Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: 2Kgs for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 9:10-31

10 Alikuwepo mfuasi wa Yesu katika mji wa Dameski aliyeitwa Anania. Katika maono Bwana alimwita, “Anania!”

Anania alijibu, “Niko hapa, Bwana.”

11 Bwana akamwambia, “Amka na uende katika mtaa unaoitwa Mtaa Ulionyooka. Tafuta nyumba ya Yuda[a] na uliza kuhusu mtu anayeitwa Sauli anayetoka katika mji wa Tarso. Yuko katika nyumba hiyo sasa, anaomba. 12 Ameoneshwa katika maono kuwa mtu anayeitwa Anania anamwendea na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.”

13 Lakini Anania akajibu, “Bwana, watu wengi wameniambia kuhusu mtu huyu. Wameniambia kuhusu mambo mengi mabaya aliyowatendea watu wako watakatifu katika mji wa Yerusalemu. 14 Na sasa amekuja hapa Dameski. Viongozi wa makuhani wamempa mamlaka ya kuwakamata watu wote wanaokuamini wewe.”[b]

15 Lakini Bwana Yesu akamwambia Anania, “Nenda, nimemchagua Sauli kwa kazi maalumu. Ninataka ayahubiri mataifa mengine, watawala na watu wa Israeli kuhusu mimi. 16 Nitamwonyesha yote ambayo lazima atateseka kwa ajili yangu.”

17 Hivyo Anania aliondoka na kwenda nyumbani kwa Yuda. Akaweka mikono yake juu ya Sauli na kusema, “Sauli, ndugu yangu, Bwana Yesu amenituma. Ndiye uliyemwona barabarani wakati ukija hapa. Amenituma ili uweze kuona tena, pia ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Ghafla, vitu kama magamba ya samaki vikaanguka kutoka kwenye macho ya Sauli. Akaanza kuona tena! Kisha akasimama na kwenda kubatizwa. 19 Baada ya kula chakula, akaanza kujisikia kuwa na nguvu tena.

Sauli Aanza Kuhubiri Juu ya Yesu Kristo

Sauli alikaa pamoja na wafuasi wa Yesu katika mji wa Dameski kwa siku chache. 20 Baadaye alianza kwenda katika masinagogi na kuwahubiri watu kuhusu Yesu. Aliwaambia watu, “Yesu ni Mwana wa Mungu!”

21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa. Wakaulizana, “Je, huyu si yule aliyekuwa anajaribu kuwaangamiza watu wanaomwamini Yesu[c] katika mji wa Yerusalemu? Na hakuja hapa ili awakamate wafuasi wa Yesu na kuwarudisha kwa viongozi wa makuhani?”

22 Lakini Sauli aliendelea kuwa nguvu katika kuthibitisha kwamba Yesu ndiye Masihi. Uthibitisho wake ulikuwa na nguvu kiasi kwamba Wayahudi walioishi Dameski hawakuweza kubishana naye.

Sauli Awatoroka Wayahudi

23 Baada ya siku nyingi kupita, baadhi ya Wayahudi waliweka mpango wa kumwua Sauli. 24 Waliyalinda malango ya mji usiku na mchana. Walitaka kumwua Sauli, lakini aliambiwa kuhusu mpango wao. 25 Usiku mmoja baadhi ya wafuasi ambao Sauli aliwafundisha walimsaidia kuondoka mjini. Walimweka katika kikapu, wakamtoa kwa kumshusha kupitia kwenye tundu lililokuwa kwenye ukuta wa mji.

Sauli Katika Mji wa Yerusalemu

26 Kisha Sauli alikwenda Yerusalemu. Akajaribu kujiunga na kundi la wafuasi, lakini wote walimwogopa. Hawakuamini kuwa naye amekuwa mfuasi wa Yesu. 27 Lakini Barnaba alimkubali Sauli, akamchukua na kumpeleka kwa mitume. Akawaeleza namna ambavyo Sauli alimwona Bwana akiwa njiani na namna ambavyo Bwana aliongea naye. Kisha akawaambia namna ambavyo Sauli amehubiri kwa ujasiri kuhusu Yesu katika mji wa Dameski.

28 Sauli alikaa na wafuasi na kwenda kila mahali katika mji wa Yerusalemu akihubiri kwa ujasiri kwa ajili ya Bwana. 29 Kila mara alibishana na Wayahudi waliokuwa waliozungumza Kiyunani,[d] ambao walianza kutengeneza mpango wa kumwua. 30 Waamini walipoujua mpango huu, walimchukua Sauli mpaka Kaisaria, na kutoka huko walimsafirisha mpaka katika mji wa Tarso.

31 Kanisa katika Uyahudi yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, vikundi hivi vya waamini vikawa na nguvu katika imani na kuonesha utii kwa ajili ya Bwana kwa namna walivyoishi. Hivyo kanisa kila mahali liliongezeka kwa idadi.

Luka 3:7-18

Makundi ya watu walimwendea Yohana ili awabatize. Lakini aliwaambia, “Enyi nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia hukumu ya Mungu inayokuja? Badilisheni mioyo yenu! Kisha onesheni ya kuwa mmebadilika kwa namna mnavyoishi. Ninajua mtasema kuwa, ‘Ibrahimu ni baba yetu.’ Hilo halijalishi chochote. Ninawaambia Mungu anaweza kumwumbia Ibrahimu watoto kutokana na mawe haya! Na sasa shoka liko tayari kukata miti,[a] kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.”

10 Watu wakamwuliza Yohana, “Tufanye nini?”

11 Akajibu, “Ukiwa na mashati mawili mpe moja asiyekuwa na shati. Kama una chakula, kigawe pia.”

12 Hata watoza ushuru walikuja kwa Yohana. Walitaka wabatizwe. Walimwambia, “Mwalimu, tufanye nini sisi?”

13 Akawaambia, “Msitoze ushuru zaidi kuliko kiwango kilichoamriwa.”

14 Askari wakamwuliza, “Vipi kuhusu sisi? Tufanye nini?”

Akawaambia, “Msitumie nguvu au kutengeneza mashtaka ya uongo ili watu wawape pesa. Mtosheke na mishahara mnayopata.”

15 Kila mtu alitarajia kuja kwa Masihi,[b] na walijiuliza wakisema, “Labda Yohana ndiye Masihi.”

16 Yohana aliwajibu watu wote, akasema, “Ninawabatiza ninyi katika maji, lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17 Yuko tayari sasa kuja kusafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri na makapi, na kuiweka katika ghala yake kisha ataichoma ile isiyofaa katika moto usiozimika.” 18 Hivi ndivyo ambavyo Yohana aliwahubiri watu Habari Njema. Aliwaonya sana kuwa wanatakiwa kubadili njia zao.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International