Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Semicontinuous)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with sequential stories told across multiple weeks.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Jer for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waebrania 3:7-4:11

Tunapaswa Kuendelea Kumfuata Mungu

Ni kama vile anavyosema Roho Mtakatifu:

“Kama leo mtaisikia sauti ya Mungu,
    msiifanye migumu mioyo yenu kama hapo zamani,
mlipomgeuka Mungu.
    Hiyo ndiyo siku ulipomjaribu Mungu mle jangwani.
Kwa miaka 40 jangwani, watu wako wakaona niliyoyatenda.
    Lakini walinijaribu na ustahimilivu wangu.
10 Hivyo nikawakasirikia.
    Nikasema, ‘Mawazo yao siku zote hayako sahihi.
    Hawajawahi kamwe kuzielewa njia zangu.’
11 Hivyo nilikasirika na kuweka ahadi:
    ‘Kamwe hawataingia katika sehemu yangu ya pumziko.’”(A)

12 Hivyo ndugu na dada, muwe makini ili asiwepo miongoni mwenu atakayekuwa na mawazo maovu yanayosababisha mashaka mengi ya kuwafanya muache kumfuata Mungu aliye hai. 13 Bali mhimizane ninyi kwa ninyi kila siku, maadamu mna kitu kinachoitwa “leo.”[a] Msaidiane ninyi kwa ninyi ili asiwepo miongoni mwenu atakayedanganywa na dhambi akawa mgumu sana kubadilika. 14 Tunayo heshima ya kushirikishana katika yote aliyo nayo Kristo endapo tutaendelea hadi mwisho kuwa na imani ya uhakika tuliyokuwa nayo mwanzoni. 15 Ndiyo sababu Roho anasema:

“Kama leo mtaisikia sauti ya Mungu,
    msiifanye migumu mioyo yenu kama hapo zamani,
    wakati mlipogeuka mbali na Mungu.”(B)

16 Ni nani hawa walioisikia sauti ya Mungu na kugeuka kinyume naye? Walikuwa watu wote ambao Musa aliwaongoza kutoka Misri. 17 Na ni kina nani waliokasirikiwa na Mungu kwa miaka 40? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi. Na maiti zao zikaachwa jangwani. 18 Na ni watu gani ambao Mungu alikuwa akisema nao alipotoa ahadi kuwa kamwe wasingeingia mahali penye mapumziko? Alikuwa anazungumza nao ambao hawakumtii. 19 Hivyo tunaona kuwa hawakuruhusiwa kuingia na kupata pumziko la Mungu, kwa sababu hawakuamini.

Na bado tunayo ahadi ambayo Mungu aliwapa watu wake. Ahadi hiyo ni kwamba tuweze kuingia katika sehemu ya pumziko. Hivyo tunapaswa kuwa waangalifu ili asiwepo atakayeikosa ahadi hiyo. Ndiyo, habari njema kuhusu hilo zilielezwa kwetu kama ilivyokuwa kwao. Lakini ujumbe waliousikia haukuwasaidia. Waliusikia lakini hawakuupokea kwa imani. Ni sisi tu tunaoamini tunaoweza kuingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu. Kama Mungu alivyosema:

“Nilikasirika na nikaweka ahadi:
    ‘Hawataingia kamwe kwenye sehemu yangu ya pumziko.’”(C)

Lakini kazi ya Mungu ilikamilika tangu wakati ule alipoumba ulimwengu. Ndiyo, mahali fulani katika Maandiko alizungumza juu ya siku ya saba ya juma. Alisema, “Hivyo katika siku ya saba, Mungu alipumzika kazi zake zote.”(D) Lakini katika Maandiko ya hapo juu Mungu alisema, “Hawataingia kamwe katika sehemu yangu ya pumziko.”

Hivyo fursa bado ipo kwa baadhi kuingia na kufurahia pumziko la Mungu. Lakini waliosikia kwanza habari njema juu yake hawakuweza kuingia, kwa sababu hawakutii. Hivyo Mungu akapanga siku nyingine maalumu. Inaitwa “leo.” Alizungumza juu ya siku hiyo kupitia kwa Daudi siku nyingi zilizopita kutumia maneno tuliyonukuu mwanzoni:

“Kama leo mtaisikia sauti ya Mungu,
    msiifanye migumu mioyo yenu.”(E)

Tunajua kuwa Yoshua hakuwaongoza watu hadi sehemu ya pumziko ambayo Mungu aliwaahidi. Tunalijua hili kwa sababu Mungu alisema baadaye kuhusu siku ya pumziko. Hii inaonesha kuwa pumziko la siku ya saba[b] kwa watu wa Mungu bado linakuja. 10 Mungu alipumzika alipokamilisha kazi yake. Hivyo kila mmoja anayeingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu vilevile atapata pumziko kutoka katika kazi yake kama Mungu alivyofanya. 11 Hivyo hebu na tujitahidi tuwezavyo kuingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu. Tunapaswa kujitahidi ili asiwepo miongoni mwetu atakayepotea kwa kufuata mfano wa wale waliokataa kumtii Mungu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International