Old/New Testament
Yesu Awatuma Wanafunzi Kumi Na wawili
9 Yesu akawaita pamoja wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka na uwezo wa kufukuza pepo wote na kuponya magonjwa yote. 2 Kisha akawatuma waende wakautangaze Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
3 Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha; na msichukue nguo za kubadili. 4 Mkikaribishwa katika nyumba yo yote muwe wageni wa nyumba hiyo hadi mtakapoondoka katika kijiji hicho. 5 Po pote ambapo hamtakaribishwa, mnapoondoka kung’uteni mavumbi miguuni mwenu kama ishara ya hukumu ya Mungu juu yao.”
6 Wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa. 7 Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka!” 8 Wengine wakasema, “Ni Eliya ametutokea” na wengine kwamba, “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” 9 Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?” Akajaribu sana amwone Yesu.
Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
10 Wanafunzi waliporudi walimweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua wakaenda peke yao mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. 11 Lakini watu wengi wakafahamu alipokwenda, wakamfuata. Akawa karibisha, akawafundisha tena kuhusu Ufalme wa mbinguni na akapo nya wangonjwa. 12 Ilipokaribia jioni, wale wanafunzi kumi na wawili wakamwambia Yesu, “Waruhusu watu hawa waondoke ili waweze kujitafutia chakula na mahali pa kulala katika vijiji na mashamba ya jirani kwa maana hapa tuko nyikani.” 13 Akawajibu, “Wapeni chakula.” Wakasema, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili. Unataka tukanunue chakula cha kuwatosha watu wote hawa?” 14 Kwa kuwa walikuwapo wanaume wapatao elfu tano! Lakini Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini-hamsini.” 15 Wakawaketisha wote. 16 Yesu akaichukua mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavi bariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. 17 Kila mtu akala na kutosheka na vilipokusanywa vipande vilivyobaki, vilijaa vikapu kumi na viwili.
Copyright © 1989 by Biblica