Book of Common Prayer
Mungu Amesema Kupitia Mwanaye
1 Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa kuwatumia manabii. Alisema nao mara nyingi na kwa njia nyingi tofauti. 2 Lakini sasa katika siku hizi za mwisho Mungu amesema nasi tena kupitia Mwana wake. Mungu aliuumba ulimwengu wote kupitia Mwana wake. Na alimchagua Mwana kumiliki mambo yote. 3 Huyo Mwana huuonesha utukufu wa Mungu. Yeye ni nakala halisi ya asili yake Mungu, na huviunganisha vitu vyote pamoja kwa amri yake yenye nguvu. Mwana aliwasafisha watu kutoka katika dhambi zao. Kisha akaketi upande wa kuume[a] wa Mungu, aliye Mkuu huko Mbinguni. 4 Mwana akawa mkuu zaidi kuliko malaika, na Mungu akampa jina lililo kuu zaidi kuliko lolote katika majina yao.
5 Mungu kamwe hajamwambia malaika yeyote maneno haya:
“Wewe ni Mwanangu.
Mimi leo hii nimekuwa Baba yako.”(A)
Mungu pia kamwe hajasema juu ya malaika,
“Nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa mwanangu.”(B)
6 Na kisha, pale Mungu anapomtambulisha Mwanaye mzaliwa wa kwanza ulimwenguni,[b] anasema,
“Basi malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.”[c]
7 Hivi ndivyo Mungu alivyosema kuhusu malaika:
8 Lakini hivi ndivyo alivyosema kuhusu Mwana wake:
“Mungu, ufalme wako utadumu milele na milele.
Unatumia mamlaka yako kwa haki.
9 Unapenda kilicho sahihi na kuchukia kilicho na makosa.
Hivyo Mungu, Mungu wako, amekuchagua wewe,
na amekupa heshima na furaha zaidi kupita yeyote aliye kama wewe.”(D)
10 Pia Mungu alisema,
“Ee Bwana, mwanzo uliiumba dunia,
na mikono yako ikaliumba anga.
11 Vitu hivi vitatoweka, lakini wewe utaendelea kuwepo.
Vyote vitachakaa kama mavazi makuu kuu.
12 Utavikunja hivyo kama koti,
navyo vitabadilishwa kama mavazi.
Lakini wewe hubadiliki,
na uhai wako hautafikia mwisho.”(E)
Yesu ni Neno la Mungu la Milele
1 Mwanzoni Kabla ulimwengu haujaumbwa
alikuwepo Neno.[a]
Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu,
na Neno alikuwa Mungu.
2 Alikuwepo pamoja na Mungu
toka mwanzo.
3 Kila kitu kilifanyika kupitia kwake.
Hakuna chochote katika uumbaji wa Mungu
kilichofanyika bila yeye.
4 Ndani yake Neno kulikuwemo na uzima,
na uzima huo ulikuwa nuru
kwa ajili ya watu wa ulimwenguni.
5 Nuru[b] hiyo yamulika gizani,
na giza halikuishinda.[c]
6 Alikuwepo mtu aliyeitwa Yohana, aliyetumwa na Mungu. 7 Alikuja kuwaambia watu kuhusu nuru. Ili kupitia kwake watu wote waweze kusikia kuhusu yule aliye nuru na wamwamini.
Yesu, Mwanakondoo wa Mungu
29 Siku iliyofuata Yohana akamwona Yesu akija kwake na kusema, “Tazama, Mwanakondoo wa Mungu mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu.” 30 Huyu ndiye niliyezungumza habari zake niliposema, “Kuna mtu anayekuja baada yangu aliye mkuu zaidi yangu, kwa sababu yeye aliishi muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwangu.” 31 Nami sikumjua yeye ni nani. Lakini nilikuja kuwabatiza watu kwa maji ili watu wa Israeli waelewe kuwa huyo ndiye Masihi.
32-34 Kisha Yohana akasema maneno yafuatayo ili kila mtu asikie, “Mimi pia sikujua nani hasa alikuwa Masihi. Lakini yule aliyenituma kubatiza aliniambia, ‘Utamwona Roho akishuka na kutua kwa mtu. Huyo ndiye atakayewabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.’ Nami nimeyaona haya yakitokea. Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama njiwa na kutulia juu ya mtu huyu. Hivyo haya ndiyo ninayowaambia watu: ‘Yeye huyo ndiye Mwana wa Mungu.’”[a]
© 2017 Bible League International