Lakini mnyama na nabii wa uongo walikamatwa. Nabii wa uongo ndiye aliyefanya miujiza kwa ajili ya mnyama. Alitumia miujiza hii kuwahadaa wale waliokuwa na alama ya mnyama na walioabudu sanamu yake. Nabii wa uongo na mnyama walitupwa kwenye ziwa la moto linalowaka kwa baruti.
Yule mnyama akatekwa pamoja na yule nabii wa uongo, aliyefanya ishara za uongo, kwa niaba yake, akawadanganya wale waliopokea alama ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.