Alijipa utukufu mwingi na kuishi kitajiri. Mpeni mateso mengi na huzuni nyingi. Kama vile utukufu na starehe aliyoifurahia. Hujisemea mwenyewe, ‘Mimi ni malkia nikaaye kwenye kiti changu cha enzi. Mimi si mjane; Sitakuwa na huzuni.’
Kama yeye alivyojitukuza kwa uasherati wake, mpe mateso na maombolezo kwa kipimo hicho hicho. Kwa kuwa kama ase mavyo moyoni mwake, ‘Mimi naketi kama malkia, si mjane wala sita pata msiba kamwe.’