Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
9 Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hapana, nimekwishaonyesha kuwa watu wote, wawe Wayahudi au wasio Wayahudi, wako chini ya nguvu ya dhambi.
Watu Wote Wana Hatia
10 Kama Maandiko yanavyosema,
“Hakuna atendaye haki,
hakuna hata mmoja.
11 Hakuna hata mmoja anayeelewa,
hakuna anayetaka kumfuata Mungu.
12 Wote wamegeuka na kumwacha,
na hawana manufaa kwa yeyote.
Hakuna atendaye mema,
hakuna hata mmoja.”(A)
13 “Maneno yao ni ya hatari kama kaburi lililo wazi.
Wanatumia ndimi zao kwa kusema uongo.”(B)
“Maneno yao ni kama sumu ya nyoka.”(C)
14 “Midomo yao imejaa maneno ya laana na hasira.”(D)
15 “Nyakati zote wako tayari kuua mtu.
16 Kila wanakokwenda wanasababisha matatizo na uharibifu.
17 Hawajui jinsi ya kuishi kwa amani.”(E)
18 “Hawamheshimu wala kumcha Mungu.”(F)
19 Tunajua ya kwamba, kile ambacho sheria inasema ni kwa ajili ya wale waliopewa sheria. Hii inamaanisha kuwa watu wote, Wayahudi na wasio Wayahudi, hawana udhuru kwa matendo yao. Hivyo ulimwengu wote unasimama mbele za Mungu na lazima ujibu kwake. 20 Kwa sababu kufuata sheria hakumfanyi mtu akahesabiwa haki mbele za Mungu.[a] Sheria inatuonyesha dhambi zetu tu.
© 2017 Bible League International