Add parallel Print Page Options

Je, Masihi ni Mwana wa Daudi?

(Mt 22:41-46; Mk 12:35-37)

41 Kisha Yesu akasema, “Kwa nini watu husema kwamba Masihi ni Mwana wa Daudi? 42 Katika kitabu cha Zaburi, Daudi mwenyewe anasema,

‘Bwana Mungu alimwambia Bwana wangu:
Keti karibu nami upande wangu wa kulia,
43     na nitawaweka adui zako chini ya mamlaka yako.’[a](A)

44 Hivyo ikiwa Daudi anamwita Masihi, ‘Bwana’. Inawezekanaje Masihi awe mwana wa Daudi?”

Read full chapter

Footnotes

  1. 20:43 chini ya mamlaka yako Kwa maana ya kawaida, “mpaka nitakapowafanya maadui zako kuwa kiti cha kuweka miguu yako”.