Book of Common Prayer
4 Sheria ilifikia mwisho wake wakati Kristo alipolikamilisha kusudi lake. Sasa kila mtu anayeiweka imani yake kwake anahesabiwa haki mbele za Mungu.
5 Musa anaandika juu ya kuhesabiwa haki kwa kuifuata sheria. Anasema: “Ili kupata uzima katika sheria imempasa mtu kuzitii.”(A) 6 Lakini Maandiko yanasema haya kuhusu kuhesabiwa haki kwa njia ya imani: “Usiyaseme haya kwako wewe mwenyewe, ‘Nani atapanda kwenda mbinguni?’” (Hii inamaanisha “Nani atapanda mbinguni kumchukua Kristo na kumleta chini duniani?”) 7 “Na usiseme, ‘Nani atashuka hadi ulimwengu uliopo chini huko?’” (Hii inamaanisha “Nani atashuka chini na kumchukua Kristo na kumfufua kutoka mauti?”)
8 Hivi ndivyo Maandiko yanavyosema: “Mafundisho ya Mungu yako karibu nawe; yako katika kinywa chako na katika moyo wako.”(B) Ni mafundisho ya imani tunayowaambia watu. 9 Ukikiri wazi kwa kinywa chako, kwamba “Yesu ni Bwana” na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua kutoka mauti, utaokolewa. 10 Ndiyo, tunamwamini Yesu mioyoni mwetu, na Mungu hutukubali kuwa wenye haki. Na tunakiri wazi wazi kwa vinywa vyetu kwamba tunamwamini Mungu na yeye anatuokoa.
11 Ndiyo, Maandiko yanasema, “Yeyote anayemwamini hataaibika.”(C) 12 Yanasema hivi kwa sababu hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi. Bwana yule yule ndiye Bwana wa watu wote. Naye humbariki sana kila amwombaye akitaka msaada. 13 Ndiyo, “kila mtu anayemwita Bwana[a] ili kupata msaada, ataokolewa.”[b]
14 Lakini watu watawezaje kumwita Bwana na kupata msaada wake ikiwa hawamwamini yeye? Na watawezaje kumwamini Bwana ikiwa hawajawahi kuzisikia habari zake? Na watawezaje kuzisikia habari zake ikiwa hayupo mtu wa kuwaambia? 15 Na mtu atawezaje kwenda na kuwaambia habari hizo ikiwa hajatumwa? Haya, hii ndiyo sababu Maandiko yanasema, “Ni jambo la kufurahisha kumwona mtu anayepeleka Habari Njema!”(D)
16 Lakini si watu wote walizipokea Habari Njema hizo. Na hii ndiyo sababu Isaya alisema, “Bwana, nani aliyeamini yale tuliyowaeleza?”(E) 17 Kwa hiyo imani hupatikana kutokana na kusikia Habari Njema. Na watu husikia Habari Njema wakati mtu anapowaeleza kuhusu Kristo.
29 Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii, na kuyaheshimu makaburi ya wenye haki waliouawa. 30 Na mnasema, ‘Ikiwa tungeishi nyakati za mababu zetu, tusingewasaidia kuwaua manabii hawa.’ 31 Hivyo mnathibitisha kuwa ninyi ni uzao wa wale waliowaua manabii. 32 Na mtaimalizia dhambi waliyoianza mababu zenu!
33 Enyi nyoka! Ninyi mlio wa uzao wa nyoka wenye sumu kali! Hamtaikwepa adhabu. Mtahukumiwa na kutupwa Jehanamu! 34 Hivyo ninawaambia: Ninawatuma manabii na walimu wenye hekima na wanaojua Maandiko. Lakini mtawaua, mtawatundika baadhi yao kwenye misalaba na kuwapiga wengine katika masinagogi yenu. Mtawafukuza kutoka katika mji mmoja hadi mwingine.
35 Hivyo mtakuwa na hatia kutokana vifo vyote vya watu wema wote waliouawa duniani. Mtakuwa na hatia kwa kumwua mtu wa haki Habili, na mtakuwa na hatia kwa kuuawa kwa Zakaria[a] mwana wa Barakia mliyemwua kati ya Hekalu na madhabahu. Mtakuwa na hatia ya kuwaua watu wote wema walioishi kati ya wakati wa Habili mpaka wakati wa Zakaria. 36 Niaminini ninapowaambia kuwa mambo haya yote yatawapata ninyi watu mnaoishi sasa.
Yesu Awaonya Watu wa Yerusalemu
(Lk 13:34-35)
37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu! Unayewaua manabii. Unawapiga kwa mawe wale ambao Mungu amewatuma kwako. Mara nyingi nimetaka kuwasaidia watu wako. Nimetaka kuwakusanya watu wako kama kuku anavyowakusanya vifaranga wake chini ya mbawa zake. Lakini hukuniruhusu kufanya hivyo. 38 Sasa Hekalu lako litaachwa ukiwa kabisa. 39 Ninakwambia, hautaniona tena mpaka wakati utakaposema, ‘Karibu! Mungu ambariki yeye ajaye katika jina la Bwana.’”(A)
© 2017 Bible League International