Mathayo 5
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mafundisho ya Yesu Mlimani
(Lk 6:20-23)
5 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda kwenye kilima na kukaa chini. Wanafunzi wake walimjia Yesu. 2 Kisha Yesu akaanza kuwafundisha watu kwa akasema:
3 “Heri[a] kwa walio maskini na wenye kujua kwamba wanamhitaji Mungu.[b]
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
4 Heri kwa wenye huzuni sasa.
Kwa kuwa watafarijiwa na Mungu.
5 Heri kwa walio wapole.
Kwa kuwa watairithi nchi.[c]
6 Heri kwa wenye kiu na njaa ya kutenda haki.[d]
Kwa kuwa Mungu ataikidhi kiu na njaa yao.
7 Heri kwa wanaowahurumia wengine.
Kwa kuwa watahurumiwa pia.
8 Heri kwa wenye moyo safi,[e]
Kwa kuwa watamwona Mungu.
9 Heri kwa wanaotafuta amani.[f]
Kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.
10 Heri kwa wanaoteswa kwa sababu ya kutenda haki.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
11 Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi. 12 Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.
Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru
(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)
13 Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yo yote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru inayong'aa ili ulimwengu uweze kuiona. Ni kama mji uliojengwa juu ya kilima unavyoonekana wazi. 15 Watu hawawashi taa na kuificha kwenye chungu. Bali huiweka kwenye kinara cha taa ili nuru iangaze kwa kila mtu. 16 Kwa namna hiyo hiyo mnapaswa kuwa nuru kwa ajili ya watu wengine. Hivyo ishini katika namna ambayo watakapoyaona matendo yenu mema, watamtukuza Baba yenu wa mbinguni.
Yesu Afundisha Kuhusu Sheria ya Musa
17 Msifikiri kwamba nimekuja kuiharibu Sheria ya Musa au mafundisho ya manabii. Sikuja kuyaharibu mafundisho yao bali kuyakamilisha. 18 Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.
19 Kila mtu anapaswa kutii kila amri iliyo katika sheria, hata ile isiyoonekana kuwa ya muhimu. Kila atakayevunja mojawapo ya amri hizi ndogo na kuwafundisha wengine kuzivunja atahesabiwa kuwa ni mdogo sana katika ufalme wa Mungu. Lakini kila anayeitii na kuwafundisha wengine kuitii sheria atakuwa mkuu katika ufalme wa Mungu. 20 Ninawambia, ni lazima muitii sheria ya Mungu kwa kiwango bora kuliko kile cha walimu wa sheria na Mafarisayo. La sivyo, hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
Yesu Afundisha Kuhusu Hasira
21 Mmesikia kuwa hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Usimwue yeyote. Na yeyote atakayeua atahukumiwa.’(A) 22 Lakini ninawaambia, msimkasirikie mtu yeyote kwa sababu mkifanya hivyo mtahukumiwa. Na mkimtukana mtu yeyote, vivyo hivyo mtahukumiwa na baraza kuu. Na ukimwita mtu kuwa ni mjinga, utakuwa katika hatari ya kutupwa kwenye moto wa Jehanamu.
23 Unapokwenda kutoa sadaka yako madhabahuni na ukakumbuka kuwa kuna mtu ana jambo dhidi yako. 24 Unapaswa kuiacha sadaka yako kwenye madhabahu na uende kupatana na mtu huyo. Ukiisha patana naye ndipo urudi na kuitoa sadaka hiyo.
25 Akiwepo mtu anayetaka kukushtaki, patana naye haraka. Jitahidi kufanya hivyo kabla ya kufika mahakamani, hata kama bado mpo njiani. Usipofanya hivyo anaweza kukupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakupeleka kwa walinzi watakaokufunga gerezani. 26 Ninakuhakikishia kuwa hautatoka huko mpaka umelipa kila kitu unachodaiwa.
Yesu Afundisha Kuhusu Uzinzi
27 Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Usizini’.(B) 28 Lakini ninawaambia kuwa mwanaume akimwangalia mwanamke na akamtamani, amekwisha kuzini naye katika akili yake. 29 Jicho la kuume likikufanya utende dhambi, liondoe na ulitupe. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote ukatupwa Jehanamu. 30 Na mkono wako wa kuume ukikufanya utende dhambi, uukate na kuutupa. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote kutupwa Jehanamu.
Yesu Afundisha Kuhusu Talaka
(Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18)
31 Ilisemwa pia kuwa, ‘Kila anayemtaliki mkewe ni lazima ampe hati ya talaka.’(C) 32 Lakini ninawaambia kuwa, kila atakayemtaliki mkewe kutokana na sababu isiyohusiana na uzinzi, anamfanya mke wake kuwa mzinzi. Na kila atakayemwoa mwanamke aliyetalikiwa, atakuwa anazini.
Yesu Afundisha Kuhusu Kiapo
33 Pia, mmesikia hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Unaweka kiapo, usishindwe kutimiza kile ulichoapa kufanya. Timiza kiapo ulichoweka mbele za Bwana.’ 34 Lakini ninawaambia mnapoweka ahadi, msiape kwa jina la mbingu, kwa sababu mbingu ni kiti cha enzi cha Mungu. 35 Na usiape kwa jina la dunia kwa sababu, dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Wala msiape kwa jina la mji wa Yerusalemu, kwa sababu nao ni mali yake Mungu, aliye Mfalme Mkuu. 36 Pia usiape kwa jina la kichwa chako kana kwamba ni uthibitisho kuwa utatimiza kiapo, kwa sababu huwezi kuufanya hata unywele mmoja wa kichwa chako kuwa mweusi au mweupe. 37 Sema ‘ndiyo’ tu kama una maana ya ndiyo na ‘hapana’ tu kama una maana ya hapana. Ukisema zaidi ya hivyo, utakuwa unatoa kwa Yule Mwovu.
Yesu Afundisha Kuhusu Kisasi
(Lk 6:29-30)
38 Mmesikia ilisemwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’(D) 39 Lakini ninawaambia msishindane na yeyote anayetaka kuwadhuru. Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto pia. 40 Mtu akitaka kukushitaki ili akunyang'anye shati, mpe na koti pia. 41 Askari akikulazimisha kwenda naye maili moja,[g] nenda maili mbili pamoja naye. 42 Mpe kila anayekuomba, usimkatalie anayetaka kuazima kitu kwako.
Wapende Adui Zako
(Lk 6:27-28,32-36)
43 Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Wapende rafiki zako(E) na wachukie adui zako.’ 44 Lakini ninawaambia wapendeni adui zenu na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 45 Mkifanya hivi mtakuwa watoto halisi walio kama Baba yenu wa mbinguni. Yeye huwaangazia jua watu wote, bila kujali ikiwa ni wema au wabaya. Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Ikiwa mnawapenda wale wanaowapenda ninyi, kwa nini mpate thawabu toka kwa Mungu? Hata watoza ushuru hufanya hivyo. 47 Na ikiwa mnakuwa wema kwa rafiki zenu tu, ninyi si bora kuliko wengine. Hata watu wasiomjua Mungu ni wakarimu kwa rafiki zao pia. 48 Ninalosema ni kuwa, mkue hata kufikia upendo kamili[h] alionao baba yenu wa Mbinguni kwa watu wote.
Footnotes
- 5:3 Heri Maana yake ni baraka kuu.
- 5:3 maskini … wanamhitaji Mungu Kwa maana ya kawaida, “maskini wa roho”, ama wenye uhitaji wa kiroho.
- 5:5 watairithi nchi Wataurithi ulimwengu ujao yaani ufalme wa Mungu unaokuja.
- 5:6 wenye kiu na njaa ya kutenda haki Kwa maana ya kawaida, “wenye njaa na kiu ya kutenda haki zaidi ya kitu kingine chochote”.
- 5:8 wenye moyo safi Au wenye mawazo safi ama wenye kukusudia mema moyoni, ama wenye nia njema moyoni.
- 5:9 wanaotafuta amani Au “wapatanishi wa watu waliofarakana”.
- 5:41 maili moja Kama kilomita moja na nusu.
- 5:48 kamili Neno “kamilifu”, hapa lina maana “imeendelezwa kwa ukamilifu”, na inaelezea aina ya upendo ambao watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa baba.
Matthew 5
Holman Christian Standard Bible
The Sermon on the Mount
5 When He saw the crowds, He went up on the mountain,(A) and after He sat down, His disciples came to Him. 2 Then[a] He began to teach them, saying:(B)
The Beatitudes
3 “The poor in spirit are blessed,(C)
for the kingdom of heaven(D) is theirs.
4 Those who mourn are blessed,(E)
for they will be comforted.
5 The gentle are blessed,(F)
for they will inherit the earth.
6 Those who hunger and thirst for righteousness are blessed,(G)
for they will be filled.
7 The merciful are blessed,
for they will be shown mercy.(H)
8 The pure in heart are blessed,
for they will see God.(I)
9 The peacemakers are blessed,
for they will be called sons of God.(J)
10 Those who are persecuted for righteousness are blessed,
for the kingdom of heaven(K) is theirs.
11 “You are blessed when they insult and persecute you and falsely say every kind of evil against you because of Me. 12 Be glad and rejoice, because your reward is great in heaven. For that is how they persecuted(L) the prophets who were before you.(M)
Believers Are Salt and Light
13 “You are the salt of the earth. But if the salt should lose its taste, how can it be made salty? It’s no longer good for anything but to be thrown out and trampled on by men.(N)
14 “You are the light of the world. A city situated on a hill cannot be hidden.(O) 15 No one lights a lamp(P) and puts it under a basket,[b] but rather on a lampstand, and it gives light for all who are in the house.(Q) 16 In the same way, let your light shine[c] before men, so that they may see your good works and give glory to your Father in heaven.(R)
Christ Fulfills the Law
17 “Don’t assume that I came to destroy the Law or the Prophets. I did not come to destroy but to fulfill.(S) 18 For I assure you: Until heaven and earth pass away, not the smallest letter[d] or one stroke of a letter will pass from the law until all things are accomplished. 19 Therefore, whoever breaks one of the least of these commands and teaches people to do so will be called least in the kingdom of heaven. But whoever practices and teaches these commands will be called great in the kingdom of heaven.(T) 20 For I tell you, unless your righteousness surpasses that of the scribes and Pharisees, you will never enter the kingdom of heaven.
Murder Begins in the Heart
21 “You have heard that it was said to our ancestors,[e] Do not murder,(U)[f] and whoever murders will be subject to judgment.(V) 22 But I tell you, everyone who is angry with his brother[g] will be subject to judgment. And whoever says to his brother, ‘Fool!’[h] will be subject to the Sanhedrin. But whoever says, ‘You moron!’ will be subject to hellfire.[i](W) 23 So if you are offering your gift on the altar, and there you remember that your brother has something against you, 24 leave your gift there in front of the altar. First go and be reconciled with your brother, and then come and offer your gift. 25 Reach a settlement quickly with your adversary while you’re on the way with him, or your adversary will hand you over to the judge, the judge to[j] the officer, and you will be thrown into prison.(X) 26 I assure you: You will never get out of there until you have paid the last penny![k]
Adultery in the Heart
27 “You have heard that it was said, Do not commit adultery.(Y)[l] 28 But I tell you, everyone who looks at a woman to lust for her has already committed adultery with her in his heart.(Z) 29 If your right eye causes you to sin,(AA) gouge it out and throw it away. For it is better that you lose one of the parts of your body than for your whole body to be thrown into hell.(AB) 30 And if your right hand causes you to sin, cut it off and throw it away. For it is better that you lose one of the parts of your body than for your whole body to go into hell!
Divorce Practices Censured
31 “It was also said, Whoever divorces(AC) his wife must give her a written notice of divorce.(AD)[m] 32 But I tell you, everyone who divorces his wife, except in a case of sexual immorality,[n] causes her to commit adultery. And whoever marries a divorced woman commits adultery.(AE)
Tell the Truth
33 “Again, you have heard that it was said to our ancestors,[o] You must not break your oath, but you must keep your oaths to the Lord.(AF)[p] 34 But I tell you, don’t take an oath at all: either by heaven, because it is God’s throne; 35 or by the earth, because it is His footstool; or by Jerusalem, because it is the city of the great King.(AG) 36 Neither should you swear by your head, because you cannot make a single hair white or black. 37 But let your word ‘yes’ be ‘yes,’ and your ‘no’ be ‘no.’[q] Anything more than this is from the evil one.(AH)
Go the Second Mile
38 “You have heard that it was said, An eye for an eye and a tooth for a tooth.(AI)[r] 39 But I tell you, don’t resist[s] an evildoer. On the contrary, if anyone slaps you on your right cheek, turn the other to him also.(AJ) 40 As for the one who wants to sue you and take away your shirt,[t] let him have your coat[u] as well. 41 And if anyone forces[v] you to go one mile, go with him two. 42 Give to the one who asks you, and don’t turn away from the one who wants to borrow from you.(AK)
Love Your Enemies
43 “You have heard that it was said, Love your neighbor(AL)[w] and hate your enemy. 44 But I tell you, love your enemies[x] and pray for those who[y] persecute you,(AM) 45 so that you may be[z] sons of your Father in heaven. For He causes His sun to rise on the evil and the good, and sends rain on the righteous and the unrighteous.(AN) 46 For if you love those who love you, what reward will you have? Don’t even the tax collectors do the same? 47 And if you greet only your brothers, what are you doing out of the ordinary?[aa](AO) Don’t even the Gentiles[ab] do the same? 48 Be perfect,(AP) therefore, as your heavenly Father is perfect.
Footnotes
- Matthew 5:2 Lit Then opening His mouth
- Matthew 5:15 A large basket used to measure grain
- Matthew 5:16 Or way, your light must shine
- Matthew 5:18 Or not one iota; iota is the smallest letter of the Gk alphabet.
- Matthew 5:21 Lit to the ancients
- Matthew 5:21 Ex 20:13; Dt 5:17
- Matthew 5:22 Other mss add without a cause
- Matthew 5:22 Lit Raca, an Aram term of abuse similar to “airhead”
- Matthew 5:22 Lit the gehenna of fire
- Matthew 5:25 Other mss read judge will hand you over to
- Matthew 5:26 Lit quadrans, the smallest and least valuable Roman coin, worth 1⁄64 of a daily wage
- Matthew 5:27 Ex 20:14; Dt 5:18
- Matthew 5:31 Dt 24:1
- Matthew 5:32 Gk porneia = fornication, or possibly a violation of Jewish marriage laws
- Matthew 5:33 Lit to the ancients
- Matthew 5:33 Lv 19:12; Nm 30:2; Dt 23:21
- Matthew 5:37 Say what you mean and mean what you say
- Matthew 5:38 Ex 21:24; Lv 24:20; Dt 19:21
- Matthew 5:39 Or don’t set yourself against, or don’t retaliate against
- Matthew 5:40 Lit tunic; = inner garment
- Matthew 5:40 Or garment; lit robe; = outer garment
- Matthew 5:41 Roman soldiers could require people to carry loads for them.
- Matthew 5:43 Lv 19:18
- Matthew 5:44 Other mss add bless those who curse you, do good to those who hate you,
- Matthew 5:44 Other mss add mistreat you and
- Matthew 5:45 Or may become, or may show yourselves to be
- Matthew 5:47 Or doing that is superior; lit doing more
- Matthew 5:47 Other mss read tax collectors
© 2017 Bible League International
Copyright © 1999, 2000, 2002, 2003, 2009 by Holman Bible Publishers, Nashville Tennessee. All rights reserved.