44)
35 Yesu alipokuwa akifundisha katika mabaraza ya Hekalu, alisema, “Inawezekana vipi walimu wa Sheria kusema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 36 Daudi mwenyewe kwa kupitia Roho Mtakatifu alisema,
‘Bwana Mungu alimwambia Bwana Mfalme wangu:
Keti karibu nami upande wangu wa kuume,
nami nitawaweka adui zako chini ya udhibiti wako.’[a](A)
37 Daudi anamwita Masihi ‘Bwana’. Itakuwaje tena Kristo awe yote Bwana na pia mwana wa Daudi?”
Hapo lilikuwepo kundi kubwa la watu liliokuwa likimsikiliza kwa furaha.
Yesu Anawakosoa Walimu wa Sheria
(Mt 23:6-7; Lk 11:43; 20:45-47)
38 Katika mafundisho yake alisema, “Jihadharini na walimu wa Sheria.” Wao wanapenda kutembea huko na huko katika mavazi yanayopendeza huku wakipenda kusalimiwa masokoni, 39 Hao wanapenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa sehemu muhimu zaidi za kukaa katika karamu za chakula. 40 Hawa huwadanganya wajane ili wazichukue nyumba zao na wanasali sala ndefu ili kujionesha kwa watu. Watu hawa watapata hukumu iliyo kubwa zaidi.
Mjane Aonesha Jinsi Ulivyo Utoaji wa Kweli
(Lk 21:1-4)
41 Yesu aliketi mahali kuvuka pale palipokuwepo na sanduku la matoleo, alitazama jinsi ambavyo watu walikuwa wakiweka sadaka zao sandukuni. Matajiri wengi waliweka fedha nyingi. 42 Kisha mjane maskini alikuja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba, ambazo zilikuwa na thamani ndogo sana.
43 Yesu aliwaita wanafunzi wake pamoja na kuwaambia, “Nawaambieni ukweli mjane huyu maskini ameweka sarafu mbili tu. Lakini ukweli ni kwamba ametoa zaidi ya matajiri wote wale.” 44 Kwa kuwa wote walitoa kile cha ziada walichokuwa nacho. Lakini yeye katika umasikini wake, aliweka yote aliyokuwa nayo. Na hiyo ilikuwa fedha yote aliyokuwa nayo kutumia wa maisha yake.
© 2017 Bible League International