Revised Common Lectionary (Complementary)
7 Kristo aliwakaribisha ninyi, hivyo nanyi mkaribishane ninyi kwa ninyi. Hili litaleta heshima[a] kwa Mungu. 8 Ndiyo, haya ndiyo maneno yangu kwenu kwamba Kristo alifanyika mtumishi wa Wayahudi ili kuonesha kuwa Mungu amefanya yale aliyowaahidi baba zao wakuu. 9 Na pia alifanya hivi ili wale wasio Wayahudi waweze kumsifu Mungu kwa rehema anazowapa. Maandiko yanasema,
“Hivyo nitakushukuru wewe katikati ya watu wa mataifa mengine;
Nitaliimbia sifa jina lako.”(A)
10 Na Maandiko yanasema,
“Ninyi watu wa mataifa mengine furahini pamoja na watu wa Mungu.”(B)
11 Pia Maandiko yanasema,
“Msifuni Bwana ninyi watu wote wa mataifa mengine;
watu wote na wamsifu Bwana.”(C)
12 Na Isaya anasema,
“Mtu mmoja atakuja kutoka katika ukoo wa Yese.[b]
Atainuka na kutawala juu ya mataifa,
na wataweka matumaini yao kwake.”(D)
13 Naomba kwamba Mungu aletaye matumaini awajaze furaha na amani kadri mnavyomwamini yeye. Na hii isababishe tumaini lenu liongezeke hadi lifurike kabisa ndani yenu kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
© 2017 Bible League International