Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: 1Sam for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 5:27-42

27 Askari waliwaleta mitume na kuwasimamisha mbele ya baraza. Kuhani mkuu akawauliza. 28 Akisema, “Tuliwaambia msifundishe tena kwa kutumia jina lile. Lakini tazameni mlichofanya! Mmeujaza mji wa Yerusalemu kwa mafundisho yenu. Na mnajaribu kutulaumu sisi kwa sababu ya kifo chake.”

29 Petro na mitume wengine wakajibu, “Ni lazima tumtii Mungu, siyo wanadamu! 30 Mlimwua Yesu kwa kumpigilia msalabani. Lakini Mungu, Mungu yule yule wa Baba zetu, alimfufua Yesu kutoka kwa wafu. 31 Yesu ndiye ambaye Mungu amemtukuza kwa kumpa nafasi upande wake wa kuume. Amemfanya kuwa Kiongozi na Mwokozi wetu. Mungu alifanya hivi ili kuwapa watu wote wa Israeli fursa ya kubadilika na kumgeukia Mungu ili dhambi zao zisamehewe. 32 Tuliona mambo haya yote yakitokea, na tunathibitisha kuwa ni ya kweli. Pia, Roho Mtakatifu anaonesha kuwa mambo haya ni ya kweli. Mungu amemtoa Roho huyu kwa ajili ya wote wanaomtii Yeye.”

33 Wajumbe wa Baraza waliposikia haya, walikasirika sana. Walianza kupanga namna ya kuwaua mitume. 34 Lakini mjumbe mmoja wa Baraza, Farisayo aliyeitwa Gamalieli, akasimama, alikuwa mwalimu wa sheria na watu wote walimheshimu. Aliwaambia wajumbe wawatoe nje mitume kwa dakika chache. 35 Kisha akawaambia, “Wanaume wa Israeli, iweni waangalifu kwa kile mnachopanga kuwatendea watu hawa. 36 Mnakumbuka Theuda alipotokea? Alijidai kuwa alikuwa mtu mkuu, na wanaume kama mia nne waliungana naye. Lakini aliuawa na wote waliomfuata walitawanyika. 37 Baadaye, wakati wa sensa, mtu mmoja aitwaye Yuda alikuja kutoka Galilaya. Watu wengi walijiunga kwenye kundi lake, lakini yeye pia aliuawa na wafuasi wake wote walitawanyika. 38 Na sasa ninawaambia, kaeni mbali na watu hawa. Waacheni. Ikiwa mpango wao ni kitu walichopanga wao wenyewe, utashindwa. 39 Lakini ikiwa ni mpango wa Mungu, hamtaweza kuwazuia. Mnaweza kuwa mnapigana kinyume na Mungu mwenyewe!”

Viongozi wa Kiyahudi wakakubaliana na kile alichosema Gamalieli. 40 Wakawaita mitume ndani tena. Wakawachapa viboko na kuwakanya waache kusema na watu kwa kutumia jina la Yesu. Kisha wakawaachia huru. 41 Mitume waliondoka kwenye mkutano wa Baraza, wakifurahi kwamba wamepewa heshima ya kudharauliwa kwa ajili ya Yesu. 42 Mitume hawakuacha kuwafundisha watu. Waliendelea kuzisema Habari Njema, kwamba Yesu ni Masihi. Walifanya hivi kila siku katika eneo la Hekalu na katika nyumba za watu.

Luka 21:37-22:13

37 Wakati wa mchana Yesu aliwafundisha watu katika eneo la Hekalu. Usiku alitoka nje ya mji na kukaa usiku kucha kwenye kilima kinachoitwa Mlima wa Mizeituni. 38 Kila asubuhi watu wote waliamka mapema kwenda kumsikiliza Yesu katika Hekalu.

Mpango wa Kumwua Yesu

(Mt 26:1-5; Mk 14:1-2; Yh 11:47-53)

22 Ilikuwa karibu ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, inayoitwa Pasaka. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walitaka kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliogopa kile ambacho watu wangefanya.

Yuda Akubali Kuwasaidia Adui wa Yesu

(Mt 26:14-16; Mk 14:10-11)

Mmoja wa mitume kumi na wawili wa Yesu aliitwa Yuda Iskariote. Shetani alimwingia Yuda, akaondoka, akaenda kuongea na viongozi wa makuhani na baadhi ya wakuu wa askari walinzi wa Hekalu. Aliongea nao kuhusu namna ya kumkabidhi Yesu kwao. Makuhani walifurahia sana hili. Wakaahidi kumlipa Yuda pesa ikiwa angefanya hivi. Akakubali, kisha alianza kusubiri muda mzuri wa kumkabidhi Yesu kwao. Alitaka kumkabidhi Yesu kwao wakati hakuna kundi la watu ambao wangeona.

Karamu ya Pasaka

(Mt 26:17-25; Mk 14:12-21; Yh 13:21-30)

Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu[a] ilifika. Hii ni siku ambayo Wayahudi daima walichinja kondoo kwa ajili ya Pasaka. Yesu aliwaambia Petro na Yohana, “Nendeni mkaandae mlo wa Pasaka ili tule.”

Wakamwambia, “Unataka tukauandae wapi?”

Akawaambia, 10 “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mtu amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. Ataingia katika nyumba. 11 Mwambieni mmiliki wa nyumba, ‘Mwalimu anakuomba tafadhali utuoneshe chumba ambacho yeye na wafuasi wake wanaweza kulia mlo wa Pasaka.’ 12 Mmiliki atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilicho tayari kwa ajili yetu. Andaeni mlo humo.”

13 Hivyo Petro na Yohana wakaondoka. Kila kitu kilitokea kama Yesu alivyosema. Na hivyo wakauandaa mlo wa Pasaka.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International